Kama EPA!!!!!!!!

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,443
Sentensi niliyo ibold hapo chini nimefananisha na wezi wa EPA, haiwezekani wafanyakazi hewa walipwe mabilioni ya walipa kodi, na solution iwe ni kuwaondoa tu kwenye payrol na si kuwapeleka mahakamani ikiwemo na waliohusika kuwalipa hiyo mishahara feki, kweli Watanzania tuna mzigo wa viongozi.



SERIKALI imepata hasara ya zaidi ya sh.bilioni saba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kutokana na kulipa mishara kwa watumishi hewa, imefahamika. Hayo yalisemwa jana mjini hapa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, wakati wa ufunguzi wa mafunzo juu ya mabadiliko ya utumishi wa umma kwa watumishi wa mkoa wa Kagera.
Alisema hasara hiyo ya sh. bilioni 7.6 ilitokana na kuwalipwa watumishi hewa katika sekta za elimu na afya, kuanzia mwaka 2005 mpaka mwaka jana.
“Hii ilibainika baada ya kufanya uhakiki kwa walimu wa sekondari na watumishi wa afya. Kutokana na ugunduzi huo, tulilazimika kuendelea na uhakiki katika idara ya mahakama na tumeshamaliza na sasa tunafanya katika sekta za kilimo na mifugo,” alisema.
Kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo, Waziri aliwataka waajiri mikoani na halmashauri zote kuondoa mara moja watumishi hewa ambao wamekuwa wakipokea mishahara bila kufanya kazi.


Source: Bilioni 7.6 zalipwa kwa watumishi h
 
Sa wanapoona hakuna udhibiti wowote toka ngazi za juu, ndiyo matokeo!
Hakuna madhara mabaya kama kiongozi wa juu anapokuwa si mfuatiliaji...Tafiti nyingi zinaonyesha hata watu wazuri katika utendaji wasipofuatiliwa kidogo au kutambuliwa kazi zao wanashusha sana productivity, ambapo mojawapo ni kuanza kufanya kazi ya kughushi!
 
aina tofauti na epa yote ni ufisadi utafikiri nchi aina wenyewe hii jamani
 
Back
Top Bottom