Kama Dr. Salim naye akiwa Na kashfa nitajiua

Kama Dr. Salim naye akiwa Na kashfa nitajiua

Maghayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Posts
20,298
Reaction score
47,340
Sijaamini kabisa the humble gentleman jaji Synde anakashfa! Hata Kama tetesi niliposoma tu humu JF nilizimia nakupooza mwili mzima baadaye Leo nikazinduka.

Ila ikitokea sasa Tena kwa huyu jamaa mpemba SAS aliyekuwa bosi huko Addis Ababa Ethiopia naye ana kashfa Basi hamna namna nitatembea uchi siku tatu mfululizo kuichia laana Kali Taifa halafu najiua mtoni nakusombwa Na mafuriko ya mto weruweru.

Kutakua hamna mantiki ya kuishi Tena kwa sababu hawa wawili tu ndio tulijua wasafi.
 
Dah ze Maulid umepotea Sana Yani hata Jimena naye haonekani humu.

Aisee Synde inasemekana anatupiga kwenye Airtel Na Meremeta gold. Niliposoma tu juz kuhusu hizi tetes nilishikwa Na cardiac arrest
Unapoingia kwenye siasa kuna watu watatumia muda, nguvu na rasilimali zao kukujenga na kukupigania, watu hao hutumia nafasi hiyo pia kukuingizia madhaifu ili baadaye waweze kuku blackmail usije ukawageuka.

Kwa nyakati tofauti Salim pia imeshawahi kuwa influencial wa nafasi za juu nchini, amewahi kuchukua form ya kuomba nia ya kugombea urais, jambo ambalo linahusisha mikakati mizito mizito na zaidi amekuwa ni mfanyabiashara wa kipindi kirefu. Hivyo usije ukashangaa kukiibuliwa tetesi juu yake kama alivyovalishwa kashfa na mtandao wa Kikwete mwaka 2005.
Muibuaji wa kashfa mwenyewe ana mikashfa isiyoelezeka yote ni ya kulitia taifa hasara za maana. Suala la TTCL halijaibuliwa kwa bahati mbaya, ingawa nalo litafifishwa kama yale mengine. Warioba anachezea timu ya Mandumila kuwili, mchana anaunga mkono serikali, lakini bendera ya taifa ikishushwa anakuwa kivingine dhidi aliposimamia mchana. Watu wa namna hii hiyo namna nzuri ya kuwapa onyo.
Kuna huyu Prof. Mwandosya amejifanya mgumu sana kugeuza shingo. Ameamua kusimamia anachokiamini na bahati mbaya kitokacho mdomoni mwake huwa na uzito. Huyu naye kupitia TTCL ni kama amepelekewa Kinyesi cha mlevi sebuleni mwake wakati nje kuna wageni wana gonga hodi. Lengo ni ili ahangaike kupambana na mazingira yanayomkabili.
Hivyo kwenye siasa kashfa ni sehemu ya maisha na kwa wanasiasa usiwekeze imani yako.
 
Sijaamini kabisa the humble gentleman jaji Synde anakashfa! Hata Kama tetesi niliposoma tu humu JF nilizimia nakupooza mwili mzima baadaye Leo nikazinduka.

Ila ikitokea sasa Tena kwa huyu jamaa mpemba SHS aliyekuwa bosi huko Addis Ababa Ethiopia naye ana kashfa Basi hamna namna nitatembea uchi siku tatu mfululizo kuichia laana Kali Taifa halafu najiua mtoni nakusombwa Na mafuriko ya mto weruweru.

Kutakua hamna mantiki ya kuishi Tena kwa sababu hawa wawili tu ndio tulijua wasafi.
Yumo enzi hizo aliwahi tamka! Kama kuna mchezo mchafu najitoa! Hakuwahi kujitoa. Na wote wamepata mgawo wa B14.3 alizolipa ttcl kwa airtel ili airtel aondoke ndani ya ttcl.
 
Back
Top Bottom