Kwetu-Mbagala
JF-Expert Member
- Jun 26, 2013
- 203
- 39
Wana-JF kwa kweli inasikitisha sana kwa viongozi/wanachama wa chama chetu tawala kutojitambua.Ukiwafuatilia ktk mikutano yao na pia hata kwenye vikao vyao, wao badala ya kuongelea na kupanga jinsi gani ya kuboresha maisha yetu. Wao wamebaki kuijadili CDM na viongozi/wanachama wake.Hii kamwe haitosaidia kuboresha maisha yetu.Sisi tunataka maendeleo kwanza, hizo siasa zenu baadae.Sasa iwapo CDM ikifa, viongozi/wanachama wa CCM mtakua na lipi kufanya/kuongea? Au huo utakua ndio mwisho wa siasa zenu pia? Acheni maneno na siasa zenu chafu, sisi tunataka maendeleo! Karibuni Mbagala!