Kama CCM yajiamini, mabilioni ya nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama CCM yajiamini, mabilioni ya nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Apr 15, 2010.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Bullet Straton Ruhinda
  Aprili 14, 2010


  NI muda mrefu kidogo sijajitokeza tena kwenye gazeti hili kuandika. Hiyo ni kwa sababu ya kazi nilizokuwa nazifanya nje ya Dar es Salaam, na hivyo kukosa muda wa kuandika makala.

  Leo, nimerudi barazani. Naomba kwa pamoja tutafakari matukio haya mawili. Wiki hii nimevutiwa na matukio makubwa mawili ambayo nimeona si vema kuyaacha yapite hivi hivi bila kujadiliwa.


  Tukio la kwanza ni ujumbe alioutoa Balozi wa Marekani nchini mwetu, Alfonso Lenhardt Mwakilishi huyo wa taifa hilo kubwa duniani alitoa changamoto ambayo sijui viongozi wetu na Watanzania kwa ujumla waliichukulia kwa uzito gani.


  Aliwaambia kwamba alikuwa anashangaa kwa nini nchi yetu ni masikini; ilhali ni miongoni mwa nchi zinazopewa misaada mikubwa sana kutoka Marekani pamoja na nchi nyinginezo za Ulaya.


  Lakini vile vile nchi yetu ina utajiri mkubwa wa maliasili. Mfano alisema kuwa Tanzania inamiliki karibu asilimia kumi na nane ya maji baridi duniani. Lakini pamoja na upendeleo wote huo toka kwa Mungu, bado tu masikini tena wakutupa.


  Ukiacha utajiri wa maji, bado tunayo madini ya kila aina, mbuga za wanyama, ardhi safi, mabonde ya yanayofaa kwa kilimo n.k.


  Balozi huyo wa Marekani aliwaambia viongozi wetu kuwa wasitarajie kwamba maendeleo yatakuja kwa kutegemea misaada.


  Sidhani kama Balozi alikuwa na haja ya kuwaambia viongozi wetu kuwa wasitie matumaini ya maendeleo kwenye misaada; maana ilitakiwa wawe wanalijua hilo tangu mapema sana. Na kama hawalitambui hilo mpaka sasa, basi, ni vema tukubali kuwa hatuna viongozi.


  Hata Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliliweka vizuri katika kazi zake kuwa “Misaada na Mikopo itahatarisha uhuru wetu”.


  Kama kejeli vile Balozi huyo wa Marekani alitoa mfano wa mahitaji ya chakula duniani na kuuliza nchi yetu imejipanga vipi kuchangamkia tenda hiyo ya kuilisha dunia? Hapo nilicheka kidogo maana hata kujilisha wenyewe hatuwezi sembuse kuilisha dunia!


  Sikupata kusoma au kuyasikia majibu ya hao viongozi wetu aliokuwa anawaambia maneno hayo ila nafikiri kwa desturi ya Watanzania, hasa viongozi wetu, nahisi walikuwa wanamshangilia! Sijui ni kushangilia kwa kuelewa alichokiimanisha au kushangilia kwa uzuzu! Mradi siku ipite.


  Hapo ndipo pa kutafakari: je tunao uongozi unaojua malengo na dhamana waliyopewa?


  Kabla vumbi la maneno ya Balozi wa Marekani halijatulia vizuri, chama tawala CCM kikaitisha mkutano mkubwa pale Mlimani City kwa ajili ya uzinduzi wa michango ya kampeni za urais na ubunge.


  Zinatakiwa Shilingi za Kitanzania billioni 40 kwa kampeni tu! Bado najaribu kutafuta mantiki ya kuchangisha pesa zote hizo kwa ajili tu ya kampeni!


  Je kama CCM wanadai wamefanya mambo makubwa kwa nchi katika nyanja zote za maendeleo, kuna haja gani ya kujitangaza kwa mbwembwe na kwa gharama zote hizo?


  Si kila mtu anaona kilichofanyika na kukubali? Kuna haja gani dada kujitangaza kuwa yeye ni mrembo au kaka kuwa yeye ni ‘handsome’? Si watazamaji wanaona na kuamua kuhusu urembo wa mtu?


  Kuna haja gani ya kuingia gharama za bure? Je, ile methali ya “chema chajiuza na kibaya chajitembeza” haina tena maana au tayari imefutwa katika orodha ya methali zetu?


  Kwa nini hayo mabilioni yasitumike kuhamasisha maendeleo? Kwa nini wasitumie mbinu hiyo ya kiuchangishaji kupata Sh. bilioni 40 kwa ajili ya kuboresha shule za kata?


  Kwa nini tusiboreshe zahanati za vijijini na barabara mbovu huko mikoani? Mfano, hivi wana CCM na Watanzania kwa ujumla kwa nini wasichangie ujenzi wa barabara ya Kibondo – Kasulu ambapo magari yanalala kwenye matope kila siku kuliko kupoteza pesa kwa ajili ya kampeni?


  Nitashangaa nikisikia kuwa viongozi wa CCM mkoa wa Kigoma nao walikuwepo katika hafla hiyo! Je CCM pamoja na hayo “maendeleo” iliyoyaleta inahofia nini kwa vyama vya upinzani ambavyo havijajenga hata shule ya chekechea?


  Ukitazama hali hiyo kwa makini utagundua kuwa matangazo na kampeni wakati tunaambiwa “maendeleo” yaliyoletwa yako wazi, ni kuhalalisha uongo. Maana yaelekea CCM hawaamini kama kweli wameleta “maendeleo” wanayoyasema.


  Sioni sababu ya mtu mzima mwenye nguvu na akili na umri wa miaka 40 amuogope na kutishika na mtoto wa miaka kumi. Kwa hali hiyo, lazima mtu huyo ana walakini!


  Nikichanganya hoja ya kwanza na ya pili, najiuliza swali; je katika aliyozungumzia Balozi wa Marekani hakuna kiongozi wa CCM au wa Serikali ya CCM, mwenye ubavu wa kujibu hoja za Balozi? Nahisi hakuna; maana alichozungumza Balozi Lenhardt ni ukweli mtupu.


  Nionavyo, tatizo letu la msingi ni kutokujua ni nini kipaumbele chetu cha maendeleo. Ilivyo sasa vipaumbele vyetu havina tija. Ni kampeni, kununua mashangingi n.k.


  Kama kipaumbele ni kampeni ili CCM kirudi madarakani, tutegemee maendeleo gani? Kama tunachanga Sh. bilioni 50 kwa kampeni tu, lakini hatuwezi kuchanga hata Sh. milioni 50 tu kwa ajili ya maabara ya shule ya kata, tunategemea maendeleo gani?


  Kama kiongozi anaweza kuwahamasisha wananchi wachange Sh. bilioni 40 za kampeni, lakini akipata uongozi anakwenda Marekani kuomba msaada wa Sh. bilioni hizo hizo 40, tutegemee nini?


  Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt bado ana kazi ya ziada kuchambua kwa nini Tanzania hatuendelei; maana yaelekea wenyewe tumeridhika!
   
 2. Ngomo

  Ngomo Senior Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 199
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ccm wanatapatapa hii inasikitisha sana. Bilioni arobaini ni kiwango kikubwa cha pesa kuweza kujenga chuo kikuu kingine katika mojawapo ya mikoa ya nchi yetu; matumizi ya kampeni yanatija gani katika taifa letu. Bora uchaguzi usiwepo kuliko kuwa na viongozi ambao hawa wajibiki kwa jambo lolote lile
   
 3. Ngomo

  Ngomo Senior Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 199
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ccm wanatapatapa hii inasikitisha sana. Bilioni arobaini ni kiwango kikubwa cha pesa kuweza kujenga chuo kikuu kingine katika mojawapo ya mikoa ya nchi yetu; matumizi ya kampeni yanatija gani katika taifa letu. Bora uchaguzi usiwepo kuliko kuwa na viongozi ambao hawa wajibiki kwa jambo lolote lile
   
 4. l

  libaba PM Senior Member

  #4
  Apr 15, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hoja ni nyepesi saana , CCM inarise fund wakiwa na lengo moja tu, kununua kura ...naamini CCM katika uwanja sawa haina ubavu wakushinda chaguzi kwa kishindo kama ilivyotokea 2005, wanahonga mawakala wa upinzani, wanahonga waiga kura, wanatumia ujinga wa Watanzania kuwapitisha na kushinda chaguzi
   
 5. C

  CLAY KITUMBOY Senior Member

  #5
  Apr 15, 2010
  Joined: Sep 8, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku ya mwisho hata jiwe litasema.
   
 6. MANI

  MANI Platinum Member

  #6
  Apr 16, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  "CHEMA CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA" Kama umefanya mema na unakubalika kama Makamba anavyodai sidhani kama kweli utahitaji nguvu ya pesa kiasi hicho urudi madarakani. Wananchi wangapi wamedhulumiwa na serekali hii, kipawa watu wamefunjiwa kwa fidia ndogo,mbagala kuna walioathirika na mabomu na fidia mpaka leo ni ndoto,wafugaji waliohamishwa kwenye bonde la Ihemi na kupigwa faini za ajabu na watendaji wa vijiji,madai ya wafanyakazi na walimu amabayo kila uchwao yanaahirishwa bila kupatiwa ufumbuzi, hawa wote bila kuwalainisha unategemea watakupa kura ya kurudi madarakani. Ndio sababu ya kutafuta hizo bilioni 40.
   
 7. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  nimekuwa nikijiuliza suwala hili kwa muda sasa! Eti wanasema vichwa vinawauma kuwa mabilioni hayo bado hayawatoshi. Ccm waelewe kuwa wanachofanya ni kutuonyesha kuwa pesa ni kila kitu kwao.
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  CCM hai-raise fund. Katika nchi masikini kama TZ huwezi ku-raise billioni 40 ni uongo. Wanachofanya ni kutumia dhamana waliyopewa kutumia fedha za walipa kodi ili kuendelea kubakia madarakani. Nimesikitika sana na michezo wanayoifanya. Juzi wamezima vipaza sauti kwa makusudi pale bungeni halafu wanaunda tume ya kuchunguza sababu, withing 24 hours wanakuja na solution ya kununua mtambo mpya?, Kweli CCM kweli!!, Kwa nini mnawahadaa watanzania?. Hapo hakuna cha mtambo mpya wala nini fungu linatoka na kelekea kwenye kampani then linaandikwa mtambo mpya, na miradi ningine mingi kama hii ndiyo CCM wanayoitumia kuihujumu nchi.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. m

  magee Senior Member

  #9
  Apr 16, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wapo wachache mno na wamebinywa mno na kusahau dhamana zao.......hawawezi fanyalolote na tatizo kubwa ni kwamba mind za viongozi karibia wote zimekuwacorrupted na macho yao yamepofuka!!!!
   
 10. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Hivi na Arumeru zimechangwa billion ngapi?
   
Loading...