GE2025 Kaliua yanunua mtambo wa shilingi bilioni 1.2 wa kutengeneza barabara, siku zote walikua wapi wanategea tukikaribia uchaguzi?

GE2025 Kaliua yanunua mtambo wa shilingi bilioni 1.2 wa kutengeneza barabara, siku zote walikua wapi wanategea tukikaribia uchaguzi?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Wakuu

Hii mitambo ya kutengeneza barabara inanunuliwa sana kipindi hiki kuelekea uchaguzi, siku zote wanakuwa wapi? au ndo kura zinatafutwa kwa kuhadaa wananchi. Alafu mtambo huo huo baada ya uchaguzi utakuta unaharibika:AAAA:
=====

Mbio za Mwenge wa Uhuru umezindua mtambo wa kutengeneza barabara (Motor Grader) wenye thamani ya shilingi bilioni 1.2 ambao utatumika kwenye shughuli za ujenzi na ukarabati wa barabara katika wilaya Kaliua iliyopo mkoani Tabora.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dk. Gerald Mongela, amesema mtambo huo utawezesha barabara za wilaya hiyo kupitika katika kipindi chote.

“Kama unavyofahamu wilaya yetu idadi kubwa ya wananchi wake wanajishughulisha na kilimo, hivyo mtambo huu utafungua barabara hadi zile za mashambani kuwawezesha wananchi kusafirisha mazao yao hususan tumbaku bila kikwazo,” amesema Dk. Mongella.

IMG-20250729-WA1190.jpg
IMG-20250729-WA1189.jpg
IMG-20250729-WA1186.jpg
IMG-20250729-WA1188.jpg
 
Yaani mbio za mwenge zimezindua mtambo??
Hizo gari zote hapo zimeenda kwa ajili ya kuzindua mashine??
 
Back
Top Bottom