Mlenge
Kuhusu vijana, kuna tatizo kidogo la ku-navigate au ku-infiltrate into the system
Siku zote serikali hasa za nchi masikini ni bureaucracy tu inayoendelea.
Kijana atengeneze mfumo utakaotumika na private sectors au individuals, pressure italazima urasimu ubadilike. Zamani cellphone haikuwa katika malipo ya serikali, pressure imeruhusu mfumo huo
Kuhusu malipo kwa mabunda ya pesa a risti za benki, pamoja na kupoteza muda mwingi sana kwa jambo la dakika 10 kuna hasara nyingi sana zinazopatikana.
Mfano, ni rahisi sana kujua senti imeingia wapi na imetokaje ukiwa na mfumo wa elektroniki
Kijana wa kizungu alikuwa anaiba senti 5 ya dola kutoka account za wateja kwa njia elektroni, kwamba kila saa 6 usiku account zinaingiza pesa kwake.
Wateja hawakujua kwasababu senti 5 ilionekana kama charges za benki. Walifuatilia account baada ya kuona imeona hakikuchukua saa, walimbaini. Ndivyo wanavyoweza kubaini monye laundering etc
Kwa sisi Tanzania tumerudi nyuma sana. Kwa wale wa miaka iliyokwenda lol, zamani malipo yalifanywa kwa money order. Unakwenda posta yoyote unalipa unafikisha kopi. Yaani miaka hiyo kumbuka!
Katika wakati wa teknolojia eti watu wanatumia siku nzima utafuta risiti.
Yaani ni rahisi kutibiwa kuliko kupata risiti ya malipo.
Huko bank nako teknolojia imebaki gizani. Hivi mtu anasimamaje bank kwa dakika 10?
electronic chip zinafanya nini. Bado watu wanafungua makaratasi kubaini account ya mtu!
Baada ya kutoka jasho bank unapanga foleni ya kuwasilisha risiti.
Hivi kwanini katika ubutu wetu wa kufikiri kwanini usipowepo mfumo wa copier machine lango la kuingilia, mtu anapigiwa copy na mhuri anaondoka. I mean pamoja na udwanzi/uzezeta wetu hata hilo halituwezi!
Foleni kuanzia kwa mhasibu, wakati mwingine amekwenda kula chapati na maarage, imepita mbele ya ofisi ya mkurugenzi wa fedha, naibu katibu mkuu hadi afisa tawala kwenda nganzi za chini karibu na choo cha akina baba mkabala na ofisi ya afisa maduhuli
Ukiuliza ni ya nini unaambiwa watu wanawasilisha risiti kutoka bank. Mwaka 2018!!!