Kalamu ya Baba Askofu Benson Kalikawe Bagonza

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
5,636
8,774
Kalamu ya Baba Askofu Benson Kalikawe Bagonza

NDOA INAHITAJIKA...

Inahitajika ndoa ya dharula ILI maisha yarejee katika hali ya kawaida. Maharusi ni Bwana NGUVU na Bi HEKIMA. Kwa nini ndoa? Jibu ni, ili tuweze kujibu maswali mawili:

1. Kwa nini watu waandamane?
2. Kama wakiandamana, kwa nini
wapigwe?

TUTAFAKARI

1. Mtihani wa Taifa wa darasa la nne ukiwa unaendelea, ikatokea karatasi ya mtihani ikakutwa inafungia vitumbua mtaa wa pili, mtihani unafutwa. Aliyechapa mtihani anakamatwa na kuhojiwa. Muuza vitumbua anakamatwa na kuhojiwa.

Chukulia mtihani wa mwisho wa madaktari na marubani ukivuja au kusingiziwa kuvuja. Utawaacha madaktari hawa waende kupasua wagonjwa au marubani wakarushe ndege?

Karatasi za kura ni nyaraka nyeti. Ni kama risasi. Ikipotea moja toka stoo isijulikane iko wapi, kila kitu kinasimama. Huwezi kujua hiyo risasi itatokezea wapi? Aliyechapa karatasi zetu za kura anaweza kutumiwa kuvuruga nchi. Kwa nini zizagae zagae? Tusikimbilie kuwalaumu wanaoandamana wala kukimbilia kutumia nguvu na mabomu yetu kwa kinachohitaji ndoa kati ya matumizi ya nguvu na matumizi ya hekima.

Nitajibiwa kuwa waandamanaji wanavunja sheria kuandamana kwa amani kudai risasi iliyopotea ipatikane isije ikaingiza nchi katika msiba mkubwa. Wanaonijibu wangetuonyesha risasi iko wapi. Wangetuambia madaktari hawa waliovujishiwa mtihani wanafaa kutibu wagonjwa wetu? Marubani hawa waliofanya mtihani uliovuja watarusha ndege zetu. Tutazipanda ndege hizi? Zitatufikisha?

Mzee Msekwa anasahau tu. Bunge la chama kimoja wakati wa Kambarage wagombea wa ubunge walikuwa wawili kwa alama za NYUMBA na JEMBE. Mijadala ndani ya Bunge ilikuwa mikali na vijijini tulijadili kipi bora kati ya nyumba na JEMBE.

Wanaowatukana mabalozi, wanaokamata wapinzani na kuwaweka ndani wanaongeza msiba kwa Taifa. Kuna mahali tumejikwaa. Wenye hekima wanasema "ukishindwa kuwa mwaminifu basi jitahidi uwe mwangalifu". Haki ya mtu kulia anapoumia haitolewi wala kuondolewa na katiba. Ni takwa la Muumba kwa viumbe wote. Pigeni lakini msizuie watu kulia.

Wengine hatujasahau, Kuna wakati tulikuwa tunabembelezwa kuandamana. Haya ni maoni yangu, nawe una yako. Tujitahidi kuhudhuria harusi ya Bw. NGUVU na Bi HEKIMA.
 
Back
Top Bottom