Kala Pina: Nimepoteza fedha nyingi sana kumsaidia Chid Benz

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059


Msanii Kala Pina akihojiwa na E News ya EATV amesema ametumia fedha nyingi sana kumsaidia Chid Benz ila anasikitika juhudi zake hazijazaa matunda na kusema angepata msaada zaidi angefanikiwa pakubwa
Amesema yeye ndie aliyemshawishi Chid kujiunga na Sober House na angepata msaada wa kuwa na Sober House yake mwenyewe angemponyesha na kuponyesha waathirika wengi
Ameendelea kusema tatizo la dawa za kulevya ni vijana wengi na sio Chid Benz tu hivyo nguvu zinahitajika
 
Kuna Siri nzito Juu ya hivi Vilevi...
Pombe inaingizia sana kipato serikali
Sigara inaingizia sana kipato pia..

Kuhusu madawa ya kulevya, wapo watu wenye nguvu serikalini wanafaidika, tena Directly na ndio maana hata misaada na juhudi zao juu ya kutokomeza ni za kinafiki sana..

Let's wait and see where we are suppose to be in future
 
Kalapina%20.jpg


Rapa Kalapina ambaye pia ni mwanaharakati wa kuwasaidia watu walioathirika na matumzi ya dawa za kulevya amefunguka na kumtaja mama yake mzazi Chid Benz kama mtu anayemuendekeza Chid na kumfanya asitoke kwenye matumizi ya dawa za kulevya.

Kalapina amesema mama huyo anampenda sana mtoto wake na amemlea kwa kumdekeza kupita kiasi na kumtetea kwa kila jambo kiasi cha mtoto kujua na kuona kwamba hata akifanya jambo fulani yupo mama yake ambaye atasimama na yeye.

Kalapina alisema hayo jana kupitia kipindi cha Planet Bongo na kusema wazazi wengi wamekuwa chanzo cha watoto wao kuingia kwenye matumzi ya dawa za kulevya na kuingia hata kwenye mahusiano ya jinsi moja sababu ya wazazi wamekuwa wakiwadekeza sana watoto au kuwapa uhuru mkubwa na kuruhusu maisha ya uzungu kutawala.

"Kiukweli mama yake mzazi Chid Benz anampenda sana mwanaye na hali hiyo inampelekea mdogo wangu yule kuona hata nikizingua mama atanitafuta tu, au kuona mama atasimama na yeye tu sababu mama yake anampenda sana, lakini siyo Chid Benz tu wazazi wengi wanawalea watoto kwa kuwadekeza sana, wazazi hawana muda na watoto na hili linachangia vijana kuingia kwenye madawa ya kulevya hata kwenye ushoga pia.
Sisi wazazi wetu zamani ulikuwa ukizingua unapigwa sana hivyo lazima utanyooka tu" alisema Kalapina
 
Kwa mdogo wangu pia baba mmoja ila mama tofauti ilimpelekea hadi dogo akachukua maamuzi ya kujinyonga, ilifikia kipindi dogo alikuwa anavunja sheria sana kuvuta uku akiendesha gari, kuvuka kwenye traffic lights bila kufuata sheria ila mama yake akikamatwa tu kafika fasta
 
Sasa mama ambebe miezi tisa tumboni ,amlee tokea hajui kusema anaumwa mpaka anakuwa jibaba ,Sio kwamba mama anafurahia anayopitia mwanae ila anasimama naye katika hali zote akiwa hai hapa duniani

Nina mama wa aina hiyo mbona mimi sivuti madawa ?
 
"toto baya zuri kwa mama yake"

hata uwe mbaya vp kwa jamii bado mama atakuona kama malaika

nilikuwaga mtukutu san pale keko enzi za utotoni lakin mama alipenda kuniita mtoto mpole

nlikuwa kilaza sana dalasan ila mama aliniita akili nying

nlikuwa mkolofi na kibuli ila father alipenda kuniita askal mtiifu

NB:kabla hatujalaumu wazaz haswa mama tutambue mama ana uchungu na huyo mtoto kuliko ww ila ni nature tu yao ya umama(mother&child bond)inawafanya wanashindwa kuwa na reaction kama yako wanajikuta wanafanya hayo!!!,
hata mm nina kijana wangu mtukutu sana,kila kukicha ni kesi za kupiga wenzake,nanunua daftal za shule kila kukicha maana akikaslika huzichana,namkong'ota kila siku ila bado nabaki kumpenda sana maana ni mwanangu na sijawah kuwaza kumpeleka kuishi mbal na mm either boarding au kwa shangaz zake

R.I.P mama...love yu
 
Kile kipindi cha Kalapina mbona sikioni tena, au wadhamini wamegoma?
 
Sasa mama ambebe miezi tisa tumboni ,amlee tokea hajui kusema anaumwa mpaka anakuwa jibaba ,Sio kwamba mama anafurahia anayopitia mwanae ila anasimama naye katika hali zote akiwa hai hapa duniani

Nina mama wa aina hiyo mbona mimi sivuti madawa ?
Hayo si malezi mazuri, hayajengi hata kama mtoto hatumii dawa si sahihi kudekezwa badala ya kufundishwa na kuelezwa misingi mizuri ya maisha!
 
Hayo si malezi mazuri, hayajengi hata kama mtoto hatumii dawa si sahihi kudekezwa badala ya kufundishwa na kuelezwa misingi mizuri ya maisha!
Ni kweli sio malezi mazuri kwako ,ila kwangu ni mazuri is there a problem Sir ?
 
The broblen is spare the rod, spoil the child!
Aint no spoiled kid ,My mother was always there for me ,on my worst situations to the best of my situations ,
If you call that something else its ok cause you are entitled to your opinions ,to me that is unconditional LOVE
 
Ukiusikiliza wimbo wa dear mama wa 2pac kwa haraka haraka madhara yake ndio hawa kina rashidi mama ana mapenzi makubwa kwa mwanae hiyo ni kawaida lakini mtoto anachezea moto badala ya kumkanya kwa kumkazia sauti unaleta mahaba matokeo yake ndio haya .
Hakuna mzazi apendae mwanae aharibike ila mzazi anacheza nafasi gani tusishikirie tu "tikiti bovu limo shambani mwako "
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom