Kakonko, Kigoma: Daktari ajiua kwa kujinyonga na taulo

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
kifo+pic.jpg
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kakonko, mkoani Kigoma , Mejo Banikira (43) amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia taulo yake.

Hayo yamebainishwa leo Mei 29 na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala wakati akizungumza na wanahabari.

Ndagala amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha daktari huyo kujiua.

“Mwili wa Dk Banikira umeondolewa nyumbani alikojinyongea na kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Kibondo wakati jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi,” amesema.

Amesema taarifa za kujinyonga zimepatikana asubuhi baada ya mke wake anayeishi kwingine, kupiga simu kwa muda mrefu bila kupokewa.

“Alipoona simu haipokewi, aliwapigia majirani ambao walikwenda na kukuta milango imefungwa, wakaripoti polisi na polisi ndiyo waliobaini mwili wake,” amesema Ndagala.

" Watu wasichukulie kujinyonga kuwa suluhisho la matatizo katika familia bali waeleze masahibu yao kwa marafiki na viongozi waweze kusaidiwa na kurejea maandiko ya misikitini au makanisani,"amesema Ndagala.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Joseph Tutuba amesema marehemu alikuwa akiishi peke yake katika nyumba za kupanga mjini Kakonko na alikuwa amewasili kituoni hapo miezi minane iliyopita akitokea wilayani Simanjiro.

Chanzo: Mwananchi
 
View attachment 789095

Why always conclusion ya amejinyonga inafikiwa kabla ya uchunguzi???
 
Maisha yanapokuwamagumu watu huchukua maamuzi ya kijinga sana,
hata hivyo, msongo wa mawazo, hasira na upweke inaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kisaikolojia kwa binadamu.
Ni wakati sasa umefika kuwe na vituo vya kutoa ushauri nasaha. Jamii isichukulie poa kabisa haya yanayotokea. Tuanzishe kampeni ya "njoo tuzungumze!!"
 
Back
Top Bottom