Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,074
- 34,844
Wednesday, March 10, 2010 10:27 AM
MKUU wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Mchungaji Zachary Kakobe, amesema umeme unaopitishwa sasa kanisani kwake hautafanya kazi ipasavyo kwa maombi atakayofanya na anaamini umeme hautawaka kwa nguvu ya Mungu kwa vile hakuna nguvu zita Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Askofu Kakobe alisema ameshangazwa na kauli ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kuutangazia umma kuwa ameridhia umeme huo kupitishwa kwenye kanisa hapo.
Alisema kwa kuwa serikali imekaidi agizo lake na yeye hana uwezo wa kukataa maamuzi hayo basi atacha ujenzi uendelee lakini hakuna umeme utkaofanya kazi mahalai hapo kut okana na maombi atakayoungurumisha kanisani hapo kupinga kupitihswa kwa ueme huo hapo.
Huu ni uonevu wa hali ya juu, sijakubaliana na maamuzi hayo kwa kuwa vipimo vyote vilivyotolewa havikuwa vya kweli, vilikuwa ni vya kughushi na ndio mana sikukubaliana na Waziri Ngeleja alivyotoa taarifa yake alisema Askofu Kakobe.
Alisema hivi sasa amegundua hawatakiwi kupinga upitishaji wa umeme huo kimwili kama walivyokuwa wamefanya huko siku za nyuma bali ni kutakiwa kukaa katika maombi kupinga suala hilo na hataweza kubishana na watu wasiomtambua Mungu.
Alisema hivi sasa amepata taarifa za uhakika kuwa baadhi ya watu wamepewa taarifa kuwa wanatakiwa kuhama katika eneo hilo kupisha upitishaji wa nguvu hiyo ya umeme kitendo ambacho kinampa ishara kuwa kuna mpango wa kanisa lake kuvunjwa.
Askofu Kakobe alipingana na madai yaliyotolewa na Mshauri Mtaalam wa Kampuni ya BICO, kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linatakiwa kuepukana na kona kali kwenye waya na kutounganisha sehemu yoyote kati ya nguzo namba 18 na 19.
Nakwambia hata wakipitisha umeme huu hapa hautawaka kwa vile nguvu ya Mungu itashinda nguvu ya umeme lakini kibaya nimesikitishwa na Waziri Ngeleja kuutangazia umma eti nimekubali umeme upitishwe hapa, nasema siyo kweli jamani, alisema Askofu Kakobe.
http://javascript<b></b>:__doPostBack('LinkButton3','')