People, u have to talk MATERIAL, na sio porojo!
Ongeeni kilichotokea, na si kuripoti tu vitu pasi na kufanya rejea!
Kwa waliokuwa makini kufuatilia hili suala, Kakobe amesimama Firm KABISA kutetea maslahi ya kanisa lake hadi dakika ya mwisho ambapo MUAFAKA umefikiwa kati yake na Waziri Ngeleja.
Actually hii ndo SPIRIT ambyo Wabongo wote tunatakiwa kuwa nayo kila uchao.
Kakobe ameweza kuwa na Msimamo wa juu kabisa na kuifanya serikali ifikirie mara ya pili, na hatimaye kutuma ujumbe wake ukiongozwa na waziri!...Hata hivyo, waliotazama mchakato huo siku hiyo, ni kwamba ilibidi waziri na Kakobe waingie mahali pa faragha ili kuongea kwa ukaribu kabisa, ndipo muafaka ulipatikana!
Mikataba ya kishenzi inaingiwa na serikali, wabongo kimyaaa!
Watu wanachukua vijisenti serikalini, wabongo kimyaa, mbaya zaidi wanawalaki watu hao wezi kama mashujaa!
KAKOBE umeonyesha kwamba mambo haya yanawezekana, na serikali iko kwaajili ya kuwatumikia watu kwa njia ya kusikilizana nao, na si kuwaburuta!
BIG-UP KAKOBE!