Kakobe aeleza mambo matatu ya msingi ili Uchaguzi uwe huru na wa haki

Duuh, Shukamoo Kakobe na asante sana kwa Ujumbe uliotukuka natamani Wasaidizi wa Kikwete ama yeye mwenyewe wapite hapa wachukue ujumbe huu mwanana.

Naam "Hatuchagui kiongozi wa kutujengea Makanisa au Misikiti..!!! Hatuchagui kiongozi wa kutupeleka Mbinguni bali kutuondolea umasikini..!!? Wasije wakatuambia ati huyu ni Chaguo la Mungu, Mungu hatuchagulii kiongozi wala Mke"!!

Asante sana Kakobe. Laiti maneno ya hapo juu yangekuwa kichwani mwa kila mmoja wetu, Ninaamini Kikwete asingekuwa kiongozi wa nchi hii.

BACK TANGANYIKA
 
Hiyo ni sauti ya mungu,na watu wanyamaze.ole wake akataaye mananeno bora agefungiwa jiwe kubwa akatupwa baharini
 
Amesha sema mtumishi wa Bwana wizara haita kaa itulie sababu ya laana.sasa serikali inafanyaje?
 
Nashauri wa muone mtumishi huyu namna gani kujinasua na laana hii ya wizara ya nishati na madini kwa kung'oa mabango ya Kakobe
 
Kuna watu hudhani mabadiliko huletwa na wanasiasa. Kila wanapoona wasio wanasiasa wanajitokeza ktk harakati huwavunja moyo kwa kuwapa "Mipasho". Muda umefika kila mmoja mwenye kupenda mabadiliko na kupigania haki aone anao wajibu wa kulitumia jukwaa alilonalo kuchochea mabadiliko. Asasi za kiraia, vyombo vya habari, vyama vya wafanyakazi, vyama vya kitaaluma, taasisi za elimu, na wengine wote kwa ujumla wetu tutambue na tusubutu kutimiza wajibu wetu.
 
Kudos Kakobe. Sikubaliani na misingi yake ya kidini/kiimani ila Kwa hili namuunga mkono.
 
Hoja nzuri sana, kwa nini uchaguzi usiwe ni siku ya kitaifa?

Tena iwe ni Alhamis ili ijumaa, jmosi hafi jpili tufatilie matokeo.
 
Maaskofu wote wangesema ukweli km kakobe hii nchi tungeshaikomboa kwenye makucha ya wakoloni weusi siku nyng!!Naona jana maaskofu wanajua tatizo lilipo ila wamebaki wanatupa mawe kichakani ilihali wanamfahamu nani anawalinda wezi!!
 
Jana katika ibada ya Christmas askofu Kakobe alieleza jinsi uchaguzi wa serikali za mitaa ulivyotawaliwa na vurugu na kusababisha watu kupoteza maisha. Alisema ni ishara mbaya sana chaguzi kama hizi zilikuwa zinafanyika kimya kimya hata watu wengine wanakuja kujua umeshaisha, hii ni dalili mbaya kwa uchaguzi mkuu.

Aliataja mambo matatu yanayosababisha na yakifanyiwa kazi uchaguzi utafanyika kwa amani bila vurugu.

1. UCHAGUZI KUTOFANYIKA SIKU ZA IBADA

Alisema chaguzi zinapofanyika siku ya ibada inawafanya watu wengi wasipige kura kwasababu watu lazima watakwenda kwenye ibada kwanza, alisema watawala kwa hofu ya kutoka madarakani wanatumia mbinu nyingi mojawapo ni kuona wanapiga kura watu wachache ili waweze kuiba kura.

Ametolea mfano uchaguzi uliopita amepata taarifa kwa washirika wake walipotoka ibada waliwahi kwenda kupiga kura wakakuta majina yao yametikiwa, kuuliza wakambiwa wameshapiga kura. Alisema uchaguzi ni jambo muhimu sana na ni haki kikatiba.

Siku ya uchaguzi iwe ni sikukuu ya kitaifa maana ziko sikukuu za kitaifa zisizo na umuhimu kama saba saba ambayo ingekuwa sikukuu ya chama baada ya mageuzi ikabadilishwa.

Alisema isipagwe Ijumaa kwa sababu ni ndugu zetu Waislam, Jumamosi ni ya Wasabato na Wakristu kama yeye akitolea mfano nchi zilizo tuzunguka Kenya, Uganda, Malawi na Zambia ufanya Jumatatu au Jumanne, A/ Kusini Jumatano.

2. Dafutari la wapiga kura

Serikali walitakiwa watoe elimu ya uraia wananchi wajue umuhumu wa kupiga kura na ni haki yao kikatiba na uandikishaji usiwe na mizengwe.

3. TUME HURU YA UCHAGUZI


Alisema tume tuliyonayo imeteuliwa na rais ambaye in mwenyekiti wa CCM, akasema anawashangaa wapinzani wanaingia kwenye uchaguzi na tume hii na wanatarajia washinde kwa tume ya CCM.

Alitolea mfano Simba na Yanga washindania mtani jembe wanaenda kucheza refa washika vibendera ni wa Yanga, Simba hata kama wamekwenda mazoezi ulaya hawawezi kushinda.

Alisema mambo haya watawala wana hofu ya kutoka madarakani haya hawawezi kuyafanya kwa kuwaomba hawawezi lazima tupige kelele tuwalazimishe wafanye.

Alisema watawala wamekuwa wanawambia viongozi wa dini waombe amani ni ujinga kuombea amani wanaosema tuombee amani ndiyo wanaondoa amani. Alisema amani na haki ni marafiki wakubwa wamebusiana watawala watende haki amani utaiona.

Alisema haoni sababu chama tawala kuangaika kutafuta mchawi aliyewafanya wachukiwe na wananchi wao ndiyo wenye serikali waondoe kero za wananchi uone kama kuna watakaoshabikia wapinzani, lakini hawana macho ya kuona wananchi wanahitaji nini!!

Aliwaonya kwamba CCM wasiobadilika hakuna kitachowazui kuondoka madarakani, akasema wako watawala walikuwa wanaitwa maprofesa wa siasa kama Moi lakini leo wako wapi!! wanaweza kuua na kung'oa watu kucha kwa hofu ya kutoka madarakani.

Wataondoka madarakani kama Herodi aliyeagiza wauawe watoto wadogo ili kumua Yesu, aliambiwa ni mfalme akafa yeye ndani ya mwaka wakati alikuwa ametawala miaka zaidi ya 30.


Alisema barua aliomwandikia rais ambayo Mungu aliowaonya wasipotubu lazima CCM itabomoka alisisitiza lazima yale yatimie akasema aliwambia hivyo hivyo Lukuvi na Ngeleja kwenye vikao vya swala la umeme pale kanisani kwake, aliwambia umeme hautapita wakacheka lakini leo miaka mitano umeme haujapita mpaka leo.

Na wakati ule aliwaambia TANESCO wamuogope Mungu alisema
TANESCO na wizara ya nishati na madini haitatulia hata akitoka Muhongo bado atakayekuja ni tatizo.

Suala la kubadilisha uongozi siyo kweli tukiweka kiongozi mpya hawezi kuleta badiliko alisema marais waliotangulia hakuna anayefanana na mwezake wote kiutendaji ni tofauti na uchaguzi uko jirani sana huu ni wa muhimu sana.

Alisema tuwe makini kwenye kuchagua sifa ya mtu tusipime kwa mambo binafsi au wa dini gani atuchagui kiongozi wa kutujengea makanisa au Miskito wala siyo wakutuongoza kwenda mbinguni bali wa kututoa kwenye umasikini tulionao.

Na maswali ya kuwauliza wagombea ni 2,

Kwanza, kwanini Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali zote tulizo nazo?

Pili, tukimpa atafanyaje kututoa hapa akieleza kinaga ubaga tumpe kama ameshawahi kuwa kwenye uongozi ngazi za juu.

Tatu, alipokuweopo alifanya jitihada gani kufanya hayo?

Mtu asilete porojo kwamba tumchague huyu ni chaguo Mungu,Mungu hatuchangulii viongozi hata mke sembuse kiongozi!!

Hiki alichokieleza Askofu Kakobe ni KWELI KWA ASILIMIA ZOTE! Ni mwenda wa zimu tu ndiye anayeweza asiuone ukweli huu!
 
Hivi kwa nini serikali hii hawajifunzi kutoka kwa wenzao kama nchi zinazo tuzunguka ambazo zinaheshimu na kutekeleza haki ya kuabudu kwa vitendo pamoja na haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Viongozi wetu wanakuwa kama wana ubia na ibilisi? Badilikeni
 
Kuna watu hudhani mabadiliko huletwa na wanasiasa. Kila wanapoona wasio wanasiasa wanajitokeza ktk harakati huwavunja moyo kwa kuwapa "Mipasho". Muda umefika kila mmoja mwenye kupenda mabadiliko na kupigania haki aone anao wajibu wa kulitumia jukwaa alilonalo kuchochea mabadiliko. Asasi za kiraia, vyombo vya habari, vyama vya wafanyakazi, vyama vya kitaaluma, taasisi za elimu, na wengine wote kwa ujumla wetu tutambue na tusubutu kutimiza wajibu wetu.

Mara nyingi sikiyo la kufa huwa halisii dawa hawa watawala kila alie jaribu kuwashauri ameonekana no adui namba moja na wanamshulikia kwelikweli madakitari walitoa ushauri mzuri waboreshewe masilai yao na nazingira masuri ya kazi na vitendea kazi bora wangefanya ingewapa kibali kwa wananchi kilichowatokea wote tunajua mifano ya washauri wazuri tunayo mingi wangemsikiliza waziri Mgimwa na mwanasheria was tanesco hawangepata asara hii kinyume chake waliwashuhulikia vilivyo hiyo ndiyo ccm inayo karibia kufa usifikiri itampenda mshauri yoyote atakuwa adui tu
 
Tume ya uchaguzi kumbe ni ya chama!!
Ni sawa na ugomvi wa mwenye nyumba na mpangaji hata ukimshinda atakutimua tu.
 
Back
Top Bottom