Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,861
- 1,302
Kuna taarifa kuwa bweni la wavulana wa kidato cha sita Kaisho sekondari iliyoko Karagwe limeunguzwa usiku wa kuamkia leo 8.2.2011 lakini hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa kwa kuwa wote walikuwa madarasani kwenye prep.
Fujo zilianza jumamosi baada ya mechi ya mpira wa miguu kati ya form six na form IV ambapo kidato cha nne walishinda. Tambo zilianzia hapo lakini zilififia.
Kwa kuwa kila jumamosi huwa ni siku ya vijana kuangalia TV, muda ulipofika wakamuomba second master awawashie TV waangalie, lakini yeye aliwambia kuwa kwa kuwa wanatarajia kupokea ugeni toka Karagwe sec kesho yake, muda huo wautumie kufanya maandalizi, Form IV hawakuridhika (wakipandishwa jazba na ushindi wa mpira) ndipo walizima umeme na kuwalazimisha form III, II na I kujiunga nao na kuanza vurugu.
Chumba cha computer na photocopy machines kilivunjwa na vyote kuharibiwa, ream za karatasi zkachanwachanwa; duka la shule lilivunjwa na walipokuta humo vinywaji wakalewa kabisa kisha wakavamia stoo ya vyakula na kuharibu maharage, sukari mchele nk kwa kuvitupa nje, magari mawili ya waalimu yalivunjwa vioo! nk.
Jana baada ya kikao,. kidato cha nne wakaamriwa kurudi makwao; lakini la ajabu ni usiku wa leo kutokea hayo ya kuchoma moto bweni.
Habari hizi nimezisikia toka Radio Fadeco ya Kayanga Karagwe.
Inasemekana malalamiko ya wanafunzi ni pamoja na kutaka mkuu wa shule aliyeacha kazi hivi karibuni arudishwe.