Kairuki aeleza changamoto ya vyeti feki ilivyomtesa

Kairuki aeleza changamoto ya vyeti feki ilivyomtesa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Dar es Salaam.
Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amesema uhakiki wa vyeti ni changamoto aliyokumbana nayo alipokuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Amesema hayo leo Jumatano alipokabidhi ofisi kwa Waziri mpya wa Utumishi, George Mkuchika. Amesema changamoto ya uhakiki wa vyeti hawezi kuisahau.

"Nchi kama vile Afrika Kusini, India na Pakistan walifanya jambo kama hili kwa awamu na bado hawajamaliza, lakini sisi tumelifanya kwa jumla, haikuwa kazi nyepesi," amesema.

Kairuki amesema mbali ya uhakiki, baadhi ya watendaji alioshirikiana nao hawakuwa waaminifu ambao walipenyeza watu wasiokuwa na sifa.

"Waliopenya katika hatua hii naamini Mkuchika atapambana nao ipasavyo," amesema Kairuki.

Amesema uhakiki ulichukua muda mrefu kiasi cha kuwakatisha tamaa watumishi wa umma.
Masilahi ya watumishi wa umma amesema lilikuwa changamoto nyingine kwa sababu Serikali inatamani kuyaboresha lakini fedha inayokusanywa haikidhi mahitaji.

Amewatoa shaka watumishi ambao hawajapandishwa madaraja akisema fedha kwa ajili watumishi zaidi ya 163,000 zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza hilo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi, waziri Mkuchika amesema mbali ya kuendeleza mazuri aliyoyaacha Kairuki, ikiwemo kudumisha nidhamu katika utumishi wa umma, atasisitiza elimu ya kupiga vita rushwa.

Mkuchika amesema atazungumza na Waziri wa Elimu ili elimu ya kupiga vita rushwa ianze kutolewa kuanzia shule ya msingi. Amesema nchi zilizofanikiwa kupiga vita rushwa ziliwekeza katika kutoa elimu juu ya madhara yake.

"Miaka ya nyuma ilikuwa hakuna mtu mwenye kuheshimika kama mtumishi wa umma. Wasomi wenye weledi na ujuzi walikuwa watumishi wa umma, hapa kati hali ikabadilika,” amesema.

Mkuchika amesema kazi iliyopo ni kuirudisha nidhamu hiyo na kuhakikisha watumishi wa umma wanakuwepo ofisini muda wote kutoa huduma kwa wananchi.



ITV
 
Mawaziri na Rais wao wote hawaeleweki
Raisi ana sema nchi ina hela
Waziri anasema pesa inayokusanywa haikidhi

TRA wanasema wamevuka lengo

Tunaomba albadir nyingine
Kuongea uongo consistently ni kazi sana, ndio maana muda mwingine wanatereza na kuongea ukweli
 
Mawaziri na Rais wao wote hawaeleweki
Raisi ana sema nchi ina hela
Waziri anasema pesa inayokusanywa haikidhi

TRA wanasema wamevuka lengo

Tunaomba albadir nyingine
tehe tehe tehe
eti tunaomba albadir nyingine
 
huyo mama nae embu apambane na hali yake kwanza
 
Mawaziri na Rais wao wote hawaeleweki
Raisi ana sema nchi ina hela
Waziri anasema pesa inayokusanywa haikidhi

TRA wanasema wamevuka lengo

Tunaomba albadir nyingine
Ulisha wahi wapi budget au pesa ya serikali ikatosha wewe,? Huku kwenyewe kwa trump na uchumi wake mkubwa bado kila siku wanalia pesa ya govt haitoshi na ndio hao wanatoa aids kwa third world countries. Pesa uwa haitoshi hata kama ww ni Dangote.
 
aisee mume anasema no salary hadi uzalishaji uongezeke, mke anasema haya duh
 
Waache waendelee na unafiki wao. Lakini hayo yoote yana mwisho
 
Kuongea uongo consistently ni kazi sana, ndio maana muda mwingine wanatereza na kuongea ukweli
Ni kweli kati ya mazoezi magumu kuyamudu duniani ni pamoja na kuongea uongo muda wote.
 
Kumbe awamu 5 simple kupata uongozi wwe kamata hata bangi cheo hicho mkuu wilaya.ngoja niende huku bush nikatafute wavuta bangi uenda nikapewa cheo na mkulu
 
Wanahabari wa nchi hii weupe kichwani na waoga,wanauliza mambo simpo yaliyo wazi. Unamuliza waziri mapambano ya vyeti halafu humuhoji kuhusu Bashite
 
Mawaziri na Rais wao wote hawaeleweki
Raisi ana sema nchi ina hela
Waziri anasema pesa inayokusanywa haikidhi

TRA wanasema wamevuka lengo

Tunaomba albadir nyingine
Mara ooh,tunahakik ivyeti, mara ooh, hata kama Bashite hajui kusoma hata A, mradi anakamata wauza madawa ni msomi.
 
Back
Top Bottom