Kaimu rpc awatimua waandishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaimu rpc awatimua waandishi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Oct 19, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  ......................................Kabla ya kuanza kuhojiwa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo mkoani Arusha, Akili Mpwapwa, aliwafukuza waandishi wa habari waliofika kufuatilia tukio hilo katika kituo cha Polisi.

  Mpwapwa alisema: “Tokeni hapa kwani mnafanya nini hapa Polisi, huu sio muda wenu huu. Nyie si mnakuja saa tano asubuhi na saa hizi ni saa nane mpo hapa. Ondokeni hapa sitaki kuwaona, tawanyikeni,” alisema huku akionyesha kukasirika.
  Kamanda Mpwapwa aliwaeleza waandishi hao kuwa kama wanataka habari za Millya waende kuzitafuta mitaani, kwani huko ndiko kwenye habari na siyo Polisi.
  Waandishi hao waliondoka kituoni na kwenda karibu kusubiri kuzungumza na Millya baada ya mahojiano hayo.
  Hali hiyo ilizua gunzo kwa wanahabari na kuanza kuhoji uhalali wa Polisi kuwafukuza wasiripoti tukio hilo, ambalo limeibua hisia kuwa ni la kisiasa ingawa linaonekana kuwa ni mpambano kati ya UVCCM na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha.
  Waandishi hao walihoji kwa nini na Polisi wanawatolea kauli za kashfa wanapofuatilia taarifa za Millya wakati wamekuwa wakiwaita mara kwa mara kuwapa taarifa za matukio mbalimbali.
  Hata hivyo wanahabari hao wamepitisha azimio la kuacha kwa muda kuandika habari za Polisi mkoani Arusha hadi hapo Akili Mpwapwa atakapowaomba radhi.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  :poa???????????????????????????????
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Za mauaji ya chadema mliitwa mkakimbia nusu mkatike miguu.
   
 4. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AAAAAAAA......... Kumbe ni afande UBWABWA Polisi kwishney.
   
 5. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Walichelewa kufika au?! Je millya anashikiliwa na polisi au?? Kwa tuhuma gani??
   
 6. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huyu kaimu RPC hafai hata kuwa koplo sugu kwa sababu ni mwoga!
   
Loading...