Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma anza na hii tume ya utumishi wa mahakama Tanzania

MP CHACHANDU

JF-Expert Member
Dec 4, 2016
875
616
Nichukue fursa hii kukupongeza kwa kuteuliwa na rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania kuchukua nafasi ya jaji mstaafu Othman chande hongera kwa hilo watanzania wengi tuna imani sana na utendaji kazi wako uliotukuka wa hali ya juu na weledi usiopingika matumaini yetu kuwa utaleta maendeleo chanya ndani ya mahakama zetu nchi.

Mhe kaimu jaji mkuu Tanzania prof Ibrahim Juma nikuombe uanze na uozo ambao upo kwenye hii tume ya utumishi wa mahakama Tanzania kwenye kitengo cha maafisa utumishi kumekuwepo na unyanyasaji mkubwa sana pamoja ukiukwaji wa sheria kwa waajiriwa wa mahakama kunyanyaswa na kunyimwa haki zao za msingi na maafisa utumishi mfano kuna posho ya lunch kwa watumishi wote wa mahakama nchini hizi pesa hupewa watumishi wa mahakama kwa kila wiki hizi pesa mara nyingi haziwafikii walengwa wake na kuishia kuliwa na maafisa utumishi wa mahakama hili ni tatizo kubwa sana tunaomba ulifanyie kazi.

Mhe, kaimu jaji prof. Ibrahim Juma, mnamo tarehe 01/06/2016 siku ya jumanne tume ya utumishi wa mahakama iliajiriwa vijana 348 nchi nzima baada ya hawa vijana kushinda usaili wao vijana hao waliajiriwa kwenye vitengo mbalimbali kwenye mahakama za mwanzo , wilaya, mikoani na rufaa mfano waliajiriwa kama mahakimu , walinzi, wasaidizi wa ofisi,madreva, nk walipewa mikataba wakasaini na walipewa barua za kupangiwa vituo vya kazi na walipewa fedha kujikimu kila mmoja alipewa kiasi cha laki sita na sehemu baada ya kuanza zoezi la uhakiki wa watumishi hewa hawa vijana walirudishwa nyumbani kwa mda ili kupisha uhakiki wa watumishi hewa toka mwezi wa sita mwaka Jana sasa wanakalibia kumaliza mwaka wapo nyumbani hakuna taarifa yeyote juu ya hatima yao majina yao haya hapa walipoitwa kazini.

a24fb5bb9daee614453370d957364543.jpg
0cf48da6e99c1adf00c005201a6d6a6c.jpg
18c1cbb9a53160ad7f445dcf46e9a3b3.jpg


Mhe kaimu jaji mkuu Tanzania wewe ni kiongozi shujaa mpigania wanyonge tunagemea sana busara zako juu ya vijana hawa watanzania walio na nia ya kuitumikia nchi yao isitoshe wametumia na fedha za serikali ambayo ni mabilioni ya fedha ambazo ni jasho na kodi za watanzania tunaomba kwa hekima zako shughulikia hili swala vijana hawa wajue hatima yao.

Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki mahakama ya Tanzania .

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma watanzania tuna imani na wewe sana.
 
Kweli mkuu jamaa namkubali san

Kukubalika na jamii ni lazima aoneshe kuwa mahakama atakayoingoza itapinga tyrannic rule na authoritarianism!! Samatta alipokuwa CJ aliweza kusimamia independence ya judiciary bila kuingiliwa na Executive arm!!!

Inaelekea kupewa hiyo nafasi kukaimu ni kutaka kumpima kama he will toe the line au atakuwa na msimamo independent; ili kama wataona ni mtu independent waweze kuweka boya lao litakalofuata amri za mtawala!!
 
Kukubalika na jamii ni lazima aoneshe kuwa mahakama atakayoingoza itapinga tyrannic rule na authoritarianism!! Samatta alipokuwa CJ aliweza kusimamia independence ya judiciary bila kuingiliwa na Executive arm!!!

Inaelekea kupewa hiyo nafasi kukaimu ni kutaka kumpima kama he will toe the line au atakuwa na msimamo independent; ili kama wataona ni mtu independent waweze kuweka boya lao litakalofuata amri za mtawala!!
Umeongea kweli mkuu
 
Back
Top Bottom