Kaimu DEO idara ya sekondari na mtaaluma wanachangia sana kuangusha kiwango cha elimu hapa wilayani na hasa hapa shuleni kwetu Ewong'on.
Sisi waalim wa Ewong'on sekondari tulipeleka malalamiko yetu kwa DEO na Mtaaluma kuhusu uendeshaji mbovu wa shule yetu lakini hakuna hatua thabiti zilizochukuliwa kuhakikisha mambo yanarekebishika.
Tuliandika barua yetu iliyobeba malalamiko yetu kuhusu uongozi mbovu, ukosefu wa idara muhimu ktk uendeshaji shule, shule kutokuwa na makamu mkuu wa shule kwa mwaka mzima, kutokuwepo kwa bodi ya shule na mambo mengine ambayo yanachangia kupungua kwa morali ya waalimu na wanafunzi ktk kufundisha na kujifunza hvyo kusababisha taaluma kushuka hapa shuleni.
Tulijua kaimu DEO Mr.Kimweri ni mtu muungwana ambae anaijua background ya headmaster wetu vizuri hivyo angeweza kulitatua tatizo letu ila cha ajabu alikuja akajifungia ofisini na mtuhumiwa ambae ni mkuu wa shule wakaongea yao na waalim hawakuitwa wala kuhojiwa lolote zaidi ya wao kuondoka na mambo yanaendelea kuwa mabovu.
Hatujui tumlalamikie nani maana Mkurugenzi wa wilaya nae anajua jambo hili ila amenyamaza. Hivyo kupitia hapa JF tunajua ujumbe unaweza kuwafikia wahusika wa ngazi za juu zaidi ambao watatusaidia kutatua au kutuondolea uongozi huu mzigo.
Tunaamini pia wachangiaji wa hapa mtatoa mawazo yatakayotuwezesha kupata ufumbuzi ili tufikie lengo la kuiinua taaluma ya shule yetu , wilaya na Taifa kwa ujumla.