GE2025 Kailima Ramadhani: Acheni upotoshaji, idadi ya wapiga kura iko sahihi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwizukulu wa Buganda

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2024
Posts
638
Reaction score
1,771
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imesema kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 16 (5) sheria ya Uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani Na.1 ya mwaka 2024, Tume imekamilisha uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa awamu zote mbili.

Akizungumza na kwenye Mkutano wa Kitaifa kati ya Tume na Wazalishaji Maudhui Mtandaoni, leo Agosti 3, 2025 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi Bwa. Kailima Ramadhani amesema, awamu ya kwanza ilianza tarehe 20 Julai 2024 na kukamilika 25 Machi 2025, ambapo awamu ya pili ilianza Mei 4, 2025 na ilikamilika Julai 4, 2025.

Akitolea ufafanuzi wa taarifa zilizotolewa hivi karibuni na baadhi ya Wanasiasa, kwamba takwimu ya idadi ya wapiga kura inatofautiana na ile ya Sensa ya watu na makazi, Kailima alisema si kweli na kuwataka wanaotoa taarifa hizo waache upotoshaji.

"Niombe wale wote wanaotaka kupata taarifa za Tume waje kwetu kupata taarifa milango iko wazi, wasikae huko pembeni wakaanza kutoa taarifa zao ambazo haziko sahihi, kufanya hivyo ni kuleta taharuki na kunaweza kuharibu mchakato mzima wa uchaguzi jambo ambalo halina manufaa kwa amani na usalama wa Nchi yetu"

Akizungumzia uboreshaji huo, Kailima amesema, jumla ya vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura ni 40,170 idadi iliyojumuisha vituo 130 vya Magereza ya Tanzania Bara na vituo 10 vya vyuo vya mafunzo kwa Zanzibar.

"Kama ambavyo Mwenyekiti wa Tume Jaji Mwambegele alieleza, kwa sasa wapo wapiga kura 37,655,559 ambapo idadi hii ni ongezeko la asilimia 26.55 ya wapiga kura 29,754,669 waliokuwepo kwenye Daftari la mwaka 2020" alisema Bwa. Kailima.

Akiendelea kutoa ufafanuzi wake Mkurugenzi huyo wa Tume alisema kati ya wapiga kura walioandikishwa 36,650,932 wapo Tanzania Bara na wapiga kura 1,004,627 wapo Tanzania Zanzibar ambapo wanawake ni 18,943,455 sawa na asilimia 50.31 na wanaume ni 18,712,104 sawa na asilimia 49.69 ya wapiga kura wote.

Aidha Kailima alisema kwa mujibu wa kanuni tarehe 27 julai, 2025 Tume ilivapatia vyama vya siasa nakala tepe (soft copy) ya daftari la kudumu la wapiga kura

Akizungumzia zoezi la upigaji kura Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima Ramadhani alisema, jumla ya vituo vya kupigia kura 99,911 vitatumika katika zoezi hilo ambapo vituo 99,349 ni upande wa Bara na vituo 2,562 upande wa Zanzibar, likiwa ni ongezeko la vituo 18,344 kutoka vituo 81,567 vilivyotumika wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Chanzo: Jambo TV
 
Message sent and delivered! Tunashukuru amepata ujumbe kuwa wanapika kura feki!
Screenshot_20250703-140259~2.png
 
Wanaowasaidia kuiba kura wamekiri, sasa anatoa wapi credibility ya kusema ukweli
 
Kwa

Hiyo no reforms no election imefeli
 
Awadanganye wajinga wenzake. Ila ukweli utabakia palepale! Hakuna wapiga kura milioni 37 kasoro wa kukubali kushiriki kwenye maigizo ya Bongo muvi.
 
Ulitegemea mwizi atoke hadharani na kujitangaza kuwa yeye ni mwizi?

Huyo ni agent wa uovu ulioandaliwa. Alaaniwe yeye na waovu wenzake wote.
 
Back
Top Bottom