Kahama wamtaka Zitto; Mbunge wao Lembeli yuko kwenye malumbano ya kisiasa na chama chake

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
BAADHI ya wananchi wa Jimbo la Kahama wamemuangukia Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kufika jimboni kwao ili ajionee kero na changamoto za kimaisha zinazowakabili.

Wananchi hao wamedai kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kubaini mbunge waliomchagua ameendekeza malumbano ya kisiasa yasiyo na tija kwa maendeleo ya wilaya yao.

Wakieleza sababu za kumhitaji Zitto wananchi hao wakiongozwa na wazee kwa nyakati tofauti walisema wanatambua uchapakazi wa mbunge huyo unaolenga maslahi ya taifa, tofauti na Mbunge wa Jimbo lao James Lembeli, waliodai kuwa ameishajipambanua kuwa hana muda wa kushughulikia matatizo yao zaidi ya kujiingiza katika malumbano ya kisiasa na viongozi wake wa Chama Cha Mapinduzi.

Walisema kuwa wanasikitishwa na Mbunge wao Lembeli ambaye anatambua fika kuwa msimu huu wa kilimo kuna hatari ya wapiga kura wake kukabiliwa na janga la njaa kutokana na baadhi ya maeneo mbalimbali katika jimbo lake kukabiliwa na upungufu mkubwa wa mvua ilihali mbunge wao akishindwa kuchukua hatua stahiki.

" Tunashangaa toka miaka mitano iliyopita kwa mbunge wetu kukalia mambo haya haya haya ya marumbano huku wananchi wa jimbo lake tukikabiliwa na changamoto nyingi za maendeleo zikiwemo barabara mbovu, huduma za msingi za kijamii haziridhishi katika maeneo mbalimbali ya jimbo hili; sasa sijui tukimbilie kwa nani? Labda kwa Zitto Kabwe aliyeonyesha uzalendo kwa kujali maslahi ya Buzwagi," alisema.

Walizitaja changamoto nyingine zinazowakabili ikiwamo wakulima kupatiwa pembejeo za ruzuku zisizo na ubora ambazo pia haziwafikii kwa wakati.

Hali kadhalika mzozo wa bei ya tumbaku ambayo licha ya uzalishaji kuwa mkubwa lakini makampuni yamegoma kununua zao hilo kwa bei ya msimu uliopita tena yakisisitiza kutonunua kiwango cha uzalishaji uliofikiwa msimu huu.

Pia wananchi hao wamelalamikia tatizo la ajira katika mgodi wa Buzwagi. Kwa upande wa elimu, wamelalamika baaadhi ya walimu wa sekondari za kata katika jimbo hilo ambao waliajiriwa Januari 31 mwaka huu kutolipwa posho za kujikimu pamoja na nauli zao huku wakicheleweshewa mishahara yao, hali ambayo inawafanya maisha yao katika shule wanazofundisha vijijini kuwa magumu.

Walisema badala ya mbunge huyo kushughulikia kero hizo amekalia malumbano ambayo hayasaidii kuleta maendeleo katika Jimbo la Kahama na ustawi wa taifa zima.
 
Aendelee kuufuata ushauri wa Sitta wakati ule aliyemwambia aendelee hukohuko Kigoma na aachane na mambo ya kahama hata kama anaasili ya huko.... na hii ni kwa usalama wake kisiasa
 
Prove me wrong... dont just say, be realistic...

huoni namna hoja inavyoelea hewani? hao wazee ni kina nani,labda hata jina moja litatosha.wameenda kumuona lini na wapi na majibu yake yalikuwa ni nini.
 
isije kuwa story ya kupika maana humu kwa tetesi napakubali

Imetokea mtaa gani na lini? Majengo, Mhongolo, Nyasubi, Nyakato, Nyahanga? Usituletee habari za mti wa siasa nje ya ofisi za ccm! Hii habari si kweli.
 
Huku kwetu tofauti sana na sehemu nyingine,mtu anaweza toka kokote kule na kutawala wenyeji ijapo wanasema Tanzania hakuna ukabila wala ukanda lakini kwetu ndivyo ilivyo.

Maeneo ya Wanyamwezi na Wakamba wa Kahama anakotokea Maige na Lembeli,ni moja ya sehemu ambazo zinaegemea upande wa koo na kabila.

Ukitangaza nia Kahama lazima wakuulize unatoka ukoo wa nani?wewe ni nani?kama hawakujui sahau kuwa mbunge.

Sijui kwenu kama wageni wanatawala nashangaa kusikia Zitto anataka kuja kugombea Kahama kwenye Uchifu wa Kitemi.

Hapo asahau huku siyo Kigoma.
 
ZZK hata akiwa Raisi kwa jinsi anavyofanya kazi akimaliza miaka mitano anaweza akaenda kugombea Uraisi Mali,wenzako wameshamuomba hivyo
 
Ataenda Kahama, atapewa uchifu then atagombea ubunge na kushinda, simply like that!
 
Huku kwetu tofauti sana na sehemu nyingine,mtu anaweza toka kokote kule na kutawala wenyeji ijapo wanasema tanzania hakuna ukabila wala ukanda lakini kwetu ndivyo ilivyo.maeneo ya wanyamwezi na wakamba wa kahama anakotokea maige na lembeli,ni moja ya sehemu ambazo zinaegemea upande wa koo na kabila.ukitangaza nia kahama lazima wakuulize unatoka ukoo wa nani?wewe ni nani?kama hawakujui sahau kuwa mbunge...sijui kwenu kama wageni wanatawala.nashangaa kusikia zitto anataka kuja kugombea kahama kwenye uchifu wa kitemi......hapo asahau huku siyo kigoma.

Nikupe kwanza pole kwa yale yote yaliyotokea hapo nyuma. Kahama ya sasa siyo ile ya zamani. Kwa sasa Kahama ina mchanganyiko wa watu, hivyo atakaye gombea hapo hategemei kura za upande mmoja tu.
 
Huyu anatafuta kick tu, mwaka 2010 alikua anaongea ngonjera hizo hizo,:matokeo yako alirudi Kg Kaskz, usishangae pamoja na kusema ameshaaga jimboni akatengeneza drama nyingine na kurudi kugombea jimbo hilohilo!
 
Huyu anatafuta kick tu, mwaka 2010 alikua anaongea ngonjera hizo hizo,:matokeo yako alirudi Kg Kaskz, usishangae pamoja na kusema ameshaaga jimboni akatengeneza drama nyingine na kurudi kugombea jimbo hilohilo!
Zitto ni master of deception
 
Last edited by a moderator:
Nashangaa sana naposikia kwamba zitto anakubalika kahama,hivi kahama ipi?au siku hizi kigoma kuna kahama?au kahama ya buzwagi aliyohongwa na maccm afu akakaa kimya?nani anajua kilichoondelea baada ya kuibuka hoja ya buzwagi chini ya zuberi zitto kabwe?anasena aliwatetea watu wa kahama kuhusu mgodi wao,je alipotetea nini kilichoendelea buzwagi tofauti na yeye kunafaika na mgodi huo?zitto kwanini unapenda kuibua hoja afu mwishoni unakula kona?kahama ukija usizani tutakupokea kama kipindi kile ulipokuwa mpambanaji.zitto ulikuwa paka mtiifu kwa mwenye nyumba ila sasa ni paka poli(kimburu)umekimbia ndani na kwenda polini na kazi yako sasa ni kula vifaranga...na mbwa haitwi jina ukubwani...akiitwa haitiki.
 
Kama wewe ndiyo msemaji wa watu wa Kahama basi Kahama kuna tatizo la uelewa.
 
ZZK Kumbuka KAHAMA si KIGOMA jaribu uone mwenyewe yatakayokupata hutasahau maana una chapa na NEMBO ya USALITI usoni kwako.
 
Back
Top Bottom