KAHAMA: TFDA yateketeza zaidi ya tani 4 ya bidhaa zisizofaa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Mamlaka ya chakula na dawa TFDA kanda ya ziwa imefanya msako mkali katika maduka ya dawa, maduka ya vipodozi na maduka ya vyakula katika maeneo tofauti wilayani Kahama na kukamata shehena ya bidhaa mbalimbali ambazo hazifai kutumika kwa matumizi ya binadamu.

Ktika msako huo TFDA imekamata na kuteketeza zaidi ya tani 4 za bidhaa zisizofaa.

Akizungumzia sakata hilo mkaguzi wa dawa kutoka mamlaka ya chakula na dawa kanda ya ziwa, Bw.Andrew Mwabuki amewatahadharisha wafanyabiashara wa dawa wilayani Kahama kuzingatia vigezo na masharti ya biashara hiyo, huku akizitaja takwimu za bidhaa ambazo zimekamatwa na kuteketezwa.

Makaya William Msonda, akizungumza kwa niaba ya mkaguzi mkuu wa mamlaka ya chakula na dawa ofisi ya kanda ya ziwa amesema ili bidahaa kutoka nje ziruhusiwe kuingia nchini, ni lazima vigezo vilivyowekwa kitaifa na kimataifa vizingatiwe, huku mfamasia mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bw. John Mfutakamba akitanabaisha bayana baadhi ya sababu zinazosababiusha kuwepo kwa bidhaa bandia na vyakula visivyofaa.
 
Back
Top Bottom