Kagera Sekretariati ya mkoa rais kawaasa mfanye kazi kwa bidii kwelikweli

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
17,034
7,590
Juzi tu akiwa hapo mkoani aliwapa changamoto za kimaendeleo. Sasa nyinyi kama wasomi, wataalamu na wazoefu ni tayari kazi imeshawekwa mezani na ni wajibu wenu kutekeleza. Kwa kifupi, raisi aliwamegea kidogo mtimize yafuatayo;

1. Kushughurikia na kusimamia kilimo cha kisasa kwa njia za umwagiliaji katika mkoa.

2. Kuhakikisha bei za mazao zinaboreka kwa kufuta lundo la kodi za kinyonyaji

3. Kuanzisha viwanda vinavyotokana na mazao ya kilimo, uvuvi, mifugo na madini ya bati katika mkoa.

4. Kutengeneza miundombinu ya kuondoa umaskini ( barabara, maji, masoko n.k ) na kuchochea maendeleo

Kwa ujumla wake, haya maagizo mmeagizwa nyinyi na mmepewa assignment kwamba siku akirudi akute mambo yanaenda tayari. Sasa kosa mtakalolifanya ni pale mkapofikiria hasi kwasababu tu hilo jimbo liko chini ya upinzani, lakini mkasahau kwamba huyu raisi haeleweki na hana uvumilivu katika maamuzi. Mkikaa mkafikiri hivyo basi mjue mtakuwa mnajichongea wenyewe, yeye haoni tabu kukutumbua pale akiri yake itakapomtuma na hutamweleza bla bla. Rais haeleweki iwe mchana ama usiku, kiangazi ama kwenye masika, jamaa hasomeki kabisa.

Ninawashauri mtimize wajibu wenu kwa kufanya kazi kweli kweli. Naamini hata nyinyi mnaona anakopita na kuwasifia baadhi ya maeneo kwa wale wanaofanya vizuri, msidhani haoni nani anafanya kazi na nani anazuga. Na nawahakikishieni, mkikaa tu mkalegea mkafikiri mnamkomoa Lwakatare basi mkae mkijiandaa kutumbuliwa, huyu ni rais wa sifa na anafanya maamuzi akiwa site tu. Pale pale anaamua na anafanya kweli. Atakutumbua na utatumbulika kwa aibu kweli kweli.

Yangu ndo hayo kwenu, nawatakieni mapinduzi mema.
 
Mmeona sahivi kila mkoa viongozi wanashindana dhidi ya majirani zao mikoa mingine, wakuu wa idara na mikoa wanashindana kwa kuongeza ubunifu katika kazi zao wakati nyinyi mnazidi kuuchapa. Kitakachowasaidia mbele za bosi wenu ni kimoja tu, kumsoma na kuzisoma vyema arama za nyakati
 
Back
Top Bottom