Kagera: Rais, serikali haitajenga nyumba za waathirika wa tetemeko. Azuia msaada wa chakula Missenyi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Rais Magufuli leo amefanya ziara Wilayani Missenyi ili kujionea athari za tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa wa Kagera.

Rais akiongea kwa ujasiri amesema kuwa hili tetemeko limeipiga serikali pia hivyo wananchi waliodanganywa kuwa serikali itawajengea nyumba mwananchi mmoja mmoja kwa walioathirika na kupelekea kubomoa nyumba zao zilizokuwa zimeathirika kidogo basi MWAFA ( Mmekufa).

Pia Rais amesema hatapeleka msaada wa chakula katika wilaya ya Missenyi na kuwataka wananchi kutumia mvua iliyoanza kunyesha kulima mazao ya chakula.

Pia amemtaka mkuu wa wilaya kama ameshindwa kusimamia suala la njaa amwambie Rais kuwa ameshindwa kuongoza wilaya hiyo ili hatua zichukuliwe.

 
Nani alimwambia Watanzania wanataka Serikali iwajengee wahanga nyumba zao zilizoharibika!?

Watanzania tunataka bilioni 16 zilizochangwa na Watanzania na nchi marafiki ziende kwa wahanga badala ya kuzikwapua. Muwape pesa zao haraka sana bila kukosa.
 
Tuna kazi nyingi za kufanya kwa hiyo hatuna muda wa kukaa tunaombea majitu hapa!
 
Back
Top Bottom