pantheraleo
JF-Expert Member
- Jan 5, 2013
- 692
- 887
Ngara. Mahakama ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera imewahukumu raia wanne wa Rwanda kwenda gerezani miaka 20 kila mmoja, baada ya kukutwa na hatia ya makosa manne waliyotenda kwa kuingia nchini mwaka 2016 kinyume cha sheria.
Mwendesha mashtaka wa polisi wilayani hapa, Respicius John mbele ya hakimu Andrew Kabuka aliwataja raia hao kuwa ni Yauza Faustine (68) mkazi wa Nyarutete, Akizamunga Augustine (52), Kasasila Twagilaelo (37) na Ndikubihimana Oscar (22) wote kutoka maeneo mbalimbali ya Rwanda.
Alidai kuwa walikamatwa katika hifadhi ya wanyamapori ya Burigi baada ya kuingia bila kibali cha mkurugenzi wa wanyamapori.
Kosa la pili ni kuingia nchini bila kibali huku kosa la tatu ni kukutwa na nyara za Serikali ambazo ni nyama za wanyama mbalimbali zenye thamani ya Dola 540,000 za Marekani (Sh988.8 milioni).
Alisema kuwa washtakiwa walikutwa na vifaa vya kuwindia wanyama ambavyo ni nyaya, mapanga, kamba za aina mbalimbali, pinde na mishale lakini pia walijihusisha na uharibifu wa mazingira.
Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani Agosti 29, 2016 kwa mara ya kwanza na kufunguliwa kesi namba 03/2016 ya kuhujumu uchumi. Hata hivyo, walikana mashtaka hayo.
Akisoma hukumu hiyo, hakimu Kabuka alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka mahakama imejiridhisha pasi na shaka kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo.
Hakimu Kabuka alisema washtakiwa wote wametiwa hatiani kwa makosa manne hivyo watakwenda jela miaka 20 kila mmoja na kulipa faini ya Sh3 milioni kila mmoja.
Hata hivyo, washtakiwa walishindwa kulipa faini na kupelekwa gerezani kuanza kutumikia adhabu ya kifungo.
Chanzo: Mwananchi
Sent Using Yono Vibe