Kagera: Mchungaji aishi kinyumba na wake wa waumini kwa madai ya kushukiwa na Roho mtakatifu

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya KARAGWE Mkoani KAGERA imelazimika kuhamia kwa muda katika kanisa la kipentekoste la HURUMA KATIKA KRISTO kufuatia kuwepo madai ya mchungaji wa kanisa hilo kuishi kinyumba na wake za waumini wake kwa kile anachodai kushukiwa na Roho Mtakatifu.

Mchungaji ambaye pia ni mmiliki wa kanisa hilo JAPHES JOSEPHAT anadaiwa pia kukatisha masomo baadhi ya wanafunzi katika kijiji cha NYAKINTUNTU ambao wamejiunga na kanisa lake.



9b0e490e5bfb97c5bc1b004c1a72301d.jpg
 
ad45a4ceb6b2e55cb0254eb1c8bee07e.jpg
5bda8a308136f024d045ef1e3faabbb4.jpg
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera imelazimika kuhamia kwa muda katika kanisa la kipentekoste la Huruma Katika Kristo kufuatia kuwepo madai ya mchungaji wa Kanisa hilo kuishi kinyumba na wake za waumini wake kwa kile anachodai kushukiwa na Roho Matakatifu

Mchungaji ambaye pia ni mmiliki wa Kanisa hilo Japhes Josephat anadaiwa pia kukatisha masomo baadhi ya wanafunzi katika Kijiji cha Nyakintuntu ambao wamejiunga na kanisa hilo.

Chanzo: TBC habari
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya KARAGWE Mkoani KAGERA imelazimika kuhamia kwa muda katika kanisa la kipentekoste la HURUMA KATIKA KRISTO kufuatia kuwepo madai ya mchungaji wa kanisa hilo kuishi kinyumba na wake za waumini wake kwa kile anachodai kushukiwa na Roho Mtakatifu.

Mchungaji ambaye pia ni mmiliki wa kanisa hilo JAPHES JOSEPHAT anadaiwa pia kukatisha masomo baadhi ya wanafunzi katika kijiji cha NYAKINTUNTU ambao wamejiunga na kanisa lake.
9b0e490e5bfb97c5bc1b004c1a72301d.jpg

87c5af7b0c2847845253d7507e930674.jpg
Hawa wachungaji wa siku hizi,nikiwaona,huwa nahisi nimekutana na majambazi ya kiroho,wanawake ndio wahanga sana was haya majitu,kule Mkoani Songwe,inapofika wakati wa mavuno,mikutano kibao ya injiri vijijini,wenyeji wakaniambia hao wanakuja kipindi hicho kwa ajiri ya kujipatia kipato,baada ya mavuno hawaonekani tens mpaka msimu ujao,
 
Aiseeeh, ama kweli ulimwengu hadaa!

Yeye huyo , ameona aweke kabisa kambi na pampunchi za waumini wake, na kujipigia apendavyo!

Hakika, Mungu ana kazi ngumu sana nyakati hizi kuliko wakati anaumba huu ulimwengu na vilivyomo!!
 
Kuna habari nimeiona TBC
Mchungaji akamatwa kwa kutembea au kuoa mke wa MTU.Sasa kilicho nishangaza Mkuu wa wilaya ameingia kanisani na kupewa mic na kuanza kusema makosa ya Mchungaji mbele ya waumini wake.

Mimi napenda kumwambia asifikirie kuwa ana mamlaka kila sehemu Kanisani na msikitini ni mahali penye utaratibu wake kama Mchungaji amevunja sheria ni vema angemtafuta na kwenda kumuoji lakini sio kwenda kanisani kwake na kuanza kusema matatizo ya Mchungaji ni tabia mbaya sana.

Nawasilisha
 
Nimeisikia hii habari tbc kuwa kuna baba mmoja aitwaye apollo ndiye aliyepeleka malalamiko kwa DC kuwa mchungaji amemuweka kinyumba mkwewe (mke wa mwanaye) na kwamba mume wa huyo mwanamke ameridhia jambo hilo kwa misingi hiyo hiyo ya "roho mtaka tifu"

My take: viwanda vya risasi havimudu kuzalisha risasi za kutosha kuua wajinga wote duniani.

Ila namshukuru DC amekamata mchungaji, mume na mke wote tia ndani ma kuna uwezekano wakafunguliwa kesi ya ugoni maana kuna ndoa halali kwenye hiyo equation.
 
Back
Top Bottom