Kagame: Tanzania kufanya biashara na Rwanda inatupa amani

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
kagame.jpg

RAIS wa Serikali ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame amesema nchi yake inapata amani kuona kuwa Tanzania iko tayari kufanya nao biashara.

Hayo yamesemwa leo, wakati Rais Kagame alipokuwa akifungua maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwl. Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

“Inatupa amani kuona Tanzania iko tayari kufanya biashara na Rwanda, naahidi kuwa tutaendelea kujifunza zaidi na kufanya biashara zaidi” amesema Rais Kagame.

Soma zaidi hapa => Kagame: Tanzania kufanya biashara na Rwanda inatupa amani | Fikra Pevu
 
Nimemsikia Leo nilikuwa pale sabasaba, sikuwahi kupata kumsikia huyu jamaa akiongea, Leo nimebahatika na kumuona.......ukiachilia mbali uzuri wa speech yake ila pia na umakini wa kila neno analotamka kwangu Mimi nakubali Rwanda wana kiongozi.
 
Inaonekana anawajal wananch wake sana na wamepata unafuu wa maisha mpaka kubadilisha katiba aendelee kuongoza
Magu anataka kumwiga nafkir
 
Nimemsikia Leo nilikuwa pale sabasaba, sikuwahi kupata kumsikia huyu jamaa akiongea, Leo nimebahatika na kumuona.......ukiachilia mbali uzuri wa speech yake ila pia na umakini wa kila neno analotamka kwangu Mimi nakubali Rwanda wana kiongozi.
I was lucky to hold a talk with him in Kigali. Ukiachana na mapungufu yake tunayoyaona jamaa kwa kweli ana nia Njema na nchi yake. Ni mtu aliejipanga kuipeleka nchi yake kwenye maziwa na asali, bahati mbaya hajamuandaa Joshua wa kuendeleza atakapoishia
 
Ngoja tusubiri kubadili katiba yetu baba nanii aendelee kuongoza, maana mwalimu wake kishabadili mbona
 
I was lucky to hold a talk with him in Kigali. Ukiachana na mapungufu yake tunayoyaona jamaa kwa kweli ana nia Njema na nchi yake. Ni mtu aliejipanga kuipeleka nchi yake kwenye maziwa na asali, bahati mbaya hajamuandaa Joshua wa kuendeleza atakapoishia
Nikiwa na wenzangu tuliruhusiwa kufanya mazungumzo mafupi nae Kigali- Village urugwiro ni mtu makini mwenye nia njema na nchi yake. Alitueleza hatua walizochukua kudhibiti rushwa na jinsi walivyowashughulikia wala rushwa. Anazungumza pole pole na yuko makini katika kile anachoongea.
 
think quickly,speak slowly..ndo wanavofundishwa majasusi,usishangae
 
Back
Top Bottom