babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 16,311
- 20,895
Ndugu wana Jamii,
Baada ya kusoma kuhusu kukamatwa kwa huyu Mmarekani, Mr. Peter Erlinder, nchini Rwanda nimesoma kuhusu hili sakata na nimejiuliza mambo mengi sana. Kati ya hayo ni kuhusu uhalali wa Laywers/ wanasheria kusimamia kitu "wasichokikubali" kwa ajili ya kupata pesa na pili ni double standard katika mataifa ambapo mataifa madogo hayana haki ya kuhoji mataifa makubwa wala watu wake.
Kwanza, huyu Erlinder ni Mmarekani ambayo inakubali kuwa genocide imefanyika nchini Rwanda. Je anapingana na serikali yake inayokubali hilo? Je kama amekuwa akiwatetea watuhumiwa walioko ICTR kwa kukana kutokea kwa genocide wakati mahakama yenyewe ndiyo jukumu lake, ni kutaka apate pesa au ni kwa kuwa anaamini kuwa hakuna genocide? Au kutetea "haki" for the sake of it? Hapa nina wasiwasi kwani ilinakiliwa na media y US kuwa Erlinder aliomba aachiliwe ili akosoe aliyo yasema kukana genocide!
Pili, sijawahi kusikia Mmarekani yeyote akipinga Jewish Holocaust na pia hawatangazi kuichukulia sheria Israel ambayo inawanyanyasa wa Palestina. Na kama atakuwepo sijui ataadhibiwa kiasi gani
Kuhusu uamuzi wa Rwanda, Marekani imekuwa na kigugumizi kwani walisema aachiwe kwa kuwa hana afya nzuri ikiwa ni pamoja na kuwa ana tatizo la kiakili (kichaa). Hili nimeliona kama tatizo la kutotaka kukanusha genocide kwani Rais Bill Clinton alikiri alipokuwa Rwanda mwaka 2000 (kama sikosei)
Mwisho, nikuomba wana Jamii tuangalie kiundani, kweli wanasheria waendelee kuwa juu ya sheria? Hata kama wako mahakamani watetee hata kitu wasichoafiki ilmradi wapate pesa? I think it is high time that everyone has to be accountable in any job.
Wanyarwanda nao wamejitetea hivi: http://www.newtimes.co.rw/index.php?issue=14295&article=30425
Anjo
nendeni Germany,Netherland,Israel etc mseme holocaust haikutokea then mrudi kuandika hapa kilichowatokea,wewe interahamwe babukijana naona bado una fight the lost war & failed idealogue,unatakiwa kwenu ukajibu mashtaka ya genocide...acha kujificha!