Kafulila: Nina bomu zito la Escrow

ras mkweli

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
280
Reaction score
105
Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia NCCR-Mageuzi David Kafulila amesema kwamba analo bomu lingine kuhusu sakata la uchotwaji wa zaidi ya shilingi bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow.Mbunge huyo anasema kuwa bomu hilo likilipuka litatikisa serikali na vigogo waliohusika katika kashfa hiyo akiwemo Waziri wa nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
Nini maoni yako?


==========================

Chanzo: Nipashe
 
Kafulila tangu amuoe yule dada wa chadema naye ameanza kutisha watu kanachekesha kweli.
 
Sasa ndo nini hii... Kama unao ushahidi dhidi ya mtu ni bora uutoe hadharani..
Kuzidi kuubana huo ushahidi ni sawa na kumuweka kiporo huyu mtuhumiwa!!

Hii ni lugha ya wabunge wala rushwa anatishia kwamba niletee mzigo wa hela nisitoe siri.Ndio maana kasema wazi Muhongo limalize ili nisimwage siri.Kusema hadharani ni kutishia kuwa usiponipa hela mimi na wewe.

Kafulila na Zitto ndio staili zao za kudai rushwa si kwamba wana uzalendo.Katika wabunge wala rushwa waliokubuhu ni Zitto na Kafulila.
 
Kafulila Sasa utaniudhi brother,hebu njoo front umwage vitu huyo kiranja wa Wezi aondoke hapo alipo, nini kinakupa kigugumizi?

Nakiambiwa anadai rushwa kijanja atakataa....!? Kama ushahidi huo anao kabla ya maamuzi ya Bunge nitakuwa na uhakika kuwa Kafulila anadai Rushwa....mambo mazito yanaogusa maisha ya watanzania siyo ya kusubiri...Hasa unapokuwa na uhakika na jambo hilo. Kafulila jirekebishe.
 
Kafulila ni -----! Sasa Ake na topic ingine hiyo ishapita! Umaarufu kupitia escrow umefika mwisho! Afanye mambo mengine sasa!
 
Kwa hiyo kwa lugha ingine alificha ushahidi alipotakiwa kutoa kwa Takukuru na CAG? Nakumbuka aliitwa kutoa ville zo!
 
Kama Upo ni bora auweke wazi kwa uma...isijekuwa kama list ya walioficha pesa nje ya nchi ilivyomtia kigugumizi Zitto mpaka leo
 
Safi sana......mbona hadi leo mwigulu hakuwahi toa ushahidi flani. Akiutoa sasa hivi watachakachua. Abaki nao hadi muda muafaka. Ni strategy nzuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…