Kafulila na Hamad Rashid wametoswa?

Wanaandaliwa zawadi nono toka kwa mabwana zao CCM kwa kazi nzuri ya kuivuruga kambi ya upinzani bungeni.
 
"Nimefurahi kazi yetu ya jana (juzi) imesaidia Mrema na Cheyo wamepata uenyekiti wa kamati zinazotakiwa kuongozwa na wabunge wa upinzani," alisema Hamad.

Mrema na Cheyo kuongoza kamati za bunge kwa niaba ya upinzani ni kuimarisha upinzani bungeni???? Hawa kila kukicha hawaachi kuisifia CCM. Hamad mwenyewe alimfukuza Cheyo uwaziri kivuli kwenye bunge lililopita. Leo amesahau au anataka kutuambia Cheyo amebadilika? Mkiambiwa mmetumwa kuja kuharibu kambi ya upinzani mnahamaki lakini ukweli wenyewe unaonekana.
 
Back
Top Bottom