Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 1,555
- 1,153
Mkurugenzi Mkuu wa PPP nchini Bw David Kafulila kupitia kipindi cha DK 45 kinachorushwa na runinga ya ITV ameeleza kuwa Mwekezaji aliyewekeza kwa Ubia na Serikali ya Paul Kagame ya Rwanda kwa thamani ya zaidi US$ 60M ameonesha nia ya kutaka kuwekeza katika Sekta hiyo ya maji hapa nchini.
Aidha, Mkurugenzi huyo Mkuu Bw David Kafulila amesema watakaa na kuangalia kama tunaweza kumpokea na kuingia nae mkataba ili asaidie kusambaza katika baadhi ya Majiji ili kuongeza kasi ya ushindani katika Usambazaji na utoaji wa maji na salama kwa wananchi wetu.