Kafulila aifagilia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kafulila aifagilia CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by howard, Mar 2, 2011.

 1. howard

  howard Senior Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  NAHISI KAMA KUCHANGANYIKIWA KUNA THREAD NYINGINE HUMU INAONYESHA KAFULILA KAIPONDA CHADEMA NA HII JE?

  MBUNGE wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi) amemshangaa Rais Jakaya Kikwete kuogopa kazi nzuri inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kuzungumza na wananchi.
  Licha ya kumshangaa rais Kikwete kwa hofu aliyonayo amekipongeza CHADEMA na kusema chama chake kinajipanga kwenda kwa wananchi kwa kuwa ni utekelezaji wa kazi za siasa.
  Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya NCCR-Mageuzi Dar es Salaam jana, Kafulila aliyewahi kuwa kada wa CHADEMA, alisema hofu ya kupinduliwa aliyonayo rais inatokana na watawala kushindwa kutimiza wajibu wao na kusababisha wananchi wengi kukata tamaa.
  Mbunge huyo aliweka wazi msimamo wake kwamba licha ya kutofautiana kwenye baadhi ya mambo na chama alichokuwepo mwanzo alisema kazi nzuri inayofanywa na CHADEMA mikoani inastahili kuigwa na vyama vingine.
  Alisema sababu ya kutoweka kwa hali ya amani nchini sio wanasiasa bali ni watawala kushindwa kutimiza wajibu wao hivyo ni rahisi kwa waliokata tamaa kufanya lolote watakaloona inafaa.
  “Rais Kiwkete ni rais wetu namheshimu lakini katika hili natofautiana nae…CHADEMA wapo mikoani wanazungumza na wananchi, hiyo ni kazi ya chama chochote cha siasa binafsi nawapongeza, mimi na chama changu tunawaunga mkono. Wapo sahihi kabisa.
  “…Hata sisi tutakwenda kwa wananchi tutafanya mikutano, unajua kuvunjika kwa amani ni matokeo ya watawala kushindwa kutimiza wajibu wao sasa wananchi wanakata tamaa wanaamua kufanya yao,” alisema Kafulila.
  SOURCE: TANZANIA DAIMA
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Anakumbuka too late kuwa yuko kwenye chama bogus!
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kweli Kafulila ni mbunge wa watanzania, tatizo chama alichojiunga nacho!!!!
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,758
  Likes Received: 6,062
  Trophy Points: 280
  Hawa NCCR-Mageuzi (Kafulila na Mwenyekiti wao) are the stupidiest politicians existing in the country today. Yaani wala hawaeleki wanachokitaka. Mara leo unaongea hivi, kesho unaongea vile. Kwenye siasa ni lazima uwe na msimamo na malengo yanayoeleweka wazi badala ya undumilakuwili.

  Hivi majuzi (Kafulila) walivyoshirikiana na CCM/CUF kuwadhihaki na kuwazomea CDM walivyopinga ukiukwaji wa taratibu na sheria halafu ghafla leo "unawafagilia" tumweleweje? Kaka (Kafulila na wengineo) usijifanye mnafiki baada ya kuanza kuona matunda bali tangu mwanzo uwe sehemu ya harakati za kuyatafuta hayo matunda.
   
 5. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kafulila amefanya vizuri kuwapongeza CHADEMA kwasababu wanatetea maslahi ya taifa hili ila ni kigeugeu, haaminiki na ajue kuwa waliompa ubunge hawakumtaka aende bungeni kutetea mafisadi na maslahi yake binafsi!! Viva CHADEMA!!
   
 6. G

  Giroy Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Simshangai sana Kafulila kwa utoto wake. Mtu mbovu,mnafiki,ni James Mbatia huyo jamaa tangu amekuwa mwenyekiti nccr kazi yake ni kuwabomoa wapinzani wenzake,badala ya kujenga chama chake.simpendi kabisa huyo jamaa.Kafulila kaingia choo cha kike.
   
Loading...