Kafulila agonga mwamba

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]JUMAMOSI, SEPTEMBA 08, 2012 08:48 NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali ombi dogo la pingamizi la kesi ya msingi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa NCCR-Mageuzi, lililowasilishwa mahakamani hapo na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.
Kwa mujibu wa Mwanasheria wa NCCR-Mageuzi, Mohamed Tibanyendera, ombi hilo dogo lilikataliwa jana mahakamani hapo, baada ya kasoro za kisheria kubainika katika hati ya kiapo cha Kafulila alichokiwasilisha katika mahakama hiyo.

Tibanyendera alisema kwamba, kesi hiyo namba 218 ya mwaka 2011 inayosikilizwa na Jaji Alice Chinguwile, pamoja na kukataliwa kwa ombi hilo la Kafulila, shauri hilo liliaihirishwa hadi Novemba 22, mwaka huu.

Alisema kesi ya msingi ya pingamizi lililopelekwa mahakamani hapo na Kafulila, akipinga kuvuliwa uanachama kupitia kikao cha dharula cha Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho, haijaanza kusikilizwa.

Kwa upande wake, Kafulila, alipoulizwa na MTANZANIA ili kupata maoni yake, alisema hana taarifa za ombi hilo dogo kutupwa na mahakama hiyo kwa sababu, hakuwapo mahakamani hapo na wala hajui kama kesi hiyo ilisikilizwa jana.

Hata hivyo, alisema atawasiliana na wakili wake kisha atatoa taarifa za kilichoendelea mahakamani hapo.

Kafulila na wajumbe wengine sita akiwamo aliyekuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Hashim Rungwe, walivuliwa uanachama wa NCCR-Mageuzi Desemba mwaka jana.

Kafulila, Rungwe na wenzao walivuliwa uanachama baada ya wajumbe wa NEC kudaiwa kutoridhishwa na mwenendo wao kisiasa.

Wakati wanachama hao wa chama hicho cha upinzani wakivuliwa uanachama, kulikuwa na taarifa za kutokea kwa vurugu, ambapo askari polisi walifika eneo uliokuwa ukifanyika mkutano, Kinondoni Dar es Salaam na kukuta hali ni tulivu.

Wakati Kafulila na wenzake hao wakifutiwa uanachama, Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali kupitia chama hicho, alipewa onyo kali baada ya wajumbe hao kuonyesha kutoridhishwa na mwenendo wake kisiasa.

 
TOTAL RECALL... POLITICAL GREED sometimes succumbs MENTAL RETARDATION
 
Sitaki kusikia uchaguzi mdogo..zilizofanyika zinatosha. Lets concentrate on other develoment issues. uchaguzi sasa basi!!
 
Waanzilishi wa ADC bana dah!

Kwa taarifa yako muasisi wa ADC ni Ahmad Rashid Mohamed na wanachama wengine wa CUF.Labda kama akina Kafulila wajiunge nacho tu. Eti mdhamini wa ADC awe mwanachama wa chama kingine? (Kama Ahmad Rashid bado ni mwanachama wa cuf mpaka mahakama itakapotengua maamuzi ya cuf yaliyomfukuza) alafu anajidai kuwa yeye ni mlezi tu ADC, hajui hata kudanganya?
 
dogo ni moja kati ya threat kwa serikali bungeni... sijui kama atachomoka kwenye hii kesi
 
Sitaki kusikia uchaguzi mdogo..zilizofanyika zinatosha. Lets concentrate on other develoment issues. uchaguzi sasa basi!!
Napenda urudiwe ili baadhi ya mambo yaweze wekwa clear.Katika hizo chaguzi CCM wanaweza jitathimini kama wao ni brand tena, au kama ni kinachoweza kipaumbele pale vyam tofauti na CDM wakiachi jimbo.
 
Back
Top Bottom