Kadri unavyo iacha pwani ndio kadri unavyo kutana Mapishi ya hovyo

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,712
6,517
Upishi uko ukanda wa pwani na kidogo mikoa kadhaa kutoka pwani, baada ya hapo hakuna mapishi, nenda huko Kanda ya Ziwa nenda jiji kama Mwanza hakuna kitu pale, chakula wanajua kujaza nyanya wakizania ndio upishi wenyewe, unakula.chakula kama unakula tope hakina radha. Nenda sijui huko Mara ni balaaa tupu kabisa kwenye upishi.

Kwa kifupi ukitoa ukanda wote wa pwani na jirarani zake huko kwingine hakuna mapishi.

Nilikaa Kigoma nyakati fulani niliondoka bila kula wali, sana nilikuwa nakula Ugari wao wa muhogo basi.
 
Nipo kanda ya ziwa,nakuunga mkono kwa hili,kuchambua mchele tu ni tatzo

Usijaribu kula chinese kanda ya ziwa lakin chinese likipikwa pwani unaweza sahau mboga zote ukawa unataka upikiwe chinese tu kila siku

Chai ya rangi sasa ni kama unakunywa dawa ukiwa kanda ya ziwa

Kanda ya ziwa wanachojua ni kuchanganya dona na unga wa mhogo na wanatoa ugali safi sana
 
Nipo kanda ya ziwa,nakuunga mkono kwa hili,kuchambua mchele tu ni tatzo

Usijaribu kula chinese kanda ya ziwa lakin chinese likipikwa pwani unaweza sahau mboga zote ukawa unataka upikiwe chinese tu kila siku

Chai ya rangi sasa ni kama unakunywa dawa ukiwa kanda ya ziwa

Kanda ya ziwa wanachojua ni kuchanganya dona na unga wa mhogo na wanatoa ugali safi sana
Ni kweli mkuu, kwenye upishi ni shida sana sio tu kanda ya ziwa bali sehemu nyingi za nchi hiii ukiacha pwani
 
Nachojua nimekula nimeshiba huko wana mbwembwe tu za mapishi.

hafu sio kila unachokipenda wewe mwenzio anakipenda wengine tunapenda ugali na mlenda kuliko kitu chochote tukija huko tutaona tu vitu vya ajabu ajabu tu.
Sijazungumzia aina ya chakula nazungumzia upishi mkuu, Mfano Chai kule pwani inawekwa viongo vya kutoasha sasa huko kwingine wanacho jua ni majani na sukari basi kazi imeisha
 
Utamu wa chakula ni mapendeleo ya mtu na mazoea ya aina ya chakula alichozoea mtu hivyo siyo kwamba sehemu nyingine hawajui kupika, sifa ya chakula chochote kizuri ni usafi chakula kilichopikwa katika hali ya usafi na kisafi katika jamii husika nikitamu na ukifanya mazoea nacho unakipenda pia.

Huko Pwani vyakula vinapikwa kwa kutumia viungo vingi na bajeti ya kupika chakula cha viungo vingi inahitajika kuwa kubwa ila wao wanasaidiwa na vitu hivyo kupatikana maeneo yao kwa urahisi ila hayo mapishi ya kuweka viungo vingi kanda ya ziwa hawayapendi wao wanapenda chukuchuku kwenye chakula cha Kila siku na vile vya kuchanganya viungo wanapenda kula mara moja moja hasa siku maalumu ambazo wamepumzika maana wanaona siyo vyakula vya kuwapa nguvu.
 
Pwani ndio mjini Toka enzi na enzi,mababu wa kipwani washafanya sana biashara ya utumwa kwenda bush huko kuwabeba wasukuma na wanayamwezi na kuja kuwauza pwani Kwa waarabu na wazungu, magorofoa pwani yapo Toka miaka ya 1700 huko wakati huo huko bara watu wanavaa magome. Usishangae pia pwani kua na asili ya misosi sababu bahari ilifanya wapwani wapate recipes nyingi tofauti tofauti.
 
Pwani ndio mjini Toka enzi na enzi,mababu wa kipwani washafanya sana biashara ya utumwa kwenda bush huko kuwabeba wasukuma na wanayamwezi na kuja kuwauza pwani Kwa waarabu na wazungu, magorofoa pwani yapo Toka miaka ya 1700 huko wakati huo huko bara watu wanavaa magome. Usishangae pia pwani kua na asili ya misosi sababu bahari ilifanya wapwani wapate recipes nyingi tofauti tofauti
Ukitoa dar mikoa mingine ya pwani kama Lindi, pwani, mtwara, na tanga Kuna umaskini wa kutisha
 
Sijazungumzia aina ya chakula nazungumzia upishi mkuu, Mfano Chai kule pwani inawekwa viongo vya kutoasha sasa huko kwingine wanacho jua ni majani na sukari basi kazi imeisha
Huo upishi upo sawa tu, kama Pwani wanatumia tangawizi na hiriki na mikoa mingine majani ya chai na sukari maana yake wengi wa hilo eneo wanapenda chukuchuku na ukipenda kutengezewa hiyo ya viungo pia unatengezewa ni kiasi cha kwenda na ingredients zako tu kama ni mamantilie ila hotel zote za mikoa yote zina menu Kuna Tea masala na chai kama chai isiyo na viungo ni wewe tu kuchagua, ila na mazingira nayo tunayokula ndo shida hasa huko mamantilie wanapika vyakula vinavyopatikana sehemu husika kibaya ni uchafu tu ila chakula kisafi wewe kula kulingana na jamii husika.
 
Mtoa Uzi naweza nikasema una upeo mdogo sana wa maisha yaani kitu usichokipenda wewe basi wanachokipenda ni wajinga au kitu usichokizoe unakiona kibaya.

Mfano ukienda Uganda vyakula vingi wanachemsha hawakaangi kama huku Tanzania, mganda akija Tanzania atalalamika chakula Cha huku ni kibaya sababu yeye amezoea kula vyakula vya kuchemsha.

Ukienda afrika ya kati utashangaa kuona viwavi jeshi wanakula kama mboga, ukienda china au India utashangaa sana kuona vyakula wanavyokula vya ajabu ajabu.

Mazoea yako ya vyakula vya pwani yasiwe ni tiketi ya kuona jamii nyingine hawajui kupika, wao pia wanaona vyakula vya pwani ni vibaya ni mazoea tu ndo naweza sema hivyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom