Kadi za Kieletroniki kwa usafiri wa Mabasi mwendo kasi kuanza kutolewa leo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,720
55,858
13501734_925760307534944_5149549392710075541_n (1).jpg

Kadi za kieletroniki kwa ajili ya wasafiri wa mabasi yaendayo haraka katika jiji la Dar es Salaam zitaanza kutolewa leo katika juhudi za kupunguza msongamano wa kununua tiketi za karatasi.

Wauzaji wa tiketi hizo MaxMalipo na Shirika la Usafiri Dar es Salaam UDA kitengo chake cha mradi wa mabasi yaendayo haraka wamesema tiketi hizo za kieletroniki zitauzwa katika vituo vikubwa kwa shilingi elfu tanio na mnunuzi atahitaji kusajil ili hata kama kadi yake itapotea akiba ya fedha iliyokuwa imebaki iingizwe kwenye kadi mpya atakayopewa.

Mkurugenzi mtendaji wa UDART, David Mgwassa amesema kadi hizo zitaanza kuuzwa kesho katika vituo vikuu vya mabasi vya Kimara, Ubungo, Morocco, Gerezani na Kivukoni.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Maxcom Afrika ambao ndiyo watengenezaji wa kadi hizo, Juma Rajab amesema bei ya kadi hiyo ni Sh 5,000 na itakuwa na Sh 4,500 ndani yake ambazo abiria anaweza kuzitumia kama nauli kwa safari nane.

Ameaema kadi hizo hazitakuwa na namba ya siri na kuwa kiwango cha juu kitakachowekwa katika kadi hiyo ni Sh30,000.
 
Hii inaitwa unasafiri bila nauli mfukoni ukiwa na kadi tu we wapiga route zako saafi japo nayo hii ni changamoto kwa waswahili kama Sie tusiojua maana ya kadi namna ya kuitunza na kutembea nayo coz utakuta kuna watu wanasafiri au kutembea tembea bila ya hata kitambulisho tu
 
Wale kina kajamba nani tunaotoka kimara had kivukon..Tukiamka tunasachi kibubu tunatoa mia tano,tukipapasa mfukoni nguo nlovaa jana nakutana na mia mbili..Mia saba hiyo naparamia kitu cha mwendo kas...Sasa hii budget ya kujaza credit nauli ya elfu thelathin kwenye hiyo kad niitoe wapi mie??
Wapande tu wafanya kazi mi narud kwenye daldala.
 
Hiyo kadi inauzwa bei ghali sana, mathalani kwa Mtanzania mwenye kipato cha chini asubuhi anaianza na jero mfukoni. Hizo kadi zingeuzwa buku tu, na credit zinunulike kirahisi kwa tigopesa, mpesa, halomoney na zingine bila matozo ya ziada.
 
Wale kina kajamba nani tunaotoka kimara had kivukon..Tukiamka tunasachi kibubu tunatoa mia tano,tukipapasa mfukoni nguo nlovaa jana nakutana na mia mbili..Mia saba hiyo naparamia kitu cha mwendo kas...Sasa hii budget ya kujaza credit nauli ya elfu thelathin kwenye hiyo kad niitoe wapi mie??
Wapande tu wafanya kazi mi narud kwenye daldala.
Hapo mleta uzi amesema.....
Kadi itauzwa kwa bei ya shilingi 5000.
Kisha ndani ya kadi panakua na salio la 4500 ambazo zitaweza kutumika kwa safari zako mara nane.
Na kwa kila kadi moja unaweza ukaweka salio hadi la 30,000 tu.
 
Tshs 4,500 / 8 routes = Tshs 562.5 per route, ukisema aghali watasema nenda kwa kusota kama ilivyokuwa kupiga mbizi ferry
 
Hapo mleta uzi amesema.....
Kadi itauzwa kwa bei ya shilingi 5000.
Kisha ndani ya kadi panakua na salio la 4500 ambazo zitaweza kutumika kwa safari zako mara nane.
Na kwa kila kadi moja unaweza ukaweka salio hadi la 30,000 tu.
Mi nimeelewa bt naongelea wale wasio na hata uhakika wa mlo wa kesho,,sembuse nauli!sasa hiyo 4500 ikishaisha kwa hizo safar nane watapata vp pesa za jumla kwa usafiri? hata kuongeza elf kumi wanashindwa.Si watarud kweny daladala tu
 
Hii inaitwa unasafiri bila nauli mfukoni ukiwa na kadi tu we wapiga route zako saafi japo nayo hii ni changamoto kwa waswahili kama Sie tusiojua maana ya kadi namna ya kuitunza na kutembea nayo coz utakuta kuna watu wanasafiri au kutembea tembea bila ya hata kitambulisho tu
vilevile namna ya kuitunza isiharibike maana siku tatu tu utakuta haiwezi kutambuliwa na mashine mara imekunjwa kunjwa, imechubuka, n.k. Lakini kibaya zaidi ni kuibiwa na mateja wa jiji
 
Nimenunua hio kadi yao aisee ni nzur na hata kwenye zile get zao inasoma fasta kuliko tiket... Ni nzur kiujumla ila zinahitaj maboresho kw mfano: kuangalia salio ni mpaka kituoni ila ingekua poa kama mtu ungekua unaweza ukaangalia salio hata kwa simu yako au kwa mtandao .. Yan kiufupi iwe na njia mbadala za kuangalia salio kama ilivyo kwenye kuongeza salio... Ni hayo tu
 
Wale kina kajamba nani tunaotoka kimara had kivukon..Tukiamka tunasachi kibubu tunatoa mia tano,tukipapasa mfukoni nguo nlovaa jana nakutana na mia mbili..Mia saba hiyo naparamia kitu cha mwendo kas...Sasa hii budget ya kujaza credit nauli ya elfu thelathin kwenye hiyo kad niitoe wapi mie??
Wapande tu wafanya kazi mi narud kwenye daldala.

Utaratibu wa ticket unaendelea kubaki kama kawaida.
 
Mi nimeelewa bt naongelea wale wasio na hata uhakika wa mlo wa kesho,,sembuse nauli!sasa hiyo 4500 ikishaisha kwa hizo safar nane watapata vp pesa za jumla kwa usafiri? hata kuongeza elf kumi wanashindwa.Si watarud kweny daladala tu
Naamini watakua na salio kiasi kidogo kwaajili ya watu kuweza ongeza salio kutokana na vipato vyao
 
Back
Top Bottom