KADI: Hadithi kali, fupi

KADI: Hadithi kali, fupi

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,315
KADI
Hadithi fupi, kali: iliyoandikwa miaka zaidi ya karne moja iliyopita. Imefasiriwa kwa Kiswahili na Wako Mtiifu.

Richadi Buruweli, wa New York, hataweza kamwe kuacha kujuta kwa nini lugha ya Kifaransa haikuwa sehemu ya mafunzo yake.

Hii ndio sababu:

Siku ya pili jioni baada ya Buruweli kuwasili Paris, alijihisi mpweke pasipo mkewe na bintiye, ambao walikuwa bado wanamtembelea rafiki kule London, mawazo yake taratiib yakielekea kwenda kwenye burudani. Hivyo, baada ya kuangalia kalenda ya burudani, aliamua kutembelea Folies Bergère, ambako alikusikia kuwa moja ya vivutio vizuri. Wakati wa mapumziko alienda kwenye bustani nzuri, ambapo makundi ya watu wenye furaha walizurura baina ya maua, na taa, na maji yabubujikayo. Alipokuwa amekaa tu kwenye meza ndogo yenye miguu mitatu, mandhari ya kuvutia ikiwa mbele yake, ndipo macho yake yalipovutiwa na binti mrembo, aliyevalia kisawasawa, japo kwa kuzingatia maadili, aliyepita karibu naye, akimuegemea jamaa moja aliyekuwa naye. Kitu pekee alichobaini kuhusu mwanaume huyo kilikuwa ni kwamba alikuwa amevaa mawani.

Tuelewe, Buruweli hakuwa mtu wa vimwana, na hakuamini macho yake pale mrembo yule alipomwacha jamaa aliyekuwa naye na, akigeuka kama aliyesahau kitu, akapita karibu naye, na kwa namna yake akaweka kadi mezani. Kadi ilikuwa imeandikwa maneno fulani ya Kifaransa kwa wino wa rangi ya hudhurungi, lakini kwa vile hakuijua lugha ile, hakuweza kuelewa nini maana yake. Yule binti hakumwangalia zaidi, bali, akijumuika tena kwa yule jamaa aliyevaa miwani, aliondoka mahali pale kwa heshima na taadhima mithili ya binti mfalme. Buruweli alisalia palepale akiitazama kadi ile.

Kwani inahitaji kusema kwamba, hakuweza tena kutafakari burudani au vivutio vingine vilivyokuwepo. Kila kitu kilionekana kinaboa na michosho tu kulinganisha na maono yenye nuru aliyoyaona na kutoweka kwa namna ya kushangaza. Shauku yake kuu sasa ilikuwa ni kubaini maneno yaliyoandikwa kwenye kadi.

Akaita bodaboda, akaenda mpaka Hôtel Continental, ambako ndiko alikofikia. Alienda moja kwa moja ofisini na akimchukua meneja chemba, alimuuliza iwapo angemfanyia hisani kumfasiria maneno mawili matatu ya Kifaransa kwa Kiingereza. Maneno yote yaliyokuwapo hayakuzidi ishirini.

(edit 1)
“Hilo tu,” alisema meneja, na kwa upole wa Wafaransa, alitupia macho yake kwenye ile kadi. Na kadiri alivyokuwa akisoma, sura yake ilikunjwa kwa mstuko, na, akimwangalia Buruweli kwa makini, alimuuliza:

“Umeipata wapi kadi hii, mkuu?”

Buruweli alianza kujieleza, lakini alikatizwa hivi: “Inatosha, inatosha. Ondoka hapa hotelini.”

“Una maana gani?” aliuliza jamaa yule toka New York, kwa msangao.

“Unatakiwa kuondoka hotelini sasa—hivi tunavyoongea—bila kuchelewa,” aliamrisha meneja akiwa si wa kawaida.

Sasa ilikuwa ni zamu ya Buruweli kukasirika, na akajigamba kwa hasira kwamba iwapo hakutakiwa katika hoteli hii palikuwapo hoteli nyingine nyingi jijini Paris ambako angekaribishwa. Na, kuonyesha alivyo mtu wa heshima, lakini aliyejeruhiwa moyoni, alilipa bili yake, akaagizia mizigo yake, na kuondoka akipitia Rue de la Paix mpaka
Hôtel Bellevue, ambako ndiko alikolala.

Edit 2
Kesho yake asubuhi alikutana na mmiliki, ambaye alionekana ni mtu mtaratibu, na, akiwa anataka kuangalia matukio ya jioni iliyopita kama yalivyo ya kustaajabisha, Buruweli alieleza kilichomsibu, na alifarijika kupata mtu aliyemsikiliza kwa makini.

“Huyo jamaa zitakuwa hazimtoshi,” alisema mmiliki. “Ngoja niione hiyo kadi; nitakuambia ina maana gani.” Lakini kadiri alivyokuwa akiisoma, uso wake na alivyo vilibadilika mara moja.

“Hili ni jambo kubwa,” alisema kwa ukali. “Sasa naelewa kwa nini afisa wangu wa mapokezi alikataa kukuhudumia. Nisamehe tu mkuu, lakini inanibidi kufanya kama alivyokufanyia.”

“Una maana gani?”

“Huwezi kuendelea kubakia hapa.”

Akisema hivyo aligeuka akikanyagia kisigino, na mgeni aliyegadhibika hakuweza kumshawishi aendelee kumsikiliza.

“Tutaona,” alisema Buruweli, kwa hasira kali.

Edit 3

Hapo ilishakaribia kufika adhuhuri, na mtu wetu huyu toka New York alikumbuka mipango aliyoagana na rafikiye wa Boston, ambaye akiwa na familia yake, alikuwa amefikia Hôtel de l'Alma. Akiwa na mizigo yake kwenye gari la kukodi, alimuagiza dereva aendeshe moja kwa moja kwenda huko, akidhamiria kupata ushauri kwa mzalendo mwenziwe kabla ya kuchagua sehemu nyingine ya kufikia.

Rafiki yake aligadhibika sana aliposikia kisa chake—jambo ambalo lilimpa Buruweli faraja si kidogo, akitambua, kama kwake pia, kwamba rafikiye alikuwa mweledi wa tamaduni za watu kutokana na kuishi kwa muda mwingi ughaibuni.

“Patakua na makosa ya kijinga tu mahali, rafiki mpendwa; ingekuwa mimi wala nisingejali. Agizisha tu mizigo yako waishushe nawe ukae hapa. Lakini, awali, ngoja nikuandalie ‘kishusha pumzi’ kidogo.”

Baada ya kupata ‘mashtuzi’ kidogo ya vitafunwa vyao vya ki-Manhattan, rafiki wa Buruweli aliomba udhuru kidogo ili akawaite kina mama.

Alikuwa ametoka tu kidogo hatua mbili tatu pale alipogeuka, na kusema:
“Acha tuione kadi yako ya kustaajabisha iliyoleta zahma yote hii.”

Haikuchukua duru toka ainyakue mkononi mwa Buruweli pale alipostuka na kusema:—
“Mungu wangu, aisee! Unataka kuniambia—hii kwa kweli—”
Kisha, kwa mwendo wa ghafla aliweka mikono kichwani mwake, akaondoka pale.

Edit 4
Alikuwa ameondoka kama dakika tano hivi, na aliporudi sura yake imesawajika.

“Nisamehe sana,” alisema kwa mashaka; “lakini wale wakina mama wananiambia—yaani, mke wangu—kichwa kinamuuma sana. Hatutaweza kupata lanchi pamoja.”

Mara moja akibaini kwamba hii ilikuwa ni sababu geresha tu, na akiumizwa sana na matendo haya ya rafiki yake, mtu huyu aliyestaajabishwa aliinuka mara moja na kuondoka bila kusema neno. Nini inaweza kuwa maana ya maneno yaliyoko kwenye kadi ile maaluni?

Akinufaishwa na uzoefu huu dhalili, alichukua tahadhari kubwa kutomuonyesha kadi ile mtu yoyote kwenye hoteli ambayo sasa alihamia,—mahala fulani tulivu karibu na Nyumba ya Sanaa.

Mchana kutwa hakufikiria kitu kingine isipokuwa ile kadi, na akatafakuri njia anuai za kubaini maana yake bila kujidumbukiza kwenye matatizo zaidi.

Jioni ile alienda tena kule Folies Bergère akitumai angeweza kumuona yule mwanamke asiyejulikana, kwani sasa alikuwa na hamasa kuu mno kutanabahi yu nani.

Au labda alikuwa ni mmoja wa wale magaidi, au, pengine, ni jasusi wa Urusi, kama ambavyo amekuwa akisoma katika simulizi mbalimbali za vitabuni.

Lakini hakufanikiwa kumpata, si siku ile wala jioni nyingine tatu zilizofuatia ambazo alipita tena palepale. Wakati huo kadi aliihisi kuwa kana kwamba ni kaa la moto mfukoni mwake. Alihofia kukutana na mtu yeyote anayemfahamu, wakati wingu hili la kutisha likiendelea kumzingira.

Alinunua kamusi ya Kifaransa-Kiingereza na kujaribu kupata maana neno moja baada ya jingine, lakini hakufaulu. Aliona yote ni Kichina tu. Kwa mara ya kwanza maishani mwake, Buruweli alijuta kwanini hakusoma Kifaransa wakati alipokuwa mwanachuo.

Baada ya jitihada nyingi zisizo na tija za ama kutatua au kusahau kitendawili kile kitesi, hakuona njia nyingine zaidi tena ya kuwasilisha tatizo lake kwa kampuni ya upelelezi.

Hivyo, alikabidhi inshu yake kwa agent de la sûreté aliyeshuhudiwa kuwa mweledi na mtu ambaye ni wa kuaminiwa.

Waliongelea chemba, na, haswaa, Buruweli alimuonyesha ile kadi. Alifarijika kuona mpelelezi wake hakuonesha dalili yoyote ya mstuko. Ila tu hakueleza wala kutaka kueleza nini maana ya maneno yale.

“Ni vema,” alisema, “kwamba bosi wangu asijue chimbuko la kadi hii kwa sasa. Nitakuwa na heshima ya kukuona bosi wangu kesho hotelini kwako, na hapo bosi wangu atajua kila kitu.”

“Kwa hiyo ni jambo kubwa?” aliuliza mtu yule mwenye masaibu.

“Kubwa sana,” ndilo lilikuwa jibu.

Saa ishirini na nne zilizofuata zilimpitia Buruweli akiwa kwenye homa ya shauku. Wakati akili zake zikiumba uwezekano wa kuogofya mmoja baada ya mwingine, alijuta sana kwa nini hakuichanilia mbali kadi ile maaluni tangia mwanzo. Hata hapo aliinyakua—akijiandaa kuichanachana vipandevipande, ili kuhitimisha zahama lote lile. Lakini hapo ubishi wake wa Kimarekani ulijitokeza tena, na akaamua kupambana mpaka mwisho, liwalo na liwe.

“Kwanza,” alijifariji, “siyo kosa kwa mwanamume kuchukua kadi ambayo mrembo amemuwekea mezani kwake.”

Edit 5

Iwe kosa, au isiwe kosa, lakini, ilionekana ni kama vile amefanya kosa fulani zito sana pale ambapo, kesho yake, mpelelezi wake alikuja na gari, akiambatana na askari mpelelezi, na kumtaka Mmarekani huyu aliyekanganyikiwa aongozane nao kwenda makao makuu ya polisi.

“Juu ya nini?” aliuliza.

“Ni utaratibu tu wa kawaida,” alisema mpelelezi; na pale Buruweli alipozidi kulalamika, askari aliyevaa yunifomu alisema: “Tii bila shuruti, monsieur; hakuna namna nyingine, tunaondoka nawe.”

Ilipopita saa nzima baadaye, baada ya mahojiano mazito na afisa mwingine wa polisi, ambaye alitaka taarifa nyingi kuhusu umri wa Mmarekani huyu, mahali alipozaliwa, makazi, kazi, n.k., jamaa hakuamini macho yake alipojikuta ameswekwa mahabusu.

Kwa nini yuko pale au nini kitakachofuatia, Buruweli hakuwa na miundombinu ya kuelewa; lakini kabla siku haikuisha alifanikiwa kutuma ujumbe kwa Ubalozi wa Marekani, ambako alitaka mara moja apewe ulinzi wanaoustahili raia wa Marekani.

Hata hivi, ilifika jioni, pale Mheshimiwa Balozi, mtu mwenye hadhi yake, alipofika gerezani. Hapo palikuwa na mahojiano makali, ambako mtuhumiwa alitumia maneno makali, maafisa wa Ufaransa nao wakinyosha mikono na kuongea haraka sana na Balozi akisikiliza kwa makini pande zote mbili, akisema machache, na kuvuta sigara ya aina yake.

“Nitawasilisha suala lako kwa Mheshimiwa Waziri Marekani,” alisema wakati akiinuka ili aondoke, “ na nitakufahamisha matokeo hapo kesho.”

“Lakini hii siyo haki kabisa. Una maana unataka kusema—"

Hata hivyo, kabla hajamaliza, Balozi, akimtupia jicho la kutuhumu, aligeuka na kuondoka pale.

Usiku huo Buruweli alilala lupango.

Kesho yake asubuhi alitembelewa tena na Balozi yule asiyeshawishika, ambaye alimuarifu kwamba taratibu zimekamilika, na kwamba ataachiwa huru hivi punde.

“ Hata hivyo, yanibidi kukuambia,” alisema, “kwamba ni kwa jitihada kubwa mno ndio tumefikia hapa, na kuachiwa kwako kunakuja na sharti kwamba uondoke hapa nchini ndani ya saa ishirini na nne, na kwa vyevyote vile usirudi hapa tena.”

Buruweli alikasirika, hasira kali, na kubembeleza; lakini haikufaa kitu. Balozi hakuyumbishwa, lakini hata yeye alikataa katakata kutanabahisha chanzo cha uonezi huu mkubwa.

“Hii hapa kadi yako,” alisema, akimpatia bahasha kubwa iliyofungwa kwa lakiri na muhuri wa Ubalozi. “Nakushauri uichome moto na uachane kabisa na suala hili.”

Usiku ulipofika, jamaa alipanda treni kwenda London, moyo wake ukiwa umejaa chuki dhidi ya taifa zima la Ufaransa, akiwa na dhamira kali ya kulipiza kisasi.

Alimtumia ujumbe mkewe wakutane stesheni, na kwa muda mrefu alijiuliza iwapo amweleze mkewe ukweli huu unaouma. Mwishowe aliona ilikuwa ni busara kukaa kimya.

Edit 6

Lakini, alipomuona tu, machale yake kama mwanamke yalimwambia mumewe anataabika na mawazo mazito. Na Buruweli haikumchukua muda kubaini kwamba haingewezekana kumficha mkewe siri hii nzito, hasa pale alipoanza kuzungumzia safari yao waliyoipanga kuzurura ndani ya Ufaransa.

Ni wazi kabisa hakuna kisingizio chochote kingemridhisha kwa nini Buruweli amekataa kusafiri, kwa vile walikuwa wameisubiri safari hii kwa hamu kwa miaka mingi; na sasa ilikuwa haiwezekani tena kwake kukanyaga ardhi ya Ufaransa.

Hivyo hatimaye alimwambia mkewe kisa kizima, mke akicheka au kulia mara hii au ile. Kwake, kama ilivyokuwa kwa Buruweli, haikuyumkinika kwamba masaibu makubwa vile yangetokana na jambo dogo vile, na kwa vile alikuwa ni mwanazuoni mweledi wa Kifaransa, alitaka kuiona kadi ile maaluni.

Mumewe alijaribu, pasi na fanaka, kupotezea suala hilo kwa kupendekeza wasafiri kwa kupitia Italia. Mkewe hakukubali kitu mpaka aione kadi ile ya kustaajabisha ambayo sasa Buruweli alishawishika ilimpasa awe ameshaiteketeza muda mrefu uliopita. Baada ya kumkatalia kwa muda mrefu, hatimaye alikubali matokeo. Lakini, ingawa alishajifunza kuhofia matokeo ya kuionyesha kadi ile iliyolaaniwa, hakuamini macho yake na kile kilichofuatia.

Edit 7

Aliisoma, rangi ya mwili ikapauka, akavuta pumzi kwa tabu, na almanusura adondokee sakafu.

“Nilikwambia usiisome,” alisema; na kisha, akimuonea huruma anavyoteseka, aliushika mkono wake na kumbembeleza atulie. “Walau basi niambie kadi inasema nini,” alisema. “Tutastahamili yote haya kwa pamoja; niamini tu.”

Lakini mkewe, kama vile aliyezidiwa na ghadhabu kali, alimsukumilia mbali na kusema, kwa aina ya sauti ambayo hakuwahi kumsikia akiitoa, kwamba aslan, kamwe, hawezi kuishi naye tena. “Wewe ni zimwi!” alipayuka. Na hayo ndio yalikuwa maneno ya mwisho aliyoyasikia kutoka kinywani mwake.

Baada ya kushindwa kwa jitihada zote za mapatano, mtu wetu huyu alieanza kuheuka, alipanda meli ya kwanza iendayo New York, akiwa amepata zahma kubwa zaidi ndani ya siku ambazo hata hazifiki majuma mawili kuliko alizowahi kuzipata maisha yake yote yaliyopita. Safari yake ya kujiliwaza ilikuwa imetibuliwa, alikuwa ameshindwa kukamilisha madili muhimu ya biashara, na sasa ndoa yake ilikuwa imevunjika na furaha yake kupotezwa.

Edit 8

Wakati wa safari karibu muta wote alibakia chumbani, akilala kifudifudi kwa machungu. Katika huzuni yake jambo moja lililompa tumaini lilikuwa ni wazo la kuonana na mmiliki mwenzie wa biashara, Bwana Jaki Eveli, rafiki wake wa utoto, wakishirikiana mafanikio, jasiri sana, rafiki sana wa kutegemewa nyakati zote.

Akikabiliwa na hali isiyofaa kama hii, alihisi busara za Eveli zitamsaidia kuepuka masaibu yake haya. Alipofika tu New York, hakukawia kuharakia pwani na kupeana mikono na mshirika wake, aliyekuwa amekuja kumpokea bandarini.

“Jaki,” lilikuwa ndilo neno lake la kwanza, “Niko kwenye taabu kubwa, nawe ndie mtu pekee duniani awezaye kunisaidia.”

Saa moja baadae Buruweli aliketi meza ya maakuli ya rafiki yake, wakiongelea yaliyotukia. Eveli alikuwa mpole, na mara kadhaa macho yake yalimjaa machozi wakati akisikiliza simulizi la Buruweli.

“Richadi, kwa haraka inaonekana ni suala lisilowezekana,” alisema, “ndivyo mambo kama hayo yalivyo; lakini nitakuwa nawe liwalo na liwe; tutapambana tukiwa upande mmoja. Lakini hatuwezi kununua mbuzi kwenye gunia. Nipe kadi niione.”

“Hiyo hapo kadi maaluni,” alisema Buruweli, akiitupa kadi mezani.

Edit 9
Eveli aliifungua bahasha, akaitoa kadi, na kukodoa macho yake akiiangalia viandishi vyake vya hudhurungi.

“Unaweza kuisoma?” Buruweli aliuliza kwa hamasa.

“Pasi na shida,” mshirika wake alisema. Kufumba na kufumbua, rangi ya ngozi ikamgeuka, na sauti yake ikabadilika. Kisha akamshika mkono rafiki yake, na kuendelea kuushikilia kwa nguvu.

“Richadi,” alisema polepole, “kama mtoto wangu pekee angeletwa hapa amekufa isingenipa huzuni kubwa kama kadi hii ifanyavyo. Umeniletea taarifa mbaya kuliko zote anazoweza mtu kumpelekea mwenziwe.”

Kustuka na kusikitika kwake kulimuathiri Buruweli mithili ya hukumu ya kifo.

“Niambie, rafiki,” alilia; “usinifiche hata kitu. Nitastahamili kitu chochote kuliko sintofahamu hii itesayo. Niambie hiyo kadi ina maana gani.”

Eveli alikunywa fundo moja la kinywaji na kuketi, kichwa kikiinamishwa na kushikiliwa na mikono yake.

“Hapana, siwezi kufanya hivyo; yapo mambo ambayo mtu ni lazima asiyatende.”

Kisha akanyamaa tena, sura imekunjamana. Mwishowe akasema akimaanisha:—

“Hapana, sioni namna nyingine yoyote zaidi. Tumekuwa maswahiba kwa maisha yetu yote; tumefanya kazi pamoja na tumepambana na maisha pamoja bila kutengana. Afadhali ningeshindwa na kufa kuliko kuona haya yakitokea. Lakini hakuna jinsi inabidi kila mmoja ashike njia yake, swahiba; lazima kila mmoja ashike njia yake.”

Waliketi pale na kuongea mpaka usiku sana. Lakini hakuna ambacho Buruweli angeweza kufanya au kusema ambacho kiliweza kubadilisha maamuzi ya rafiki yake. Hakukuwa na la ziada isipokuwa kwamba Eveli anunue hisa za mshirika wake, au Buruweli afanye hivyo. Jamaa alikuwa mnyumbufu sana kwenye mapendekezo ya kulipana; alitenda kwa ukarimu, kama ambavyo siku zote huwa, lakini uamuzi wake haukutetereka; wawili hao lazima kila mmoja ashike njia yake. Na ndivyo ilivyokuwa.

Edit 10

Kwa kuondokewa na mshirika wake, Buruweli alihisi dunia imekula njama dhidi yake. Ilikuwa ndio imetimu wiki ya tatu tu tokea siku ile alipoipokea kadi ile ya ajabu; lakini kwa muda huo amepoteza kila kitu alichokiona cha maana duniani,—mke, marafiki, na biashara. Nini jamani afanye kuhusiana na kadi hii tata ndilo lilibaki tatizo lililokuwa likimsumbua.

Hakuthubutu tena kuionyesha; lakini hata hivyo hakutubutu kuiteketeza. Aliichukia; lakini hakuitupilia mbali.

Aliporudi nyumbani, aliifungia kadi ile maaluni kwenye sanduku lake la kuhifadhia nyaraka muhimu kana kwamba ilikuwa barua yenye bomu au chupa ya sumu kali.

Hata hivyo haikupita siku ambayo hakulifungua kabati ambako hilo likadi lilikuwa limefungiwa na kuiangalia tena na tena maandishi yake ya rangi ya hudhurungi.

Katika kuhangaika huku, mwishowe alidhamiria kuchukua mafunzo ya lugha ambayo kadi hii dhalimu ilikuwa imeandikwa. Na hata hivyo bado alihofia vibaya kuifikia siku ambayo angeweza kubaini maana yake ya kutisha.

Siku moja jioni, hata juma moja halikutimia tangu awasili New York, wakati akivuka Barabara ya Ishirini na Tatu akiwa njiani kwenda kwa mwalimu wake wa Kifaransa, aliona gari likipita mtaani.

Edit 11
Kwenye gari palikuwa na sura iliyomfanya mara moja aache kuangalia chochote kingine. Kadiri alivyoangalia tena alimtambua yule mwanamke aliyemletea zahma lote hili. Mara moja aliingia kwenye teksi nyingine na kumwagiza dereva amfuatie. Baada ya muda aliiona nyumba ambayo alikuwa akiishi.

Alienda hapo mara nyingi; lakini mara zote aliambiwa ana shughuli nyingi hawezi kuonana na mtu yoyote. Mara nyingine aliambiwa alikuwa mgonjwa, na siku iliyofuata aliambiwa alikuwa amezidiwa sana.

Matabibu watatu walikuwa wameitwa kumhudumia. Buruweli aliongea na mmojawapo akimwambia ana jambo muhimu mno la kumuona mwanamke huyu.

Yule daktari alikuwa mtu wa watu na alikubali kumsaidia. Kupitia kwa msaada wake, alifanikiwa kufikia jioni kuwa pembeni ya kitanda cha mwanamke huyu asiyejulikana. Bado alikuwa mrembo, japo sura yake ilikuwa imechoshwa na kuumwa.

“Unanikumbuka?” aliuliza huku akitetemeka, wakati akiinamia kitanda, kwa mkono mwingine ameshikilia bahasha yenye kadi isiyofahamika. “Wakumbuka kuniona pale Folies Bergère mwezi mmoja uliopita?”

“Ndio,” alijibu, baada ya kumuangalia sura yake kwa muda; na Buruweli alishukuru kubaini kwamba wanaongea lugha moja.

“Basi, mja wa Mwenyezi Mungu, niambie, yote haya yana maana gani?” alihema, akitetemeka kwa shauku.

“Nilikupatia kadi kwa vile nilikutaka u— u—”

Hapo kikohozi cha kutisha kilimtikisa mwili wake wote, na alijilaza akiwa hoi.

Mashaka makubwa yaliuingia moyo wa Buruweli. Haraka akaitoa kadi kwenye bahasha, na kuisogeza karibu na uso wa yule mwanamke.

“Niambie! Niambie!”

Kwa jitihada nyingi, mgonjwa yule mahututi polepole alijiinua kwenye mto, vidole vyake vikishikilia chuma cha kitanda.

Kisha macho yake yakafumbuka—kwa jitihada nyingi—na kuitazama kwa mshangao mkuu kadi ile ya tafrani, huku midomo yake iliyokuwa ikitetemeka ikifumbuka bila kutoa sauti, kama ambaye alikuwa akijaribu kuongea.
Na kadiri Buruweli, akizidiwa na hamu ya kufahamu, alivyoinamisha polepole kichwa chake kukisogelea cha mgonjwa, tabasamu dhaifu lilianza kujitokeza usoni pa mgonjwa. Mdomo ulitikisika tena, na kichwa cha Buruweli kikizidi kumsogelea, bila macho yake kuacha kuangalia mdomo wa mgonjwa.

Na kisha, kama kumsaidia mgonjwa kutegua kitendawili, aligeuzia macho yake kuielekea kadi.

Huku akipiga kelele za kutisha aliinuka, macho yakimtoka pima. Na ni kama wakati huohuo yule mwanamke aliangukia mto wake kwa nguvu.

Kila aina ya maandishi kwenye kadi yalikuwa yamefutika! Kadi ilikuwa tupu!

Yule mwanamke alikuwa amelala pale ameshafariki.

MWISHO

Edit 12

Hadithi hii inalo toleo la pili.
 
Wadhamini wanahitajika kwa ajili ya toleo la pili (na la mwisho).
 
bbjhjkhk
Na kisha, kama kumsaidia mgonjwa kutegua kitendawili, aligeuzia macho yake kuielekea kadi.

Huku akipiga kelele za kutisha aliinuka, macho yakimtoka pima. Na ni kama wakati huohuo yule mwanamke aliangukia mto wake kwa nguvu.

Kila aina ya maandishi kwenye kadi yalikuwa yamefutika! Kadi ilikuwa tupu!

Yule mwanamke alikuwa amelala pale ameshafariki.

MWISHO

Edit 12

Hadithi hii inalo toleo la pili.

Safi sana... Ipo poa...

Chapter Closed...

Cc: mahondaw
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni EquatorStory
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 
Back
Top Bottom