Kadhi mkuu amkana Ponda

Kadhi mkuu amkana Ponda

Sasa kila MTU anamkana SHEIKH PONDA? Mnadhani atabakia JELA MILELE? SUBIRINI atoke na Mnaomkana kila MTU mtakiona cha MOTO...
Cha moto kipi mkuu,kama huo ugaidi wetu tutapambana nao kwa nguvu zetu zote bila kuchoka mbaka tona la mwisho la damu!
 
sasa nimeamini kweli sheikh ponda anapigania haki ya waislamu yaani wewe ukapewe heka 40 kisarawe uachie heka 4 changombe halafu unajisifu mahali pazuri wakati hapo kwenye heka 4 umepashindwa kupaendeleza ni sawaswa namtu anapiga jabali kichwa halafu analisikitikia jabali badala ya kusikitikia kichwa chake

Mkuu lengu kuu ilikuwa ni kujenga Chuo kikuu,lakini uwezi kujenga chuo kikuu ndani ya heka 4,nadhani balaza la maulamaa ni makini sana ndiyo maana likaona ni vema chuo kikuu kijengwe kisarawe ambapo kuna heka 40!!
 
Hapa lazima mtu asomewe Albadri, shida tu sijajua atasomewa nani? sijui Bakwata au Polisi au hata DPP, ngoja tusubiri!
 
Kwani kuna mtu alitegemea Kadhi atamuunga mkono Ponda? Kadhi anachaguliwa na nani?
 
Hapa cha maana sio eneo kuwa mmetoa hekari 4 na mmepewa 40, cha msingi hapa ni thamani ya eneo husika. Chang'ombe ni mjini sana thamani yake ya hizo hekari 4 haiwezi lingana na hizo hekari 40 za porini kisarawe. Mie nina kiwanja kisarawe, hekari moja ni TZS 600,000/=, kwa hizo hekari 40 ni jumla ya TZS 24m. Kwa hizo hekari 4 za Chang'ombe ni zaidi ya TZS 200m, sasa wapi na wapi. Kwa ushahidi wa huyu Sheikh ni wazi kabisa wakina Ponda kumbe walikuwa na haki yakukomesha ufisadi huu na dhulma hii kwa mikono yao.
uko Kenya, Tanzania inakaribisha wawekezaji unaleta fujo utaeleweka, Ponda anaitambua BAKWATA ? mpaka aongoze uvamizi. hata mimi na mashaka na hilo lkn mimi ni wa dini nyingine, Mchungaji Mwingira auze maeneo ya kanisa lake mimi mkatoliki niongoze mapambano ya kupinga ,hakika jela inaninukia.kwanza wakubali Bakwata ni chombo kinachowasimamia waislam wote Tanzania kisha mengine yafuate yakiwemo Bakwata kuhoji taasisi wanazoziendesha.
 
uko Kenya, Tanzania inakaribisha wawekezaji unaleta fujo utaeleweka, Ponda anaitambua BAKWATA ? mpaka aongoze uvamizi. hata mimi na mashaka na hilo lkn mimi ni wa dini nyingine, Mchungaji Mwingira auze maeneo ya kanisa lake mimi mkatoliki niongoze mapambano ya kupinga ,hakika jela inaninukia.kwanza wakubali Bakwata ni chombo kinachowasimamia waislam wote Tanzania kisha mengine yafuate yakiwemo Bakwata kuhoji taasisi wanazoziendesha.

ni sawa mkuu,lakini ukumbuke kuwa wakristu hawana chombo kinacho simamia madhehebu yote ndio mana hakuna kuingiliana,sasa bakwata ya nini nawakati madhehebu ya waislam ni mengi?hicho chombo kisimamie upande mmoja sio wote ni kuwanyima haki wengine.
 
sasa kila mtu anamkana sheikh ponda? Mnadhani atabakia jela milele? Subirini atoke na mnaomkana kila mtu mtakiona cha moto...
atamwagia mtu tindikali aithee! Atakapotoka inabidi watu tuwe makini sana!
 
ni sawa mkuu,lakini ukumbuke kuwa wakristu hawana chombo kinacho simamia madhehebu yote ndio mana hakuna kuingiliana,sasa bakwata ya nini nawakati madhehebu ya waislam ni mengi?hicho chombo kisimamie upande mmoja sio wote ni kuwanyima haki wengine.
mkuu wakikatae chombo hicho na mambo yake yote. siyo hawakitambui mali ilizonazo wanazitambua, hivi CCm wakiamua kuuza uwanja wa kirumba mwanza CHADEMA wawaletee fujo ni haki kweli, kwa wakristo kuna BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA linahusisha maaskofu wa madhehebu yote yale makubwa, HALAFU kuna mabaraza ya maaskofu wa madhehebu yenyewe tu, mf maaskofu katoliki tanzania. sasa maamuzi ya baraza la maaskofu katoliki Tanzania , muumini au baraza la madhehebu mengine mf KKKT HAWAWEZI kuingilia maamuzi hayo. ndo maana baadhi ya waumini wamejitoa ktk madhehebu hayo, kwa sababu mbalimbali zikiwemo imani na maslahi na kujiunga na ULOKOLE lkn hawageuki nyuma kudai walikotoka maamuzi yanapopitishwa, MAKOSA ya BAKWATA hata mimi nayaona lkn hayanihusu maana hata kama wangeitisha michango toka kwa waislam wenzao ,wasingeshindwa kupata eneo kubwa na bado chang'ombe lingebaki kuwa mali yao kwa matumizi mengine au kuna ubaya gani? kama eneo hilo lingeuzwa kwa mnada[ japo sihafiki kuuza maeneo ya umma]
 
kani ponda kachaguliwa na nani na kiongozi wa kiislam anatakiwa achaguliwe na nani?

Mi simtambui Ponda, natambua legitimate leaders. Hivyo sijui aliemchagua na wala sio interest yangu kujua aliemchagua. BAKWATA wanasema ni kikundi cha kihuni, sasa najiweka mbli na vikundi vya kihuni.
 
KITAIFA
Na Tausi Ally

Posted Alhamisi,Decemba13 2012 saa 22:12 PM

KWA UFUPI


Baada ya kuambiwa hivyo, Habibu alidai kuwa hakuna hata mmoja anayefamfahamu katika utendaji wa kazi za Uislamu kama kiongozi kwenye baraza lakini akawatambua kimavazi kuwa ni waumini wa Kiislamu. “Ila kwa kuona, muungwana ishalaa inamuonyesha kuwa kuna baibui, kanzu na kofia (baraghashia) inaonekana kuna Waislamu na wasio Waislamu.”



KADHI Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Habibu (49) amekana kumfahamu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shekhe Ponda Issa Ponda na wafuasi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.



Habibu alikana kumfahamu Ponda na wafuasi wake jana Mbele ya Hakimu Mkazi, Ritha Tarimo mara baada ya kutakiwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka awatazame kina Ponda na aelezee iwapo kuna mmoja aliwahi kuingia kwenye Baraza la Maulamaa wa Bakwata.



Baada ya kuambiwa hivyo, Habibu alidai kuwa hakuna hata mmoja anayefamfahamu katika utendaji wa kazi za Uislamu kama kiongozi kwenye baraza lakini akawatambua kimavazi kuwa ni waumini wa Kiislamu. “Ila kwa kuona, muungwana ishalaa inamuonyesha kuwa kuna baibui, kanzu na kofia (baraghashia) inaonekana kuna Waislamu na wasio Waislamu.”



Akiendelea kutoa ushahidi wake, Kadhi huyo aliiambia mahakama ; “Nathibitisha kuwa Kampuni ya Agritanza Ltd inamiliki lile eneo kwa Uhalali na kwamba haikupita uchochoroni ikaruka ukuta ikaingia ndani ya hilo eneo, ilifuata utaratibu na kupokea hati zote na haki yake,” alisema Habibu.



Alifafanua kuwa Baraza la Maulamaa ni chombo kinachotoa uamuzi ya mwisho na kutoa miongozo mbalimbali kwa Waislamu na kwamba Bakwata inawakilisha Waislamu wote Tanzania.



Alidai kuwa Baraza hilo la Maulamaa linaundwa na wajumbe 10 kutoka mikoa mbalimbali na kwamba mjumbe huteuliwa kutokana na kuwa na kiwango cha elimu kilichopevuka na uadilifu.



“Baraza hili linamiliki mali zinazohamishika na zisizohamishika na sisi ndiyo tunachukua uhimizwaji wa kuulizwa na kudodoswa kila kilichopo ndani ya Bakwata kwa kuwa ni lazima tuhusishwe hususan katika masuala ya elimu,” alisema Habibu.



Kwa mujibu wa maelezo ya Katiba, vikao hufanyika mara mbili kwa mwaka chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa pamoja na vikao vya dharura. “ Januari 3, 2011, tulifanya kikao cha kawaida ambacho kilikuwa na agenda tatu ikiwemo ya umuhimu wa kujenga chuo Kikuu cha Kiislamu ambapo wajumbe walipendekeza kijengwe katika maeneo ya Dodoma, Tanga ama Chang’ombe.”

Baada ya kutolewa kwa ushahidi huo, mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Agritanza Ltd, Seleman Mohamed (48) akitoa ushahidi wake aliiambia mahakama hiyo kuwa yeye ni mfanyabiashara na kwamba ni kweli wao waliingia mkataba na Bakwata wa kubadilishana ardhi ekari nne kwa ekari 40.


Kesi itakuja kwa ajili ya kutajwa Desemba 18, mwaka huu na itaendelea kusikilizwa Desemba 31, mwaka huu.



Ponda, Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shekhe Mukadam Abdallah Swalehe (45) na wafuasi wao wanakabiliwa na mashtaka matano yakiwemo ya uchochezi, kula njama na wizi wa mali yenye thamani ya Sh59.6 milioni.



Katika shtaka la uchochezi, Shekhe Ponda na Shekhe Mukadam wanadaiwa kuwa kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka huu katika eneo la Chang’ombe Malkazi,akiwa kama Kiongozi wa Baraza na Jumuiya ya Kiislamu Tanzania aliwashawishi wafuasi wake kutenda makosa hayo





“Kutokana na mapendekezo hayo, tuliafikiana kijengwe Chang’ombe lakini ikaonekana kuwa Chuo Kikuu cha Kiislamu kinahitaji sehemu kubwa na pale kuna Ekari 4 hapatoshi,” alisema shahidi huyo wa pili wa upande wa mashtaka.



Hivyo walimtaka Katibu Mkuu wa Baraza la Maulamaa na timu yake wafanye mchakato wa kutafuta eneo maalumu kubwa ambalo wataweza kujenga chuo hicho Kikuu cha Kiislamu na kwamba baada ya siku nne au tano walipigiwa simu na kuwa wanahitajiwa Makao Makuu (Bakwata).

Shahidi huyo alidai kuwa walipofika waliambiwa kuwa kuna kikao cha dharura na kupatiwa taarifa na Katibu Mkuu wao juu ya mchakato huo wa kutafuta eneo kuwa kampuni ya Agritanza Ltd ilijitokeza na kutaka tuwape zile ekari nne na wao watupe ekari 40 huko Kisarawe Pwani.



“Sisi tuliona ekari 40 kwa ekari 4 ni kama ardhi na mbingu na Mungu alisikia kilio chetu akawaleta hao na tukaona kabla ya mazungumzo twende tukaone, tulipofika Manshalaa eneo lilikuwa sehemu nzuri, linapendeza, linavutia na mimi nilikuwa wa kwanza kuwashawishi wenzangu tukubaliane na mabadilishano na mchakato ukafanyika,” aliongeza shahidi huyo mahakamani hapo.



Hivyo Baraza la Maulamaa liliridhia kutoa maamuzi kwa Baraza la Wadhamini kufanyika kwa mchakato na makubaliano wa maeneo hayo.


Mimi ndipo wanaponifurahisha CCM. TEC inawacha iwatumikie wakiristo. BAKWATA inawataka iwahujumu waislam. BAKWATA inawakilisha waislam wote wa tz huku serekali ikisema haina dini. Sijui hapa ccm inataka itwambie nini waislam
 
Mwalimu Nyerere alipounda BAKWATA hakuwa mjinga. aliamini hili dudu litawatafuna Milele waislam.
 
Issue hapa sio uislam issue ni ponda kwani hata viongozi wa waislam aliWatishia maisha
 
Issue hapa sio uislam issue ni ponda kwani hata viongozi wa waislam aliWatishia maisha
MWALIMU NYERERE ALIPOIVUNJA EAMWS na kuwaundia BAKWATA usidhani hakujua anachofanya. hapa ilikuwa ni sawa na CCM kuwavuruga wapinazani ili ccm iwe na nguvu. Kuundwa kwa bakwata ni kuupa nguvu ukiristo hapa nchini
 
mwandishi mwenyewe kwanza muongo....hata hakimu anayesikiliza kesi siye aliyetajwa hapo lakini pia hizo tarehe sijui kazitoa wapi...tuna tatizo sana na waandishi hawako makini na issue za mahakamani
 
Mkuu lengu kuu ilikuwa ni kujenga Chuo kikuu,lakini uwezi kujenga chuo kikuu ndani ya heka 4,nadhani balaza la maulamaa ni makini sana ndiyo maana likaona ni vema chuo kikuu kijengwe kisarawe ambapo kuna heka 40!!
sawa mkuu ekari 40 ya kisarawe ni kubwa lakini huwezi toa ekari 4 ya chang'ombe yenye thamani zaid ya 400m..bakwata ni taasisi kubwa haiwezi kosa hela ya kununua hizo ekari 400 za kisarawe ambazo thaman yake haizid hata 50m..haiitaj hta diploma kujua kitu kama hcho
 
sawa mkuu ekari 40 ya kisarawe ni kubwa lakini huwezi toa ekari 4 ya chang'ombe yenye thamani zaid ya 400m..bakwata ni taasisi kubwa haiwezi kosa hela ya kununua hizo ekari 400 za kisarawe ambazo thaman yake haizid hata 50m..haiitaj hta diploma kujua kitu kama hcho
kwa hiyo unazarau uamuzi wa baraza la maulamaa ambao ni wawakilishi halali wa waislamu?
 
Back
Top Bottom