KADCO yamwaga mamilioni gawio la serikali

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,799
21,370
Kampuni ya uendelezaji na uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KADCO) imetoa gawio la Sh2.9 bilioni kwa Serikali kwa mwaka 2016 hadi 2019.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 11, 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Christine Mwakatobe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa bajeti na mwelekeo wa Kampuni hiyo kwa mwaka wa Fedha 2022/23.

Christine amesema mchanganuo wa gawio hilo ni kwa mwaka 2016/17 Kampuni ilitoa zaidi ya Sh555 milioni, mwaka 2017/18 ilitoa zaidi ya Sh583 milioni, mwaka 2018/19 ilitoa Sh1 bilioni na mwaka 2019/20 ilitoa Sh850 milioni.

Aidha amesema sambamba na gawio hilo Kampuni hiyo imelipa kodi ya Sh6.1 bilioni katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2020.

"Kiasi hicho kimelipwa kama kodi kwa Serikali kuu lakini kuna Sh541 milioni ambayo imelipwa kama kodi kwa Mamlaka ya Serikali za mitaa na Halmashauri ambapo kiwanja chetu kinapatikana," amesema.

Akizungumzia kuhusu mkakati wa Kampuni hiyo amesema ni kuongeza idadi ya abiria na kukarabati eneo la uwanja ili kuchukua magari 200 kutoka magari 83 yanayoweza kuchukuliwa kwa sasa kwenye uwanja huo.

“Mpaka sasa mkataba wa ukarabati wa ujenzi huu umeshasainiwa na hivi karibuni ujenzi utaanza na utagharimu Sh2.7 bilioni”amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Christine amesema mchanganuo wa gawio hilo ni kwa mwaka 2016/17 Kampuni ilitoa zaidi ya Sh555 milioni, mwaka 2017/18 ilitoa zaidi ya Sh583 milioni, mwaka 2018/19 ilitoa Sh1 bilioni na mwaka 2019/20 ilitoa Sh850 milioni.

Je gawio la mwaka 2020/21 na 2021/2022 liko wapi awamu ya serikali ya 6?
Hali Sio shwari , kuna hotel inajengwa mafichoni kule karibu na uwanja wa ajili golf maji ya chai yenye ghorofa 40 Riziwani unaifahamu au ni Mali ya KIA?
 
Umefungua nyuzi nyingi zenye shutuma za rejareja zisizo na proof.

We kama una umaskini wako na unaridhika kuna wenzako wana hela na wanakesha kutafuta namna ya kuziongeza
 
Huyu jamaa atakufa na umaskini na wivu umejaa mno!!

Hotel ikijengwa si inaleta manufaa kwa nchi? Watu hawatapata ajira humo? Serikali haitapata kodi?

Wakienda kujenga nje ya nchi si ndo hela itatoweka kabisa!!? Lipo bora wainvest ndani ya nchi au nje ya nchi?
 
Back
Top Bottom