Mzungu aliyekuwepo wakati wa ununuzi wa kampuni hiyo hajaonekana tena nchini hapa, na ali'pave tu njia ya mafisadi wa hapa kuendesha kiwanja hicho kwa kujitwalia mahela kutokana na rasilimali za watanzania!
Naambiwa mkataba alioingia na serikali ulikuwa unamfanya ailipe serikali milioni 1 kwa mwaka,(is this my ass?).....
Hii mikataba ya siri hii inatumaliza jamani, shitukeni!
Niipongeze sana serikali kwa hatua nzuri ya kipekee ya hatimaye kuutwaa uwanja huu uliojengwa kwa fedha za wananchi.
Kiwanja hiki kilijengwa na wasomi wanataaluma wazuri sana wa wakati wake, maana waliweza kukiwekea miundombinu ya ukakika sana.
Runway yake ni 5km, ambapo ni viwanja vichache kabisa Eastern and Central Africa vina urefu huu!.Pia 'hangar' yake ni kubwa sana in comparison to most southern African Countries.
Lakini kubwa kuliko yote, wajenzi walipiga hesabu nzuri sana ya growth-rate ya population, maana hadi leo(over 30yrs) bado kipo mbali sana na makazi ya watu.
Mungu Ibariki Tanzania!