Aliyekuwa makamu mkuu wa chuo cha saut padri Kitima,hii leo anaagwa rasmi kwa misa takatifu,na kumkaribisha mrithi wake padri Mgeni,ambae atazika kabisa mambo ya siasa na itikadi katika chuo hicho.
Wakati wa utumishi wake Kitima amekuwa akiikosoa serikali katika udhaifu wake hasa katika kutatua matatizo ya Watanzania wengi.
Kitima pia atakumbukwa kwa mahubiri yake ambayo kila mara yaliikosoa serikali,na jambo hili liliwafanya vijana wengi chuoni hapa hasa wale mashabiki wa CHADEMA kumshangilia kila mara alipoikosoa serikali.
Je!kuondoka kwake ndio mwisho wa CDM chuoni hapo?na je mrithi wake nae atakuwa ktk mlengo huohuo wa kichadema?hatujui,ila muda utasema.
Kitima ni kiongozi wa mfano.
1. Alifanikiwa kuendesha chuo kwa ada ndogo kuliko vyuo vikuu vyote (vikiwemo vya serikali) huku akilipa mishahara mikubwa kuliko vyuo vyote. Ikumbukwe kuwa kwa vyuo vya serikali ada za wanafunzi hazitumiki kulipa mishahara (mishahara hulipwa toka Hazina), wala hazitumiki kukarabati na kujenga majengo. Kitima ameweza kutumia ada za wanafunzi hizo hizo kuendesha chuo, kulipa mishahara, kukarabati na kujenga (40% kwa kuongezea misaada).
2. Kitima hakuwa na makuu, na hakutumia mali za chuo ovyo. Tangu amekuwa VC amekuwa anatumia gari yake mwenyewe. Alianza na Toyota Hilux Surf. Anapewa na chuo lita 50 za dizeli kwa wiki na zinamtosha kwa matumizi ya gari la VC. Simu pia ana fungu maalum na hazidishi, zinazozidi anatumia mshahara wake.
3. Kitima amekuwa mtetezi sana wa wanafunzi wa vyuo vikuu vyote tu Tanzania hasa kwa mambo ya mikopo. Wanaojua hili watamkumbuka sana bila kujali walisoma chuo gani. Kauli nyingi kali dhidi ya serikali amezitoa akitetea watoto wa maskini.
4. Kitima ana msimamo na hayumbishwi hata na Rais. Wakati wa uchaguzi mwaka 2010 Rais alitoa amri kwa vyuo vikuu kutofungua kabla ya uchaguzi. Iwapo Kitima angetii, chuo chake kingepata hasara ya zaidi ya TSh. Billioni mbili kwa kulipa gharama bila ku operate. Kitima aliamua kufungua tu chuo na akaokoa hizo Billioni mbili za chuo.
na mengine mengi....
Nina mashaka na uwezo wako wa kung'amua mambo,sina shaka kuwa wewe ni juaji na ni type ya wezi ambao hawajapata nafasi ya kuiba sasa wanaitaka kwa nguvu zote hata kwa kumwaga damu,weka hoja hapa nini nikufafanulie,mtaji wa siasa ni maneno na facts,twende,cdm mmefanya nn hadi sasa kwa hivyo viti vichache tulivyowapa bungeni?
Unadhani wewe umekombolewa?bora mimi kuliko wewe unaewaza kwenda kugombea kwenu uibe hata kilichobaki kwa mgongo huu huu wa kuwasaidia wanyonge,tumeona wengi waliosema hivyo,Lissu,Wenje,Kiwia,Msigwa,n.k ambao hadi leo hakuna walichofanya zaidi ya kuwanunulia maskini viroba wakazomee ccm na kufanya fujo,so wewe ndo bado hujakombolewa,wezi nyie,mmetapeli M4C mnadhani hatuoni?mjinga wewe.
- Kwahiyo mtu yeyote
anayekosoa utendaji wa Serikali lazima awe mwanachama wa chama fulani
cha siasa particularly CHADEMA?
- Wananchi wasio na vyama hawana ruhusa ya kukosoa utendaji wa Serikali
na chama chako cha ccm?
- Huyo anayekuja ulishawahi kufanya naye kazi wapi hadi useme directly
kuwa "atazika kabisa mambo ya siasa na itikadi katika chuo hicho"?
- By the way, Dr. Kitima aliwahi kusema yeye ni kada wa CHADEMA?
Huu uzi wako naona umekaa kama yale mambo aliyokuwa akiyasema Mh.
Masaburi.
Habari ilitakiwa kuwa"
Makamu Mkuu wa chuo-SAUT amestaafu" lakini kwa kuwa siku hizi bila
kutaja CHADEMA baadhi yenu hamshindi wala kulala basi umeona ni vema
Rev.Dr.Charles Kitima umuite kada ya CHADEMA. Kumbuka makada
wapo CCM na siyo CHADEMA, najua viongozi wengi wa chama tawala
wanamchukia kwa kuwa anaikosoa serikali na kusimamia ukweli
anaoamini.Sijawahi kushuhudia makamu mkuu wa chuo chochote Tanzania
akiwatetea wananchi wake atokako lakini nimemshuhudia mara kadhaa makamu
mkuu wa chuo cha SAUT akiwatetea hadi walima alizeti wa Singida dhidi
ya sera mbovu za CCM zisizowainua wakulima.
Nimjuavyo Dr.Kitima ni mpenda mabadiliko, miaka ya nyuma
viongozi wa serikali za wanafunzi walikuwa mapandikizi wa CCM (Rejea
TAHLISO ya 2010 walipoungana na CCM TBC kupinga wanachuo kupiga kura
popote) lakini Dr.Kitima aliamuru chuo kifunguliwe mapema ili
waliojiandikisha chuoni wapige kura.Pia alishirikiana vizuri na SAUTSO
licha ya kuwa mikononi mwa Pro-CHADEMA.
mi nshamaliza kutoa ujumbe hayo mengine ni yenu,mara mwigulu,uzalendo,kuponda wala kusifia havinihusu,chadema ccm hawanihusu,ila mukusika mwenyewe alideclare kuwa chadema,sasa si kada huyo?au mlitaka niandikeje?baadhi ya wanachadema mnaamini ubishi ndio siasa hata kama ni wa kipumbavu,sioni cha kubishania hapa zaidi ya kumuombea afya njema jamaa aendelee kupiga kazi huko aendako,au hata awe mgombea binafsi maana kwanza ni padri,acheni ulimbukeni nyie chadema mliocomment hapa mnataka tuwaandikeje ndio muone kuwa hatuna bias?sabodo ni nani?sasa ikitokea tumuandike humu kada tutakosea nini?acheni ulimbukeni,siyo kila mtu anaponda kama mlivyo nyie wachache na wajinga!!!kweli jamaa alikuwa kada tena kwa mazuri,siyo kama baadhi yenu,na sisi wanachuo tunamtambua kama kada,sasa kama wewe unabisha tupe neno mbadala wa kada
je,cuf,wahariri na wabunge particularly wa ccm na watetezi wa haki za binadam nao ni wana m4c?
Hapa ndo tunakuja kuamini kuwa m4c ni chama makin,cha wanyonge,ukweli na uhakika tukiunge mkono vilivyo.
je,cuf,wahariri na wabunge particularly wa ccm na watetezi wa haki za binadam nao ni wana m4c?
Hapa ndo tunakuja kuamini kuwa m4c ni chama makin,cha wanyonge,ukweli na uhakika tukiunge mkono vilivyo.