mageuzi1992
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 2,502
- 257
Nukuu by Mwananchi.co.tz , Jumanne,Julai 30, 2013
Chama cha mapinduzi katika jiji la Mbeya kimepata pigo baada ya kada wao maarufu , David Mwankina (70) kukibwaga chama hicho na kujiunga na Chadema. Mzee huyo ambaye ni hakimu mstaafu alikabidhi rasmi kadi ya CCM kwa Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi (Sugu) Mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. Baada ya kukabidhiwa kadi ya Chadema Mzee huyo alizungumza na kusema '' uamuzi wa kuachana na siasa za CCM umetokana na kusoma alama za nyakati na kudai kwamba tayari CCM hakina mpango mzuri kwa Watanzania. Alisema baada ya kuona CCM imepoteza msingi alioacha baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere, ni bora akahamia upande wa pili wa Chadema ambacho kina Uzalendo.
ukitaka kujijua kama unalaana bila kuambiwa na mtu, ni unapo jikuta unakashfu watu waliyo kupita umri! au wewe ulizaliwa na vijana wenzako ? heshima kitu cha bureYAANI huyo kibabu bado ana ndoto tu za siasa? si bora aende shamba tu akajilimie kahawa? anajipa stress za ajabu
ukitaka kujijua kama unalaana bila kuambiwa na mtu, ni unapo jikuta unakashfu watu waliyo kupita umri! au wewe ulizaliwa na vijana wenzako ? heshima kitu cha bure
Duh! CHADEMA inajaa wanasheria sijui siku tutakayoanza kuwachukulia hatua za kisheria magamba wataponea wapi?
tatizo lugha ya hekima inamata! nan nanajua kabisa haujakosa akili kiasi cha kushindwa kugundua lugha haikuwa poa, lakini asante kwa kunielewa kwa kiasi fualani, i hope ur going to be a better man!wapi hapo nimemkashifu. nimempa ushauri wa bure tu.
Nukuu by Mwananchi.co.tz , Jumanne,Julai 30, 2013
Chama cha mapinduzi katika jiji la Mbeya kimepata pigo baada ya kada wao maarufu , David Mwankina (70) kukibwaga chama hicho na kujiunga na CHADEMA. Mzee huyo ambaye ni hakimu mstaafu alikabidhi rasmi kadi ya CCM kwa Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi (Sugu) Mwishoni mwa wiki jijini Mbeya. Baada ya kukabidhiwa kadi ya CHADEMA Mzee huyo alizungumza na kusema '' uamuzi wa kuachana na siasa za CCM umetokana na kusoma alama za nyakati na kudai kwamba tayari CCM hakina mpango mzuri kwa Watanzania. Alisema baada ya kuona CCM imepoteza msingi alioacha baba wa taifa hayati Mwalimu Nyerere, ni bora akahamia upande wa pili wa CHADEMA ambacho kina Uzalendo.