Kaburi la Kiyeyeu lang'oka!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kaburi la Kiyeyeu lang'oka!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Dec 31, 2010.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tumain Msowoya, Iringa
  HATIMAYE kaburi la kihistoria la Martine Kiyeyeu lililokuwa katika eneo la Isimila, kijiji cha Ugwachanya limeondolewa katika hifadhi ya barabara ya Tanzania-Zambia, Mkoani Iringa kwa ajili ya kupisha upanuzi wa barabara hiyo.

  Kaburi hilo ambalo lilikuwa pembezoni mwa barabara hiyo, limeondolewa katika oparesheni iliyoendeshwa na Wakala wa barabara (Tanroads) kwa akiwashirikisha wananchi wa kijiji hicho.

  Kaburi la Kiyeyeu linalokadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 40 hadi 50, lina historia ndefu kutokana majaribio ya kuliondoa mara kadhaa kushindikana.

  Moja ya maajabu ya kaburi hilo ni kushindwa kupitishwa kwa umeme kupita juu ya yake na pia linadaiwa kushindikana kuondolewa mara mbili na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyeuawa kwa nyuki na mwingine kufariki ghafla akiendesha tingatinga alipokuwa akijaribu kuling'oa.

  Lakini jana kaburi hilo na mengine 21 yaliyokuwa kwenye eneo hilo yaliondolewa na kuhamishiwa upande wa pili wa barabara, ambako kulikuwa na kaburi moja la mtoto wa kike wa Kiyeyeu, ambaye hakuzikwa katika eneo lililokuwa na makaburi ya ndugu zake.

  Wakizungumza na Mwananchi, baadhi ya watu walioshiriki katika zoezi la kuondoa kaburi hilo walisema kazi haikuwa ngumu kama walivyodhani.

  "Tumeondoa ‘kiulaini', hakuna mila wala desturi iliyofanywa kabla ya kuliondoa, na ndugu wa Kiyeyeu wanasema watakuja kazi ikimalizika kwa ajili ya kumaliza mila zao," alisema Gaitan Utenga.
  Alisema kazi hiyo imefanikiwa kutokana na ushirikiano walioupata kutoka Tanroads ambao waligharamia shughuli nzima ya kuondoa kaburi hilo ilyowashirikisha vijana zaidi ya 30.

  "Tumelipwa pesa yetu vizuri, wamenunua sanda na masanduku kwa ajili ya mazishi na hatimaye kaburi limeondolewa tofauti na imani iliyokuwa imezagaa miongoni mwa wengi kwamba ingeshindikana," alisema.
  Mwenyekiti wa kamati ya kuondoa kaburi hilo ambaye ni mmoja wa wanafamilia wa Kiyeyeu, Pulo Kikoti alisema hakuna tatizo lililotokea wakati wa kuondoa kaburi hilo. Kazi hiyo alizanza jana saa nne asubuhi na kumalizika majira ya jioni.

  Alisema ugumu ulikuwa katika kulibomoa kutokana na aina ya ujenzi wake, lakini baada ya kubomolewa kazi ya kulihamishia upande wa pili wa barabara haikuwa ngumu.
  Hata hivyo walisema tayari makaburi yote 22 yaliyokuwa katika eneo hilo yameondolewa na kwamba kazi ya kuzika mafuvu ya marehemu ambao wote ni familia ya Kiyeyeu inatarajiwa kumalizika leo mchana.

  "Ndugu wanasema mwishoni baada ya mazishi kukamilika na makaburi mapya kujengwa, watakuja kufanya mila zao, lakini mpaka sasa tumemaliza shughuli nzima ya kuondoa kwa kaburi hilo ambalo lilikuwa gumzo kwa miaka mingi," alisema.
  Mzee huyo alisema wengi waliamini kuwa eneo hilo lilikuwa la maajabu, kutokana na ukweli kwamba lilishawahi kujaribiwa kuondolewa zaidi ya mara mbili na ikashindikana.

  "Kulikuwa na imani nyingi hapa, lakini tulijitosa kuhamisha na kweli hakuna kilichotokea hapa, naweza kusema imani hizi hazikuwa za kweli, mbona tumefanikiwa?" alihoji Kikoti.

  Kuondolewa kwa kaburi la Kiyeyeu kumekuwa gumzo kwa watu wengi wakiwemo abiria wanaopita katika barabara hiyo ambapo kila mmoja amekuwa akishangaa jinsi kazi hiyo ilivyofanyika.

  Awali mkazi wa Mafinga, Sadick Mhomanzi alijitokeza akidai kuwa anaweza kuliondoa kaburi hilo la Kiyeyeu na kwamba hakuna madhara yoyote ambayo yangeweza kumpata.

  Hata hivyo mapema jana, Mhandisi aliyeshiriki operesheni ya kupitisha umeme kwenye kaburi hilo mwaka 2006, Eliasante Mwakalinga, alionya kuwa Sadick asithubutu kwani angeweza kupatwa na balaa.

  Akizungumza na gazeti hili kutoka mkoani Mtwara jana, Mwakalinga ambaye sasa ni mwalimu wa Chuo Cha Mafunzo Stadi Veta mkoani Mtwara, alisema maajabu yanayofanyika kwenye kaburi hilo, yanatisha na yanaweza kuwa hatari kwake.

  "Mimi sijui atatumia mbinu gani lakini lazima iwe ushirikina au nguvu za kiroho. Hata hivyo ni vema akatafakari kwa kina uamuzi huo kwani unaweza kumgharimu na akaongeza historia ya kaburi hilo kwamba sasa, wamekufa watu watatu badala ya wawili," alisema Mwakalinga.

  Alisema wakati wanatengeneza laini ya umeme eneo la kaburi hilo mwaka 2006, umeme uligoma kupita juu yake na wakalazimika kuhamisha njia ndipo walipofanikiwa.

  Mwakalinga alipendekeza serikali kulifanyia uchunguzi kaburi hilo na ikiwezekana litangazwe kivutio cha watalii kwani kuna mambo mengi ya ajabu mbali na watu wawili kufariki dunia walipokuwa wanajaribu kuliondoa.

  "Ukiwa huku Iringa utapata maelezo mengi kuhusu wazee wetu hawa, wengine walikuwa wanazikwa na vitu vyao, wengine walizikwa wakiwa wamekalishwa chini na hata baadhi yao walikuwa wanazikwa kwa kupakatwa na vijana wenye nguvu. Hayo yote ni historia yetu ambayo ni vyema tukaienzi,"alisema

  Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti maajabu ya kaburi hilo mkazi wa Mafinga, Sadick lijitokeza na kusema anaweza kuliondoa bila wasiwasi wala madhara yeyote tofauti na maelezo ya watu kwamba watu kadhaa wameshapoteza maisha kwa kujaribu kufanya hivyo.

  Mhomanzi alitoa kauli hiyo wakati ambapo taarifa za uhakika kutoka katika eneo la kijiji hicho zikidai juhudi za kuliondoa kaburi hilo ili kupitisha barabara eneo hilo zimekuwa zikishindikana hata pale ilipotumika familia ya Marehemu Martin Kiyeyeu mwenyewe.

  Lakini Mhomanzi kwa kujiamini alisema atakwenda yeye mwenyewe na kutumia jembe lake la mikono kuchimba na kuondoa udongo huo hadi mifupa ya marehemu Kiyeyeu na kuihamisha bila ya kudhurika.

  "Amini maneno yangu kuona kaburi linashindikana kuondolewa, hakuna mtu anayeweza kushindwa, kaka mimi niko tayari nitafanya kazi hiyo kwa mkono wangu kabisa,"alisema Mhomanzi.

  Mhomanzi alihoji "Kama ndugu wa marehemu wameridhia kuondolewa kwa kaburi hilo na kupatiwa eneo mbadala ni kitu gani kinaweza kuzuia? mimi siamini hivyo,Tanrods waniwezeshe mimi kuifanya kazi hiyo, nitakwenda na jembe langu pamoja na koleo kuifanya kazi hiyo nitakachokosa ni trekta la kubebea udongo na mifupa"alisema .

  Source: Mwananchi.

  Nadhani ile fitina kwamba watu watakufa sijui watu watapatwa na balaa mara sijui mizimu itakufata kwenye keyboard itakuwa imeisha maana hili kaburi lilikuwa ni tishio Iringa. Mie niliwahi kusema ni fikra na hisia za watu tu. Ukimuweka mungu mbele kanyaga twende basi it is all about having confidence in yourself.
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nina wasi wasi pale mahara ajari hazitakwisha bse huwa najiuliza kwa nini umeme ulipinindishwa tena hewani
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu ile ilikuwa imani tu mkuu jamaa zangu wa kihehe nawaelewa vitu kama hivi wanaviogopa sana. Sasa limeshatolewa tuachane na mambo haya tujenge taifa.
   
 4. B

  Baba Jose Senior Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya mambo yana ukweli,jiulize tu kwa nini umeme ulipindishwa,kilishofanyika ni wana ndugu wameridhia wamefanya tambiko na kumu omba mzee kiyeyu akubari ili barabara ipite kwa maendeleo ya taifa vinginevyo nakuambia kaburi lisingetoka
   
 5. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #5
  Jan 1, 2011
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,446
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  je wanataka kutuambia kuwa yale matambiko yaliyokuwa yanafanyika ilikuwa ni kiini macho? maana kwa wale wasafili nafikiri walikuwa wakiona wenyewe kiti na ngozi viliwekwa pale juu ya kaburi pamoja na pombe aina ya comoni kama ishala ya kumbembeleza akubali kuhama
   
 6. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tehe tehe.....hapo hao walioling'oa, wanalala roho juu juu kwa kihoro!
   
 7. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #7
  Jan 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Tujifunue kwenye blanketi la ujinga tulilojifunika jamani. Kuhusu umeme kupindishwa tulishajadili hapa na sababu iliyotolewa... sio ushirikina. Kama sisi tunaojua kutumia computer tunakuwa na imani mbovu kama hizi ... je huko vijijini si ndio balaa? Nani atamwokoa mwingine?
   
 8. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #8
  Jan 1, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Hivi huyo Kiyeyeu mwenyewe ana historia gani na amefanya nini kikubwa wakati wa uhai wake? Naomba kuelimishwa
   
 9. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2014
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  [h=2]Kaburi la Kiyeyeu lang'oka[/h] Friday, 31 December 2010
  HATIMAYE kaburi la kihistoria la Martine Kiyeyeu lililokuwa katika eneo la Isimila, kijiji cha Ugwachanya limeondolewa katika hifadhi ya barabara ya Tanzania-Zambia, Mkoani Iringa kwa ajili ya kupisha upanuzi wa barabara hiyo. Kaburi hilo ambalo lilikuwa pembezoni mwa barabara hiyo, limeondolewa katika oparesheni iliyoendeshwa na Wakala wa barabara (Tanroads) kwa akiwashirikisha wananchi wa kijiji hicho. Kaburi la Kiyeyeu linalokadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 40 hadi 50, lina historia ndefu kutokana majaribio ya kuliondoa mara kadhaa kushindikana. Moja ya maajabu ya kaburi hilo ni kushindwa kupitishwa kwa umeme kupita juu ya yake na pia linadaiwa kushindikana kuondolewa mara mbili na kusababisha vifo vya watu wawili akiwemo aliyeuawa kwa nyuki na mwingine kufariki ghafla akiendesha tingatinga alipokuwa akijaribu kuling'oa. Lakini jana kaburi hilo na mengine 21 yaliyokuwa kwenye eneo hilo yaliondolewa na kuhamishiwa upande wa pili wa barabara, ambako kulikuwa na kaburi moja la mtoto wa kike wa Kiyeyeu, ambaye hakuzikwa katika eneo lililokuwa na makaburi ya ndugu zake. Wakizungumza na Mwananchi, baadhi ya watu walioshiriki katika zoezi la kuondoa kaburi hilo walisema kazi haikuwa ngumu kama walivyodhani. "Tumeondoa ‘kiulaini', hakuna mila wala desturi iliyofanywa kabla ya kuliondoa, na ndugu wa Kiyeyeu wanasema watakuja kazi ikimalizika kwa ajili ya kumaliza mila zao," alisema Gaitan Utenga. Alisema kazi hiyo imefanikiwa kutokana na ushirikiano walioupata kutoka Tanroads ambao waligharamia shughuli nzima ya kuondoa kaburi hilo ilyowashirikisha vijana zaidi ya 30. "Tumelipwa pesa yetu vizuri, wamenunua sanda na masanduku kwa ajili ya mazishi na hatimaye kaburi limeondolewa tofauti na imani iliyokuwa imezagaa miongoni mwa wengi kwamba ingeshindikana," alisema. Mwenyekiti wa kamati ya kuondoa kaburi hilo ambaye ni mmoja wa wanafamilia wa Kiyeyeu, Pulo Kikoti alisema hakuna tatizo lililotokea wakati wa kuondoa kaburi hilo. Kazi hiyo alizanza jana saa nne asubuhi na kumalizika majira ya jioni. Alisema ugumu ulikuwa katika kulibomoa kutokana na aina ya ujenzi wake, lakini baada ya kubomolewa kazi ya kulihamishia upande wa pili wa barabara haikuwa ngumu. Hata hivyo walisema tayari makaburi yote 22 yaliyokuwa katika eneo hilo yameondolewa na kwamba kazi ya kuzika mafuvu ya marehemu ambao wote ni familia ya Kiyeyeu inatarajiwa kumalizika leo mchana. "Ndugu wanasema mwishoni baada ya mazishi kukamilika na makaburi mapya kujengwa, watakuja kufanya mila zao, lakini mpaka sasa tumemaliza shughuli nzima ya kuondoa kwa kaburi hilo ambalo lilikuwa gumzo kwa miaka mingi," alisema. Mzee huyo alisema wengi waliamini kuwa eneo hilo lilikuwa la maajabu, kutokana na ukweli kwamba lilishawahi kujaribiwa kuondolewa zaidi ya mara mbili na ikashindikana. "Kulikuwa na imani nyingi hapa, lakini tulijitosa kuhamisha na kweli hakuna kilichotokea hapa, naweza kusema imani hizi hazikuwa za kweli, mbona tumefanikiwa?" alihoji Kikoti. Kuondolewa kwa kaburi la Kiyeyeu kumekuwa gumzo kwa watu wengi wakiwemo abiria wanaopita katika barabara hiyo ambapo kila mmoja amekuwa akishangaa jinsi kazi hiyo ilivyofanyika. Awali mkazi wa Mafinga, Sadick Mhomanzi alijitokeza akidai kuwa anaweza kuliondoa kaburi hilo la Kiyeyeu na kwamba hakuna madhara yoyote ambayo yangeweza kumpata. Hata hivyo mapema jana, Mhandisi aliyeshiriki operesheni ya kupitisha umeme kwenye kaburi hilo mwaka 2006, Eliasante Mwakalinga, alionya kuwa Sadick asithubutu kwani angeweza kupatwa na balaa. Akizungumza na gazeti hili kutoka mkoani Mtwara jana, Mwakalinga ambaye sasa ni mwalimu wa Chuo Cha Mafunzo Stadi Veta mkoani Mtwara, alisema maajabu yanayofanyika kwenye kaburi hilo, yanatisha na yanaweza kuwa hatari kwake."Mimi sijui atatumia mbinu gani lakini lazima iwe ushirikina au nguvu za kiroho. Hata hivyo ni vema akatafakari kwa kina uamuzi huo kwani unaweza kumgharimu na akaongeza historia ya kaburi hilo kwamba sasa, wamekufa watu watatu badala ya wawili," alisema Mwakalinga. Alisema wakati wanatengeneza laini ya umeme eneo la kaburi hilo mwaka 2006, umeme uligoma kupita juu yake na wakalazimika kuhamisha njia ndipo walipofanikiwa. Mwakalinga alipendekeza serikali kulifanyia uchunguzi kaburi hilo na ikiwezekana litangazwe kivutio cha watalii kwani kuna mambo mengi ya ajabu mbali na watu wawili kufariki dunia walipokuwa wanajaribu kuliondoa. "Ukiwa huku Iringa utapata maelezo mengi kuhusu wazee wetu hawa, wengine walikuwa wanazikwa na vitu vyao, wengine walizikwa wakiwa wamekalishwa chini na hata baadhi yao walikuwa wanazikwa kwa kupakatwa na vijana wenye nguvu. Hayo yote ni historia yetu ambayo ni vyema tukaienzi,"alisema Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti maajabu ya kaburi hilo mkazi wa Mafinga, Sadick lijitokeza na kusema anaweza kuliondoa bila wasiwasi wala madhara yeyote tofauti na maelezo ya watu kwamba watu kadhaa wameshapoteza maisha kwa kujaribu kufanya hivyo. Mhomanzi alitoa kauli hiyo wakati ambapo taarifa za uhakika kutoka katika eneo la kijiji hicho zikidai juhudi za kuliondoa kaburi hilo ili kupitisha barabara eneo hilo zimekuwa zikishindikana hata pale ilipotumika familia ya Marehemu Martin Kiyeyeu mwenyewe. Lakini Mhomanzi kwa kujiamini alisema atakwenda yeye mwenyewe na kutumia jembe lake la mikono kuchimba na kuondoa udongo huo hadi mifupa ya marehemu Kiyeyeu na kuihamisha bila ya kudhurika. "Amini maneno yangu kuona kaburi linashindikana kuondolewa, hakuna mtu anayeweza kushindwa, kaka mimi niko tayari nitafanya kazi hiyo kwa mkono wangu kabisa,"alisema Mhomanzi. Mhomanzi alihoji "Kama ndugu wa marehemu wameridhia kuondolewa kwa kaburi hilo na kupatiwa eneo mbadala ni kitu gani kinaweza kuzuia? mimi siamini hivyo,Tanrods waniwezeshe mimi kuifanya kazi hiyo, nitakwenda na jembe langu pamoja na koleo kuifanya kazi hiyo nitakachokosa ni trekta la kubebea udongo na mifupa"alisema .Tumain Mso
   
Loading...