Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,836
- 730,284
Kuzimu kunaposhiba vifo hupungua duniani, kuzimu kunapohitaji shibe majanga yenye kuangamiza roho nyingi kwa mpigo hutokea, majanga hayo yanaweza kuwa ya kiasili au ya kutengenezwa na mwanadamu
Makaburi ni midomo ya kuzimu, kuchimba kaburi ni sawa na kufunua mdomo kwa ajili ya kuulisha. Mdomo ni njia ya kuelekea tumboni, na kaburi ni njia ya kuelekea kuzimu
Mauaji ya kishirikina huhusisha na kuchimba kaburi la mfano
Iko hivi;
Mchawi anapopata oda ya kuua , pamoja na mambo mengine hukuagiza ulete chochote cha unayekusudia kumuondoa duniani hata mate yake tu yanatosha,
Kisha humchukua mnyama yeyote mara nyingi paka au kuku huyu huuliwa na kutolewa kila kitu tumboni kishapo tumbo hujazwa madawa nuizi la kifo cha mhusika, kitu chake chochote hata jina lililoandikwa kwa damu ndulele nk
Mzoga ule hufungwa na kwenda kuzikwa usiku kwenye saa tano na kufukuliwa saa sita usiku kisha lile kaburi dogo la paka huachwa wazi
Maana yake ni nini?
Ulishalilisha kaburi lakini ukalipokonya chakula chake na hukulifukia hivyo litadai chakula chake(maiti)na kwakuwa kilichozikwa pale ni mzoga wa paka lakini nuizi la kifo ni la fulani pamoja na madawa husika hivyo kaburi litadai roho hiyo
Mganga atakuelekeza vile vitu uvitoe tumboni mwa mzoga wa paka na kwenda kuvitupa ambapo mhusika atapita au njiapanda na kuutelekeza ule mzoga bila kuuzika
Hapo tayari utakuwa roho ya kifo kwa mtu wako na akikatiza tu amekwisha...hapa utakuwa umelipa kisasi lakini roho yake marehemu haitakuacha kamwe , usijifariji kuwa mganga atadhurika, never yeye ni mjanja sana!kuepuka kisasi cha damu ya marehemu atakwambia kila kitu ufanye wewe...
Una mpango wa kumtoa mtu roho!?tafakari mara mbili kwakuwa hutabaki salama maisha yako yote