Kabla ya DOT COM

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,037
Reaction score
168,678
Kulikuwa na Chama kimoja, chama kushika hatamu
Kulikuwa na SHIHATA Shirika la Habari Tz
Kulikuwa hamna magazezi ya UDAKU.
Chakubanga alikuwa bonge ya staa
Nipashe ndio ilikuwa sehemu pekee ya kuchekesha kwenye gazeti la MFANYAKAZI
Redio Tanzania ndio ulikuwa mpango mzima, hakukuwa na FM
Motomoto lilikuwa ndio gazeti la kwanza la binafsi
Tulitii bendera, hata ya CCM ikishushwa au kupandishwa lazima usimame
Redio ilikuwa mwisho saa sita
Hakukuwa na Tv stesheni
Mama na mwana ilikuwa na wasikilaji kibao, hata wazee
Kulikuwa na somo la Siasa na KIlimo pia Sayansi Kimu
Juma na Roza walifahamika nchi nzima
Shule maarufu ilikuwa Mtakuja Primary School
Ukiwa na kitabu cha Willie Gamba wee ni noma
Lyrics tuliandika kwenye madaftari
Hakukuwa na CD, kanda ndio ulikuwa mpango mzima


Hebu ongezeeni tuwape shule watoto wetu wa dot com
 
hahahahaaaa umenikumbusha mbaaaali enzi za mama na mwana,,,,,,,,,,,,,na Debora Mwenda yuleee sijui
Umesahau Chei Chei shangazi,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
darasani kulikuwa na somo la uraia ambapo tulisoma kitabu kimeandikwa chama na serikali
 
somo la siasa ndio likikuwa tamu zaidi likifuatiwa na sayansi kimu na kilimo...
 
Mliokuwa na redio mlifaidi kweli,hembu leteni stori zaidi.
 

Shuleni Tulifurahia story za heri Mimi sijasema, mandawa na manenge, sizitaki nbichi hizi, Mr all of you
 
Kipindi cha fujo fujo pekee kilikuwa Club raha leo show.
 
Ninadaftari langu la lyrics hadi leo, umenikumbusha kitambo sana
 
Kulikuwa na star mmoja anaitwa mayuku
 
Tukifunga shule tunakutana stendi moshi town mjanja anakaa kwa shoe shine
 
Nimekumbuka kipinda cha "Hisia na Muziki!" Mtangazaji ni Angalieni Mpendu. Hadi leo napenda muziki wa nyumbani!
 
mi nimemfaidi ezekiel malongo enzi anatangaza mpira...

enzi za utangazaji wake,
kulikuwa na mchezaji mmoja wa kongo alikuwa anaitwa mbo mpenza!

basi jamaa alikuwa akitangaza akifikia kwenye mbo mpenza, hataji full name qulaleki.. ananishia kusema mpenza! mpenza!

aisee i loved ezekiel malongo soo much during my child hood!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…