Poa 2
JF-Expert Member
- Jul 7, 2019
- 1,294
- 1,288
Hodi jukwaani.
Nchi yetu imepitishwa katika Giza nene miaka 6 iliyopita, roho ya mauaji, mateso kutekana, kusingiziana mikesi ya hovyo, visasi, chuki na fitina ilitanda katika anga letu.
Mzaliwa wetu wa Kwanza wa awamu ya tano mwenda zake alipitisha roho ya mauti, maovu unafiki usio na kikomo na baadhi yetu walivamiwa na roho hii kiasi kwamba lilitaka kuwa Jambo la kawaida kufanya haya.
Sasa roho hii bado ipo mioyoni mwa wafuasi wake na inatenda kazi, mauaji ya kikatili yanaendelea japo si ya kisiasa, kukamatana hovyo bado kunaendelezwa na jeshi letu la polisi, kutukanana bado kunaendelea mitandaoni.
Kama tunakubali kuridhiana na kuanza upya basi Kuna haja ya kuwa na maombi ya kitaifa ili watu kujutia, kutubu na kutokomeza hii roho ya uasi iliyoanza kustawi nchini kwetu.
Sasa swali ni tufanye maombi haya kabla au baada ya maridhiano?
Mama Samia hatua unazochukua ni sahihi endelea kuupiga mwingi kuelekea upande huo kaza buti usiyumbe Wala kuyumbishwa watanzania tuko nyuma yako utashinda, utashinda na utashinda
Nawasilisha hoja