Kabila na Kagame Yao Yawaendea Bukheeri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kabila na Kagame Yao Yawaendea Bukheeri!

Discussion in 'International Forum' started by Junius, Aug 7, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  [​IMG][​IMG]
  Kagame na Kabila wakikenua

  Viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo walifanya mkutano wa kipekee hapo Alhamis ambapo waliafikiana kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na katika maswala ya usalama.
  Mazungumzo kati ya Rais Paul Kagame na mwenzake, Joseph Kabila yalifanyika katika mji wa Goma.
  "Ni hatua kubwa ya kwanza," Rais Kabila aliwaambia waandishi wa habari baada ya mkutano huo.
  Kwa upande wake, Rais Kagame alimhakikishia mwenzake kwamba Rwanda haitokubali kutumiwa kama ngome ya waasi dhidi ya serikali ya DRC.
  Rasilmali na usalama
  Viongozi hao walikubaliana kwamba nchi zao zitashirikiana katika kubuni miradi ya kuchimba rasilmali ya gesi kwenye ziwa Kivu na pia kufufua tume za pamoja.
  [​IMG][​IMG]
  Rwanda bado inamshikilia Nkunda
  Mwezi mmoja umepita tangu Rais Kagame na Rais Kabila kuteua mabalozi kwa nchi hizo mbili, ishara kwamba uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaimarika.
  Mnamo mwezi wa Januari, nchi hizo mbili zilikubaliana kuendesha harakati za pamoja za kuwaangamisa waasi wa Hutu FDLR ambao wamejenga ngome yao nchini DRD.
  Baadhi ya wapiganaji wa FDLR wanashutumiwa kwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 kabla ya kutorokea DRC.
  Laurent Nkunda
  Hali kadhalika, Rwanda imemkamata kiongozi wa kundi la waasi wa kabila la Watutsi nchini DRC, Laurent Nkunda.
  Nkunda bado anashikiliwa na Rwanda licha ya ombi la DRC la kumtaka arudishwe nchini humo ili kufunguliwa mashtaka.
  Hata hivyo, Rais Kagame alimhakikishia mwenzake, "ninaahidi kwamba Laurent Nkunda na kundi la CNDP hawatoruhusiwa kuendesha harakati zao za kuitatiza DRC wakiwa nchini Rwanda."
  Viongozi hao wawili wanatazamiwa kukutana tena mnamo mwezi wa Oktoba au Novemba jijini Kinshasa.

  SOURCE:BBC SWAHILI SERVICE
   
 2. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Tafadhali Paul mpeleke Nkunda Congo akajitetee mwenyewe kila mtu anatambua mauaji na uharamia mwingine alioufanya! au unataka kumtumia kama bargaining chip?? kulikoni? haya ndio mambo ya viongozi wa kiafrika kutotaka kukamatwa. Tunajua na wewe pia unatakiwa pamoja na Bashir na sasa hutaki kumpeleka Nkunda Congo??
   
Loading...