martin martines
Member
- Apr 23, 2016
- 43
- 21
Habari zenu,
Watu wa MUNGU mimi ni mwalimu wa secondary, nina mke ila hatujafanikiwa kupata mtoto, pia nina fanya masters evening session katika field nyingine na sio education, lengo niondoke kwenye area hii ya ufundishaji yenye malipo kidogo.
Kwenye hii shule ninayofanyia kazi kuna mtoto wa mwenye shule nina uhusiano nae wa kimapenzi kwa mwaka wa pili mfululizo sasa, baba yao amewaweka hapa wasimamie shule ingawa ana kazi nyingine, maana ni shule nyingi, group of school.
Hivi karibuni mke wangu alinasa mawasiliano yangu na huyo dada, akachukua namba na kwenda kumpigia huyo rafiki yangu wa shuleni, akamtukana matusi na wakajibizana sana, mke wangu alivyonibana nikakiri kosa, akaamua kurudi kwao, ni hapa hapa Dar.
Kutokana na kukasirishwa na matusi ya mke wangu, rafiki yangu amefura ile mbaya, ameenda kwenye stationary yangu amebeba photocopier machine, printer na desktops nne zilizokua zinatumika kwa wateja wa Internet hapo stationary, ambayo sehemu kubwa ya mtaji alinipa yeye na alininunulia yeye hivyo vitu, kachukua simu aliyoninulia na vingine vingi.
Anadai kama nataka kuendelea nae niachane na mke wangu tuoane nae, anadai alininunulia vitu hivi akijua tutakua mke na mume, anyway nimekua nikimkubalia hayo madai yake ya kumuacha wife lakini huwa sitekelezi, baada ya ugomvi huu na baada ya kuchukua vitu amedai hilo ndio sharti lake kuu ili arudi she vitu na ili tuendelee, kwamba yeye amechoka kuwa spare tyre, ingawa tangu anaomba kuwa na mimi nilimwambia kuwa nina mke.
Wadau, sijui nifanyeje maana nilikuwa bado namtegemea sana huyu dada, Masters amekuwa akinifadhili yeye, hadi sasa, nyumba yangu kwa kiasi kikubwa ni msaada wake, ingawa na mimi nilichukua mkopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ila kwenye finishing amenisaidia sana, yote tisa, kumi biashara yangu ya stationary bila yeye isingekuwepo, mshahara wangu kwa kiasi kikubwa unapumua, hivyo nawasaidia na wazazi.
Kutegemeana na sakata hili litakavyoisha, nina wasi wasi sana na kibarua changu, maana ninafanya kazi kwenye shule yao, yeye anafanya kazi kwenye shirika kubwa lakini karibu kila siku akitoka huko huja kusimamia shule.
Nisaidieni mawazo, wife amekua mbogo, hataki kusikia lolote, hadi sasa amegoma kurudi akidai nimuhakikishie kama nimeachana na yule mwanamke.Sasa sijui mlikua mnasemaje, niache kumbembeleza badala yake niishi na huyu rafiki yangu?
Mimi ni mtu wa MUNGU ni msabato kabisa, sikupenda kufanya haya sijui nimefika fikaje huku na sijui kama kanisa litanielewa.
Help please