Mleta mada uko sahihi 100%, mimi limenikuta baada ya kuishi maisha ya mwanzo kuwa na mwenza yule binti nilizaa nae ila kwa kweli tulipendana sana, ila mpaka leo sifahamu hasa kwa nini tuliachana, ila ndugu zake walichangia kiasi kikubwa utengano wetu, hasa ukizingatia ule umri tuliokua nao..,
Anyway, alikuja kuishi na jamaa mwingine ili anikomoe au aniumize roho, sijui.
Nafikiri ndio hiyo plan B, unayozungumzia.kwa kweli alianza kunifuatilia huku akiwa anaishi na jamaa mwingine, na wakikorofishana nasikia huwa anamwambia jamaa usinitishe wala kunibabaisha, baba watoto wangu yupo saa yoyote ninaweza kwenda na akanipokea.
Ila hata hivyo, daaaah..!! Ni kweli muda wowote nimwita anakuja kwa kasi ya dramliner..[emoji1787][emoji1787][emoji1787]