Kaa chonjo: Hapa pana matapeli

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Polisi jamii imezua jambo.Katika Daraja la Ubungo,Stendi ya kuelekea Mwenge,nyakati za usiku kuna matapeli.Hayo nimeyaona jana majira ya saa mbili usiku nilipokuwa nasubiri daladala kuelekea Mwenge.Matapeli hao hujifanya kuwa ni Polisi Jamii ambao wanakamata watu wanaokiuka sheria maeneo hayo.Watu ambao hujitenga pembeni kwa chini kuongea na simu au hata kusubiri gari lifike,huzongwa na watu hao wakimsingizia kuwa amejisaidia na hivyo amechafua mazingira.Kinachofuata ni mmoja wao kutoa kitambulisho(sijui halali au batili) na kutishia kumpeleka Ofisi ya Polisi Jamii Ubungo.Kutokana na wingi wao,inakuwa vigumu kwa mtu kubishana nao tena mkiwa gizani.Kidogodogo kinamtoka msingiziwa.Wanadai kuwa faini kwa kosa hilo ni 50000 au kifungo cha miezi sita.Watu wote niliowashuhudia wakikumbwa na kadhia hiyo jana waliishia kutoa 'rushwa' kwa 'Askari' hao.Wimbo wa zamani kidogo ulikuwa na maneno haya:'Bwana Mangushi nakupoa pole sana kwani hao ni walaghai.walaghai eee,wanaitwa matapeli oooooooooo,oooooooooooo wanaitwa tapeli............Kaa chonjo!!!
 
Ni kweli mkuu hata mimi pia yamenikuta wiki iliyopita nikalazimika kutoa 10,000/-kwa uwoga na wing wa wale vijana
ambao wachache kati yao wana vitambulisho.nikaona bora kutoa 10,000/-kuliko kama wangenipora simu zangu na waleti iliyokuwa na pesa.
 
Utapeli umechukua sura mpya na hata wezi nao wamebuni namna ya kufanikisha malengo yao kwa njia ya kistaarabu kabisa...juzi jamaa yangu mmoja karudishwa nyma sana kibiashara baada ya vijana hawa waliojiajiri wenyewe kwa shughuli za usiku kukata bati na kingia dukani kwa jamaa na kuchukua simu zote (jamaa alikua mfanya biashara wa simu)...km hiyo haitoshi wameambaa juu ya dari na kuingia kwenye duka lingine ndani ya jengo hilo hilo na kujicchukulia kiasi cha kikubwa cha fedha na vocha...poleni kwa mliokumbwa na maswahiba haya...
 
sasa watu wanakuwa wamejisaidia kweli? kama ni kweli kidogo itapunguza uchafu ulikithiri jijini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom