Azarel
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 29,020
- 40,848
Kabla ya kufariki kwake mwaka 2004, kuna huyu mama nilimtembelea kwake na hapohapo nilikuwa namfundisha binti mmoja Tuition nyumbani kwao. Ni huko Arusha, eneo la Jengo la Mollel karibu kabisa na Mianzini.
Wakati naingia getini kwake jioni nikaona ameshika chaki anaandika mlangoni kwake (mlango wa mbele kabisa) huku akiwa amepanda juu ya stuli wakati akiandika. Huyu mama si mshirikina kiasili na ni Mroman safi tunavyomjua.
Wakati akiendelea kuandika na kunikaribisha kwa sauti bila kunigeukia alitoka mtoto mmoja wa kiume ndani ndio akaja kunipokea getini...wakati anakuja mama akamwambia kimbia kampokee mgeni ila mama hakugeuka pia aliendelea kuandika.
Akasema ingia ndani nakuja...nikaingia mimi na mtoto. Akilini nilijua lazima atakuwa anaandika maandishi mengi kweli kwasababu alichukua muda mrefu na ni katika mlango wa mbele kabisa wa nyumba.
Mara akamwambia yule mtoto ampelekee maji ya moto...kwakuwa nilikuwa dirishani niliamua kuwa mmbea kuchungulia aliyafanyia nini yale maji...ila niliona tu akiyanawia mikono baada ya kumaliza kuandika.
Sasa wakati nikiwa mezani nikaona mezani maandishi yameandikwa habari za mambo ya urithi wa ardhi pamoja na nyumba....kisha nikaona. K + M+ B
Sasa baada ya kuongea kidogo nikamuuliza maana yake nini hiyo K + M + B ? Akanijibu kuwa tatizo letu hatumsikilizi wala kumjali sio Melkiory, Kaspary wala Baltazary. Nikabaki na mshangao kisha akaniambia flan (alimtaja jina) ameshakuja nenda kamfundishe.
Kisha yule mtoto huku akiniangalia akachukua zile karatasi akaondoka nazo kuelekea chumbani.
Baada ya kupigisha tuition kwasiku hiyo nikiwa naondoka nikaona pale mlangoni pamefunikwa na shuka.
Ila kesho yake nikaona K M B
Yule mama ni marehemu sasahv na amezikwa palepale nje kwake...karibu na Njake Petrol Station.
Naamini kabisa yawezekana wapo wanaomfahamu huku.
ILA, Mpaka leo hii nimeshindwa kuelewa alichokuwa anafanya na yule dogo sasahv ni mkubwa natamani nipate siku nimuhoji kidogo.
Niliwahi kugoogle mara kadhaa nikapata maelezo kuwa hao Kaspary, Melkior na Baltazary ni malaika waliokuwa wanajua habari za kuzaliwa Yesu kristo na walienda sambamba na wale Mamajusi wa Mashariki.
Pia baada ya kusoma kitabu kimoja nikagundua Malaika mmoja alienda INDIA ya leo, mwingine PERSIA (IRAN) na mwingine nakumbuka kama ni GREECE .
Mpaka leo hii wakristo wa nchi hizo wana siku rasmi ya kuwakumbuka Malaika hawa watatu.
SWALI LANGU: Hawa Malaika wanaabudiwa? Mbona sijawahi kusikia wakiongelewa makanisani?