GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Kwanza naanza kwa kuwapongezeni kwa juhudi zenu za kujiimarisha na kujijenga kimapambano kitu ambacho kimewafanya muwe Jeshi imara kwa ukanda huu wa maziwa makuu kitu kinachotupa jeuri ya kutukuka sisi Watanzania.
Ila kuna kitu kimoja nimekivumilia lakini naona sasa kimenifika na kama kawaida yangu huwa sipendi kukaa na dongo moyoni na natema nyongo yangu kwenu sasa.
Hivi kwani ni lazima haya mazoezi yenu ya mchakamchaka muwe mnayafanyia humu mijini na hasa katika hizi barabara zetu? Kwa mfano leo mmesababisha foleni kubwa barabara hii ya Mwai Kibaki zamani Bagamoyo kwakuwa tu Vijana wenu walikuwa wanakimbia mchakamchaka tena katikati kabisa ya barabara.
Kwanini mnatutesa hivi lakini? Kwani humo makambini mwenu hakuna viwanja vya mazoezi? au kwanini basi hata kama mnataka kuyafanya hayo mazoezi yenu msiamue tu muwe mnayafanya usiku wa manane myamalize ili sisi tunapopita asubuhi msituwekee foleni isiyokuwa ya lazima na hata kutusababishia kero zingine?
Halafu naomba tu nitoe RAI kwa Uongozi wa hivi vikosi kuwa wajitahidi kuwahimiza hawa Wapiganaji wetu wawe wanaimba nyimbo za ukombozi na zile za uhamasishaji za kizalendo kuliko hizi wanazoziimba sasa wakiwa wanakimbia mchakamchaka humu pembezoni mwa barabara.
Kwa mfano leo wakati wanakimbia na kuimba Wapiganaji hawa walijigawa katika makundi matatu ambapo lile kundi la mbele kabisa lilikuwa linaimba nyimbo ya Koffi Olomide ya SELFIE na kuna mahala walikuwa wanaserebuka kabisa na kukata mauno ( imagine hao ni WAPIGANAJI ) kundi la nyuma yake nimesikia kabisa likiimba wimbo wa SEGERE huku lile la tatu likiimba KISINGELI nikabaki najiuliza maswali mengi kuwa pengine huko vitani mnapokuwa mnaenda kwanza huwa mnaanza vita ya kucheza miziki na kukata viuno na mkishindwana ndiyo mnazichapa za kweli kweli sasa.
Tafadhali JWTZ hili lifanyiwe kazi kwani kiukweli mnatusababishia foleni humu njiani na mnatuboa kama siyo kutuchosha pia. Otherwise sina mashaka na UTENDAJI wenu uliotukuka katika MEDANI za KIVITA na tunawaombeni sasa muende pia SOMALIA mkawamalize Al Shabaab na mkimaliza hapo si vibaya mkaomba kwenda NIGERIA mkapambane na BOKO HARAM na si vibaya kama pia mtaomba kwenda SYRIA kuwamaliza ISIS ili dunia nzima ITUTAMBUE na ITUHESHIMU.
Naomba kuwasilisha.......