anjo
JF-Expert Member
- Jun 13, 2009
- 299
- 97
Moderator, napenda kuanzisha topic hii muhimu sana kwa nchi na wananchi wetu kwa sasa na siku za mbeleni.
Nchi yoyote lazima iwe na utaratibu wa kuchukua maamuzi magumu hasa yale yanayoweza kusababisha vifo kwa wananchi wake. Mawazo yangu ni kuwa nchi yoyote inaweza kumudu kupoteza hata mtu mmoja endapo interest za nchi zitavamiwa na nchi au kikundi kisichopenda maendeleo ya nchi.
Tumeshuhudia jeshi letu likipelekwa vitani Comoro bila ridhaa ya wananchi kupitia wawakilishi wao BUNGE. Je amiri jeshi mkuu hawajibiki kwa yeyote? Je, mwanajeshi anapokufa, familia itakuwa compensated vipi? Wanapata haki?
Kwa hivi sasa tumesikia jeshi letu linaelekea DRC na kwa jinsi ilivyo mpaka sasa hamna jitihada yoyote ya serikali kutaka ruhusa ya Bunge. Kwa kifupi, Bunge si kitu chochote juu ya maamuzi kama haya.
Japokuwa hakuna uharaka wa Amiri Jeshi Mkuu (Rais) kuchukua maamuzi ya kuamuru jeshi kupigana kutokana na kwamba nchi yetu haijavamiwa na interest zetu Kama nchi hazijaingiliwa ki hivyo; itakuwa busara kwa uongozi wa nchi yetu kufata taratibu zote za kutuma majeshi kwani kuna uwezekano wa kuhusika ki mapigano kama alivyoeleza Waziri Bernard Membe siku za nyuma kidogo.
Kuna uwezekano mkubwa kwamba jeshi letu chini ya Intervention Force under MONUSCO wanaweza kupigana na makundi ya waasi Mashariki mwa DRC Kama vile M23 na vikundi vingine vya Mai Mai. Kama kutakuwa na mapigano basi tuelewe wazi kuwa kutakuwa na baadhi ya majeruhi na vifo. Je, compensation itakuwa jukumu la nani? Je familia za hao wanajeshi watapata kiasi kinachotosha? Haya maswali na mengine mengi hayatakuwa na majibu kama Bunge halitahusishwa. Anayeona si tatizo aulize yaliyotokea Msumbiji. Ndugu wameshamaliza tofauti zao na watanzania waliokufa imekuwa historia.
Nadhani wabunge wana haki ya kuhoji vitu vingi hapa. Hivi suluhisho la mgogoro wa Congo ni lipi? Jeshi la Congo Lina wajibu gani na linakubalika kiasi gani kwa wananchi? Je hao waasi wana sababu za msingi kupigana au la? Je serikali ya Congo imejaribu kiasi gani kutatua matatizo ya watu wake? Je, Rais Kabila anakubalika kiasi gani hasa baada ya uchaguzi wa 2011 dhidi ya Etienne Tchisekedi? Tusiingie kusaidia yakawa kama ya msaada kwa Obote!
Mungu ibaraki Tanzania, asanteni kwa kusoma na kuchagia.